Salma Kikwete: Ni nani?


mkuu mm nasema ni kujikomba kwa wabongo kwa mkuu mpaka wanasahau majukumu yao
 
vipi wewe bana!!! Michele Obama huwa hapati hivyo ulivyouliza?

First lady yoyote duniani ana haki zake na nafasi yake katika nchi ikiwamo hizo hadhi na nafasi... hiyo hadhi ina-extend hadi watoto wa marais

Kuna haja ya kujua protocols za viongozi ili jamii ielewe zaidi
 
......
Yeye ni first lady sawa. Lakini hawajawahi kuapa kikatiba kama kiongozi sasa kupewa taarifa au kufanya kazi za kiserikali si ndio hayo hayo? anavunja katiba na sheria zetu. .......



Ni vema hili jambo likaangaliwa kwa upande mwingine.

Kama Salma hajaomba kusomewa hizo risala, wenye kiherehere na wasiojua majukumu yao, na wasiojua wanawajibika kwa nani watakuwa hao wenye kumsomea risala za maendeleo.

 

Hapa ndugu inabidi upewe elimu ya uraia yaani 'civics' Kwani hufahamu wewe kuwa ulipompigia kura Kikwete kuwa Rais ndipo ulipompigia kura Mama Salma Kikwete kuwa 'First Lady'. Au unafikiri ni suala la utashi wa mtu binafsi kuamua majukumu na haki za mke wa Rais?

Kama wataalam wa 'political science' humu jamvini na wataalam wa sheria wana wakati watakusaidia kielimu. Lakini inategemea na makusudi uliyo nayo katika kuuliza swali, kama lengo ni kujifunza ninaamini utafundishwa tu.
 
huo ni ufafanuzi maridhawa......kila mtu anahusiana kindugu na Kikwete nnchi hii anataka kuwa kiongozi, kweli haya mambo ni ya ajabu sana.
 
Na sasa anaelekea Kilimanjaro ambapo atapokelewa kwa nderemo,hoihoi, vigelegele na vifijo na UWT!
 
jamani hii ni tanzania zaidi ya uijuavyo akuna mwenye kujua itifaki zaidi jamani maana hili swala ni kubwa zaidi ya tunavyoliona au ni kujikomba kwa wahusika kwa mkuu wa nchi mana watz kwa kujikomba atujambo
...Tz jamhuri ya MABWEGE!!!! wachache sana wana akili timamu, waandishi wote wa habari ni mabwege!!
 
Tusisahau pia aliwahi kulishika Kombe la Dunia kinyume na utaratibu wa FIFA, hata kufikia hatua ya kuzuiwa na moja ya wasindikizaji wa kombe hilo:

 
Ni mbwembwe zisizo na sababu wala lazima ambazo zinaligharimu Taifa fedha nyingi ambazo zingeliweza kutumika kwa kuwasaidia na kuwapatia huduma za jamii mamia ya akina mama na watoto. Priorities!
 
Tusisahau pia aliwahi kulishika Kombe la Dunia kinyume na utaratibu wa FIFA, hata kufikia hatua ya kuzuiwa na moja ya wasindikizaji wa kombe hilo:

mama kuwa kilaza wala haina mjadala....ni kilaza kwelikweli.....mzungu wa reli.
 
Kule kwa Mswati kumbukumbu zangu kama hazijapotea zinaniambia mama alienda na dege la rais kule. Hapa sasa hivi naona amekuwa nae kama ni mtumishi wa umma, hivi je nae anapata posho? maana walinzi wake wote wanakula posho yeye je inakuwaje?
 
Anapaswa kudhibitiwa anakiherehere sana kuna wakati huwa anataka awe mbele ya Raisi haswa wanapotoka nje ya nchi utakuta anataka kuongoza msafara mbele kabla ya Raisi nadhani watu wa protokali watakuwa wamemshindwa haelewi kitu yule,mapepe mukichwa,tunajua ananafasi yake kama FL lakini hili la kutenda kazi za watendaji wa serikali mimi hapo nitapinga mpaka mwisho hastahili na najua atakuwa ameonywa ila asikii huyo
 
Nionavyo kuna kila sababu ya kuliangalia upya swala la kila First Lady kuanzisha NGO na kuondoka nayo amalizapo muda wake. Mtu akifanya tathmini ataona huwa malengo ya kuanzishwa hizo taasisi hayatofautiani sana. Kwa nini isianzishwe taasisi moja (nje ya serikali) ambayo mke wa Raisi atakayekuwepo madarakani atairatibu utendaji wake na muda wake ukiisha amkabidhi mwenzie? Tatizo ni kuwa nyingi hutegemea wahisani na kama sivyo, hela za walipa kodi.
 
Nadhani huyu mama kwao ni Singida kama sikosei!
wewe utakuwa Muha bila shaka....umequote kuwa anatoka lindi halafu unaleta tetesi juu ya confirmation kuwa anatoka Singida.....
huyu mama ni wa Lindi mkuu.
 
Wakuu Heshima Mbele,
Kiukweli Mke wa Rais anazohaki zake, Mfano haki ya kuwa na usafiri, haki ya kuwa na ulinzi , Kama ambavyo watoto wa Rais wana haki ya kupewa ulinzi pale inapobidi. Kule Marekani shule wanazosoma watoto wa Marais ni eneo maalum la ulinzi, na wale watoto wamepewa secret code za Ulinzi na C.I.A. ,Mfano Obama ni Renegade, Michele ni "Renaissance",Malia Obama's ni "Radiance," na Sasha Obama's ni "Rosebud." ili tu kuimarisha mawasiliano ya kiulinzi kwa emeregence.
Tatizo lililopo ni kwenye mipaka ya kazi, Mke wa Rais anaweza kushiriki kwenye shughuli za kijamii, lakini hii haiko kikatiba kwamba mke wa rais atafanya nini KATIKA KIPINDI CHA URAIS WA MUMEWE, mfano wakati Mkapa anaingia Ikulu Anna alikuwa afisa pale UNICEF, Aliacha shughuli zake na kuanzisha NGO yake ya EOTF.Huyu mama yetu sasa na yeye ana WAMA. Sijui huyo atakayekuja atakuja na kitu gani? Lakini iwepo mipaka Kisheria inayompa mke wa Rais kazi za Kufanya. kama ni Taasisi ijulikane na kila mke wa Rais anayeondoka madarakani aiache ili yule anayeingia aitumie ,Lakini pia ifahamike source ya Funds.
 
ndo maana tunahisi kuwa anatupa hasara kwa matumizi holela ya pesa za walipa kodi wetu masikini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…