Sallam atoa ufafanuzi kuhusu utata wa nyumba ya Diamond ya Afrika Kusini

Sallam atoa ufafanuzi kuhusu utata wa nyumba ya Diamond ya Afrika Kusini

room

Member
Joined
Dec 28, 2015
Posts
61
Reaction score
102
Kuna nyumba ilikuwa sokoni inayofanana na ile Diamond amedai kuinunua South, zinafanana tu ama ni ile ile? Hilo ni swali ambalo hadi sasa wengi wamekuwa wakijiuliza, lakini sasa Bongo5 ina jibu la uhakika.

Wiki iliyopita Diamond Platnumz alitengeneza vichwa vya habari baada ya kupost kwenye Instagram picha ya nyumba anayodai ameinunua nchini Afrika Kusini itakayotumiwa na mchumba wake Zari.

Picha aliyopost Diamond Instagram kuelezea kuwa ni nyumba aliyonunua Afrika Kusini kama zawadi ya birthday ya mchumba wake Zari. Picha hiyo aliisindikiza na maelezo mazito yaliyowalenga wale aliowaelezea kama wanaopenda kujisifia ni matajiri na kumuita yeye maskini ilhali watoto wao bado wanaishi kwenye nyumba za kupanga.

Wengi walitafsiri kuwa dongo hilo lilimlenga ex wa Zari, Ivan anayefahamika kwa kuishi maisha ya kifahari. Hata hivyo, muda mfupi baada ya Diamond kuweka picha hiyo, wametokea watu ambao wamesambaza picha ya nyumba nyingine inayofanana kwa karibu asilimia 100 na nyumba ile iliyowekwa kwenye mtandao wa privateproperty.co.za na hivyo kuzusha minong’ono mingi.

Kwa mujibu wa meneja wa Diamond, Sallam, nyumba hiyo imelipiwa Alhamis iliyopita na tayari ni mali ya muimbaji huyo wa Salome na amefafanua kwanini bado haijatolewa kwenye tovuti hiyo.

“Nyumba imelipiwa thursday haiwezi toka muda huo huo kwenye website mpaka agency amalizane na mwenye nyumba then process zote zikamilike ndio inatolewa kwenye site,” Sallam ameiambia Bongo5.

Nyumba hiyo ipo Moreleta Park, mjini Pretoria. Ina vyumba vitano, lounge 3, mabafu matatu, bwawa la kuogelea, balcony, gereji mbili na nyumba ya pembeni ya kuishi wafanyakazi. Ipo kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba, 1068.

Bei yake si haba, ilikuwa inauzwa kwa Rand 2,480,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 396 za Kitanzania. Kuhusu anachokisema Diamond baada ya watu kudhani kawapiga changa la macho watanzania, Sallam amejibu, “Anachukulia kawaida, ni mengi kila siku yanasemwa.”

Hiyo ni sababu kubwa staa huyo ameamua kujizawadia mapumziko mahsusi visiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki.

Chanzo: Bongo5.com
 
hahahhaha... wajinga wengi nchi hii wanapungua kwa kasi.......usaniii wa hovyo unakaribia mwisho.
 
basi sawa!
Ooh Yes May be he did da Transaction online...and da documents signed by Zarina...As Mond is not seen in SA for more dan a month now...My Question to da Mond's manager is...Why they let Mond buy da property in Pretoria?...Closer to Ivan?...Or da powerful woman pressurized him to buy property closer to her beloved Ex?..
 
1. His wife (by law) is living in SA. And so his daughter....
2. Buying a house is a personal stuff... Domo and his management signed a deal concerning his music not his personal life
 
jina la hati miliki ni la nani? zisiwe kelele za tu za mitandaoni wakati mmiliki atakuwa mwingine kisheria

kutakapo kucha ndipo jamaa atajua kuwa alikuwa anatumiwa.
 
jina la hati miliki ni la nani? zisiwe kelele za tu za mitandaoni wakati mmiliki atakuwa mwingine kisheria

kutakapo kucha ndipo jamaa atajua kuwa alikuwa anatumiwa.
waganda wanauliza hivii
Omg i dint wana say anything about this but i also believe ivan en zari are in on all this.they are playing mond.something is really fishy.........how come ivadon already knew about moreleta park????? En why oa ivadon attacking mond supposed girlfriends?????..this drama is just playing in their favour so that mond buys zari that house.remember in SA ivadon en zari used to fraudulent rich pple en got money.....lets just wait en see. Anyway mond atleast got babies. At the end o f the day he will cover both zari en ivadon bills
 
Always stupind mind think negative.
 
Mh! sijui ni mimi sijaelewa? Nimesoma nyumba inafanana na ile aliyonunua Mondi, baadae nikakutana na mistari ya ukakasi kwamba haijatolewa kwenye mtandao kwa sababu process hazijakamilika. Swali langu ni Je, nyumba ile kwenye mtandao ndio hiyo iliyonunuliwa au inafanana tu kama anavyoelezea Menejeri Sallam?

All in all, hongera zake, kwenye mafanikio sio kila mtu atafurahia maendeleo yako, wakiwemo ndugu na watu unaofikiria ni wa karibu yako. Ni kuwa makini tu. Watu wengi wanaotuzunguka hawapendi mafanikio yetu, wengine wataonyesha chuki waziwazi wengine kimya kimya, siku umeanguka au ku kwama ndio utaona rangi halisi za watu.
 
mimi sio shabiki wa diamond wala mziki wake.

ila nataka kusema jambo moja, watanzania wote mnaohoji sana kuhusu diamond kununua au kutokununua nyumba SA ni "mapumbavu" in benjamin mkapa's voice.

Pesa za kwake, nyumba ya kwake awe amenunua au hajanunua ni yeye, sasa watu wanashupaa na ishu wakati hata mpango wa kuweka msingi nyumba zao hawana. Unajua roho mbaya na chuki ni sumu mbaya sana kwenye maisha, inafubaza akili hauwezi kuwaza vitu vya maendeleo. Can you imagine mtu anaumia kisa kasikia mwingine kafanikiwa, seriously???
 
waganda wanauliza hivii
Omg i dint wana say anything about this but i also believe ivan en zari are in on all this.they are playing mond.something is really fishy.........how come ivadon already knew about moreleta park????? En why oa ivadon attacking mond supposed girlfriends?????..this drama is just playing in their favour so that mond buys zari that house.remember in SA ivadon en zari used to fraudulent rich pple en got money.....lets just wait en see. Anyway mond atleast got babies. At the end o f the day he will cover both zari en ivadon bills
Wor out ugandan pple.. let mond pay those bill bse he deserve to be a father.. good father look forward for his family and neither spending nor bullshitt.. keep it up platinum
 
Hivi south Africa unaweza kununua nyumba kwa TZS millioni 396? Tena Pretoria? mji mkuu wa south Africa? Hivi bei ya nyumba dar ni shs ngapi? kule mbezi beach?
 
We ndio hujui kweli..unaweza kwenda South Africa asubuhi jioni ukarudi....umeshawahi kupanda ndege wewe? Au unazionea angani tu?

Back
Top Bottom