Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
Katika gazeti la Mtanzania 21/09/2010 imeandikwa kwamba Mama Salma amesikitishwa na kuangushwa kwa Mwantumu Mahiza, Naibu Waziri wa elimu. Kwenye Majira 21/09/2010 Mama Salma anasema kuwa WAMA Foundation inapeleka watoto watano (5) yatima shule na kwenye vyuo mbalimbali kutoka katika kila mkoa. Hivi hizo fadha za kupeleka hawa watoto sio zilikuwa zinatoka wizara ya elimu kwa msukumo wa Mwantumu kweli kinyume na sheria? Unasikitika vipi kwa Mwantumu kutogombea kama hakuna maslahi binafsi? Si umwambie JK kama akishinda amteue mbunge?