TANZIA Salum Shamte wa Katani Ltd afariki dunia

TANZIA Salum Shamte wa Katani Ltd afariki dunia

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
1585546449212.png


Mkurugenzi wa zamani wa Katani Limited Salum Shamte amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Oktoba 31, 2019, Salum Shamte pamoja na wenzake akiwemo Juma Shamte ambaye ndiye Mkurugenzi wa sasa wa Katani Limited na mjumbe wa bodi, Fatma Diwani walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga wakikabiliwa na mashtaka matatu.

Walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya Sh1.14 bilioni kwa vyama vya msingi vya ushirika (Amcos).

Mapema mwezi Machi 2020, Waziri Mkuu alipokea ripoti iliyozidi kumweka pabaya Shamte (kimsingi ripoti pia inamweka pabaya zaidi Dr. Dau aliyekuwa NSSF); isome hapa chini:

WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA TIMU YA UCHUNGUZI WA ZAO LA MKONGE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya uchunguzi wa tuhuma mbalimbali katika kilimo cha mkonge mkoani Tanga na kuagiza mapendekezo yaliyotolewa na timu hiyo yakiwemo ya kurejeshwa Serikalini kwa nyumba na. 176 eneo la Bombo ambayo ilimilikishwa kwa Bw. Salum Shamte yafanyiwe kazi.

Nyumba nyingine zilizopendekezwa kurejeshwa Serikalini ni pamoja na nyumba 10 zilizoko ndani ya Jiji la Tanga katika maeneo ya Raskazoni, Bombo, Nguvumali na Mtaa wa Market ambazo zilinunuliwa na watumishi hao kwa udanganyifu.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Machi mosi, 2020) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri za mkoa wa Tanga, viongozi wa taasisi mbalimbali, wadau wa zao la mkonge pamoja na viongozi wa dini kwenye ukumbi wa hoteli ya Naivera.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wawekezaji ambao wanamiliki mashamba ya mkonge yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 2,000 ambao hawajayaendeleza wayaendeleze wakishindwa yatachukuliwa na kugawiwa kwa wananchi.

Timu hiyo maalum ya uchunguzi iliundwa na Waziri Mkuu na ilifanya uchunguzi mkoani Tanga kuanzia Novemba 29, 2019 hadi Februari 7, 2020. Timu hiyo iliyokuwa na wajumbe 13, ilihusisha maafisa kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.

Uchunguzi huo maalum ulihusu masuala mbalimbali katika tasnia ya zao la mkonge mkoani Tanga ambayo ni pamoja na uzalishaji wa mkonge, bei ya zao la mkonge katika soko la ndani na nje ya nchi.

Pia ilichunguza kuhusu mali za iliyokuwa Mamlaka ya Mkonge Nchini, ubia kati ya Kampuni ya Katani Limited na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Utendaji kazi wa Kampuni ya Katani Ltd na pia Utendaji kazi wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB).

Awali, Mwenyekiti wa timu hiyo, Bw. Gerald Kusaya alisema timu ilibaini kuwa Kampuni ya Katani Ltd tangu mwanzo ilikuwa na mgongano wa kimaslahi na kusababisha uhujumu uchumi kwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wake, Bw. Salum Shamte alikuwa mtumishi wa umma na alishiriki vikao vyote vya ubinafsishaji wa Mamlaka ya Mkonge ilhali akijua kuwa ana maslahi kwenye kampuni anayoinunua.

Uchunguzi umebaini kuwa viongozi na wanahisa wa Katani Ltd waliohusika kuingia mikataba walikuwa watumishi wa Mamlaka ya Mkonge wakati wa mchakato wote wa ubinafsishaji, hivyo walitumia vibaya madaraka yao kwa kuishawishi Serikali kuingia mkataba huo usiokuwa na tija kwa Serikali bali kwa manufaa yao binafsi. Hivyo, timu imeandaa taratibu kwa ajili ya wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.”

Bw. Kusaya amesema timu hiyo inapendekeza kuwa Serikali itoe fedha kwa ajili ya kazi ya kuyapima upya mashamba matano ya Mwelya, Ngombezi, Hale, Magunga na Magoma ili wananchi wanaoendelea kutumia mashamba hayo kwa kukodishwa na Bodi ya Mkonge kama ilivyokubalika kwenye Baraza la Mawaziri mwaka 2005 ili waweze kupewa hati ndogo (leasehold tittle).

Alisema timu inapendekeza nyumba 30 zilizopo eneo la Muheza, ambazo baadhi zilitolewa kwa wananchi waliokuwa watumishi wa Mamlaka ya Mkonge na baadhi kuachwa kwa ajili ya makazi ziendelee kuwa mali ya wananchi hao kwa kuwa eneo hilo kwa sasa lipo chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.

Nyumba 22 zilizoko ndani ya mashamba ya mkonge na maeneo ya kiwanda cha TANCORD ziendelee kubaki mali ya Serikali na nyumba iliyoko katika kiwanja Na. 176 eneo la Bombo iliyohamishwa kwenda kwa Ndg. Salum Shamte irejeshwe Serikalini kwa njia ya urekebishaji wa daftari la Msajili wa Hati.”

Kwa upande wao, viongozi wa mkoa wa Tanga wakiwemo wabunge wamemshukuru Waziri Mkuu kwa kuunda timu hiyo ya uchunguzi wa zao la mkonge kwa kuwa mapendekezo yake yamejibu changamoto zilizokuwa zinalikabili zao hilo.

Wamesema mapendekezo yaliyotolewa na timu hiyo yanakwenda kufufua kilimo cha zao la mkonge hivyo kuongeza tija kwa wakulima wa mkonge mkoani Tanga.
 
Tutaiba, tutadhulumu, tutafanya yooote, mwisho wa siku tunaondoka tukiwa watupu tunarudi Mbinguni kwa Mungu aliyetuumba.

Twendeni kwa tahadhari.

Pumzika Shamte!

Sent using Jamii Forums mobile app
Lile kundi la Wafanyabiashara wazawa linazidi kuyoyoma.......Mengi, Mafuruki, Idd Simba na sasa Shamte.
 
Nenda mwanakwenda Shamte. Ulimdhulumu sana Uncle wangu, akawa demoted, wewe na akina Marehemu Ibrahim Kaduna, mkamfanya aishi maisha magumu na ya stress sana. Mkadhulumu haki miliki za tafiti zake, aligundua jinsi ya kutengeneza pombe kwa kutumia maji ya mkonge, chakula cha kuku kwa kutumia mabaki ya mkonge na umeme kwa kutumia maji maji ya mkonge.

aliandika vitabu kuhusu mkonge lakini hakufaidika navyo. Alinieleza haya 2007 na mwaka huo huo akapata stroke, nilimuuguza Tanga, mkashindwa kumlipia hata Ambulance kutoka Tanga to Muhimbili.

nilipowatafuta kwa ajili ya matibabu yake mkaishia kunipa Tzs 50,000. Mzee Shamte unakumbuka siku ile uliniita pale fire? Ukampa dereva bahasha yenye hio pesa?
Baadae ali-recover bado mkagoma kumlipia bill, na MKUMBUKE alistahili sio kwamba ilikua fadhila.

Siku moja jioni ya 12 tukiwa tumerudi kutoka kwenye mazoezi ya viungo pale Morocco Physiotherapy clinic, STARTV wakawa wanaonyesha kipindi cha mkonge na walionyesha hizo products ambazo huyu mzee wangu ndio alikua amwzifanya yeye ila zilitangazwa kama vile ni kazi iliyofanywa na mtoto wa Shamte. Kwakuwa nilikua nine Shaun vanish a dots, nikachukua remote nikataka kubadili Chanel, ananiambia nisiondoe.

Next day akiwa kwenye mazoezi napata second stroke na ndio ikawa mwisho wake. Akina Shamte bado walishindwa hata kumsafirisha.

sina nia mbaya, kifo ni kifo but kwa kusema haya naamini nimemtendea haki Marehemu Mentor wangu. He was a true friend of Mine.
 
Back
Top Bottom