Pre GE2025 Salma Kikwete: Atoa Pole kwa Wananchi wa Mchinga kutokana na Athari za Mvua zinazoendelea

Pre GE2025 Salma Kikwete: Atoa Pole kwa Wananchi wa Mchinga kutokana na Athari za Mvua zinazoendelea

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Ndugu zangu wananchi wa Mchinga,

Napenda kuchukua fursa hii kuwapa pole kwa changamoto zinazotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika jimbo letu. Tunatambua kuwa mvua hizi zimeleta athari kwa familia zetu, makazi, na shughuli za kila siku. Hata hivyo, napenda kuwahimiza kuwa na utulivu na mshikamano katika kipindi hiki kigumu.

Ni muhimu kuendelea kuchukua tahadhari ili kujilinda na madhara zaidi yanayoweza kusababishwa na mvua hizi. Naomba tuendelee kufuatilia taarifa za hali ya hewa na kufuata ushauri wa wataalam wa usalama. Wale wanaoishi maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua hatua za kujihami mapema na, inapobidi, kuhama kwenda maeneo salama.

Katika kipindi hiki, tushikamane kama jamii na kuwasaidia wale waliokumbwa na athari kubwa zaidi. Umoja wetu na mshikamano wetu ndiyo nguzo muhimu ya kushinda changamoto hizi.

Tunaamini kuwa kwa msaada wa Mungu na jitihada zetu za pamoja, tutashinda changamoto hizi na kurejesha hali ya kawaida katika maisha yetu. Muwe na imani, na msikate tamaa — kuna nuru baada ya giza.

“Mchinga Kuchele, Tusongembele”

 
Back
Top Bottom