Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Mbunge wa Jimbo la Mchinga na mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete, amesema kuwa moja ya kumbukumbu asizoweza kusahau maishani mwake ni wakati wa kuhesabiwa kura hadharani alipogombea ubunge.
Akizungumza leo Machi 5, 2025, katika kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Halmashauri ya Chalinze, Mama Salma amesema kuwa hatua hiyo ilikuwa sahihi ili kuondoa shaka kuhusu ushindi wake.
"Kitu ambacho sitasahau maishani mwangu wakati nagombea nafasi ya ubunge ni kuhesabiwa kura hadharani. Niliona ni jambo sahihi kwa sababu kama tungehisabu ndani, wangesema nimeshinda kwa kura za itifaki," amesema Mama Salma.
Source: Nipashe