Salum Mayanga: Sina upendeleo kwa wachezaji wa Simba

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars, Salum Mayanga amesikitishwa na uongo unaoendelea kusambazwa mitandao kuwa anawachukia wachezaji kutoka Yanga huku akiwabeba zaidi wachezaji wa Simba kwenye kikosi chake.

Mayanga amesema taarifa hizo amezisikia tuu kutoka mitandaoni ila hajui wanaomzushia wana ajenda gani dhidi yake kwa hajawahi kuletewa malalamiko na Viongozi wa klabu hizo.

Hizo taarifa nazisikia sikia tuu kutoka kwenye mitandao lakini sijawahi kuletewa malalamiko na kama kuna mtu anasambaza ujumbe huo basi ni chuki tuu, Sina upendeleo kwa wachezaji wa Simba wala Yanga “,amesema Mayanga kwenye mahojiano yake na Radio ABM FM.

Mayanga amesema haijawahi kutokea kupendelea timu moja zaidi ya kuangalia kiwango cha mchezaji husika kwani hata alivyokuwa Kocha msaidizi alimshauri Kocha wa kipindi hicho, Mart Nooij kuchukua wachezaji 9 kutoka Yanga kutokana na uwezo wao kwa kipindi hicho.

Nakumbuka kipindi kile wakati nilipokuwa msaidizi wa Mart Nooij mimi ndiye niliyemshauri tukateua wachezaji 9 kutoka Yanga, Wanayanga waukubali ukweli juu ya kikosi chao, angalia beki wa kati, alikuwa Bossou, kwenye viungo kuna Kamusoko na Niyonzima, wakati safu ya ushambuliaji ni Ngoma, Tambwe na Chirwa, pale nifanyeje kama si kunionea?”,alimaliza Mayanga kwa kuhoji.

Kocha huyo wa Stars amesema kwa kutambua upungufu kwenye safu ya ulinzi, alimuomba Kelvin Yondani aje kuimarisha nguvu lakini beki huyo aliombwa aachwe ili akamilishe kwanza mipango ya ndoa yake.

Mayanga aliongeza kwa kusema kuwa inakuwa vigumu kuwaita Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haji Mwinyi, Salum Makapu na Aggrey Morris baada ya Zanzibar kupata uanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Taifa Stars wikiendi iliyopita ililazimishwa sare ya goli 1-1 na timu ya taifa ya Rwanda mchezo uliopigwa kunako dimba la CCM Kirumba.

Chanzo: Bongo5
 
Cha msingi asing'ang'anie kuchukua wachezaji wa Yanga na Simba tu! Timu zipo nyingi anaweza akapata wachezaji wazuri kibao!Kila siku wanawatumia wachezaji wa Yanga, Simba na Azam na timu inaboronga kwa nini wasijaribu kwingine? Kuna timu ya taifa iliitwa Kakakuona miaka ya zamani iliundwa na wachezaji walioonekana wakawaida lakini ilifanya vema kuliko hata stars iliyoundwa na mastaa kibao! Hata hivyo Mayanga hatoshi kuwa kocha mkuu wa Taifa stars!

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu lakini akifanya hivyo na bado timu ikayumba kabla hawajakomaa si ataambiwa hakuna kujaribu?
 
Juma Abdul, Kaseke, Ajib, na Yondan uwezo wao haujawahi kushuka hata siku moja ukilinganisha na akina Kichuya, Muzamil, Mkude ambao wanabahatisha tu uwanjani. Mayanga una jambo
 
Juma Abdul, Kaseke, Ajib, na Yondan uwezo wao haujawahi kushuka hata siku moja ukilinganisha na akina Mwashuya, Muzamil, Mkude ambao wanabahatisha tu uwanjani. Mayanga una jambo
Kweli aisee...analialia tu huyo kocha. Hata Dante yuko vizuri tu.
 
Huyu kocha bwege sana,unaacha washambuliaji wa maana unamchua John Boko? kama sio upuuzi ni nini?
 
Juma Abdul, Kaseke, Ajib, na Yondan uwezo wao haujawahi kushuka hata siku moja ukilinganisha na akina Mwashuya, Muzamil, Mkude ambao wanabahatisha tu uwanjani. Mayanga una jambo
Undeni timu yenu ya taifa ya wachezaji wa vyura pekee kama hamjapigwa hamsa au week kabsa kama kule Algeria-stars yenye kikosi Cha kandambili 0 vs 7 Algeria!

Pogba wa tz nchi imekushinda!
 
Juma Abdul, Kaseke, Ajib, na Yondan uwezo wao haujawahi kushuka hata siku moja ukilinganisha na akina Mwashuya, Muzamil, Mkude ambao wanabahatisha tu uwanjani. Mayanga una jambo
Anamchukua Ndemla ambaye hana namba ya kudumu kwenye timu yake

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Ajib ni muda mrefu tok akiwa simba hakuwa na namba taifa stars. Sasa si kwa sababu kahamia yanga ionekane ni majungu.tuacheni uswahili mimi ni mwanamichezo tatizo letu waswahili tuna majungu sana. Yondan na mwashiuya mara ya mwisho wamechezea taifa stars lini?
Juma Abdul, Kaseke, Ajib, na Yondan uwezo wao haujawahi kushuka hata siku moja ukilinganisha na akina Mwashuya, Muzamil, Mkude ambao wanabahatisha tu uwanjani. Mayanga una jambo
 
Sasa mkuu mbona hawa tunaowaona wazoefu ndio kila siku wanatutia aibu?

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
Tatizo letu ni kuamini kwamba tayari tuna timu nzuri kwa sababu tu wachezaji na makocha wetu wanaonekana kufanya vizuri kwenye Ligi yetu. Hicho si kigezo sahihi maana kila Ligi duniani wachezaji na makocha wao huonekana kufanya vizuri. Lakini Je, Ligi yetu ni bora kuliko nyengine? Je wachezaji wetu au wanaon'gara kwenye Ligi yetu wanafanya vizuri nje ya Ligi yetu? Je kuna mocha wetu yeyote aliyefanya vizuri nje ya Ligi yetu?Ukiwachilia Samatta (ambaye naye tunampaisha zaidi kuliko uwezo wake halisi) na Nonda Shaaban, jawabu ni hapana. Akina Said Mwamba, Issa Othman, Othman China (Daraja la nne UK), Talib Hilal, Ahmad Amasha walishindwa kuwika angalau kwenye Ligi za Arabuni. Sunday na Kassim Manama, Boniface Njohole waliishia kuwacha historia kwamba walicheza Ulaya. Haruna Moshi na Emmanuel Okwi ndio wameshindwa kabisa. Kwa hivyo Ligi yetu si bora na wachezaji au makocha wetu si mahiri kama tunavyojidanganya. Ndio maana Ngoma asiye na namba kwenye timu ya kwao ya Taifa watu wanajilaumu kwa nini si raia wetu ili achezee timu ya Taifa. Hapo ndio pa kuanzia.
 
Issue siyo wachezaji wa Yanga kuachwa, issue ni uteuzi mbovu wa Stars.
Undeni timu yenu ya taifa ya wachezaji wa vyura pekee kama hamjapigwa hamsa au week kabsa kama kule Algeria-stars yenye kikosi Cha kandambili 0 vs 7 Algeria!

Pogba wa tz nchi imekushinda!
Taifa Stars pekee iliyoshiriki CHAN iliundwa na wachezaji wengi wa timu ya wananchi. Mikia FC haina rekodi ya wachezaji wake kufanya vizuri kwenye timu ya Taifa.

Wahenga wa kale walisema: 'Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake'. Mnyonge akiisha nyongwa hawezi kupokea haki tena, mimi Makoye Matale (Mhenga wa sasa) nasema:

Mnyonge mpeni haki yake kwanza ndipo mnyongeni!
 
Hakuna kikosi kilichocheza CHAN kikiwa ni kikosi cha yanga! Tunapaswa kumwachia kocha nafasi ya kufanya kazi. Yanga kwa sasa haina wachezaji wakuchezea stars. Hao kina Dante, mwashuya na Yondani wananini. Tuache kikosi cha vijana kicheze. Upuuzi huu mnaoendekeza ndio matokeo yake kupigwa 7-0. Timu ni nzuri wachezaji wajitume tu.
 
Acha porojo wataje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…