Mkoa wa Mara, unapata shida ya kuendelea pamoja na historia kubwa iliyo nayo, shida mojawapo ni kupata mkuu wa mkoa wenye sifa stahili ya kuwa mkuu wa mkoa.
Mfano dhahiri wa ombwe la uongozi katika mkoa wa Mara ni aina ya RC aliye madarakani. How on earth ... Mkuu wa mkuu wa mkoa anasoma taarifa kwa First Lady... Inamaanisha huyu RC hajui anawajibika kwa nani!!
Kwa vile First Lady, anaishi nyumba moja moja na mkuu wa kaya, anafikiri kuwa First Lady ni sahihi kupokea taarifa na ataifikisha kwa mkuu wa kaya..... haa haaa. Hii inanikumbusha Lucy Kibaki , anavyowaingilia na hata kuwapiga vibao watendaji wasiojitambua kule Kenya. Huyu mkuu wa mkoa ni aina ya viongozi ambao mke wa kiongozi anaweza akawafanya lolote, kwani ni watupu! tupu! tupu!
Hebu sikiliza alichosema huyu First Lady, anawambia watu wa Tarime waache kuoa wake wengi!!! Ndiyo maana alihitaji ulinzi wa FFU, kwani alikuwa anasema mambo ambayo si kipaumbele kabisa cha watu wa Tarime.
Inamaanisha, huyu First Lady hajui shida zinazowakabili wana Tarime?
Angekuwa First Lady makini na kutumia taasisi yake ya WAMA, angegusia ukosefu wa maendeleo unaotokana na wamama wa Tarime kufukuzwa katika maeneo yao ya ardhi kwa kupisha shughuli za uchimbaji mkubwa wa madini, ukosefu wa amani na jinsi mambo haya yanamwathiri mwanamke wa Tarime. Hawa wamama , wanahitaji msemaji na mtu ambaye anatambua matatizo yao.
Matatizo yao ni kukosa ajira, shughuli endelevu na yeye angewapa moyo na jinsi gani taasisi yake inaleta jambo la faraja au nuru mpya kwao. Lakini First Lady , wetu amefikiri kama mwanasiasa wa kitanzania, ambao huwa hawana lolote la kusema , bali kusema chochote alimradi kasema.
Kama Salma anapinga kuoa wake wengi je anaupinga uislam? Je mbona na yeye yupo katika ndoa ya wake wengi????