Salute to women

Kaka Sam

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2009
Posts
540
Reaction score
78
Kuna tukio nililiona MAISHANI:
Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote;
IMAGINE:

ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!

UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!

UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.

UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!

CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!

UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!

UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!

Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!

HIVI INGEKEWA WANAUME
TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?

Kwa leo acheni tu niwape

heshima zao wanawake wote:

I SALUTE AND LOVE THEM WOMEN!
 
Bro D5 hii kuna mtu aliiweka ikadisikasiwa jana au juzi mambo mengi kichwani
The unit ...uwe na weekend njema
 
Umeirudia tena hii kitu? tena ume copy paste kwa michuzi!
 
Mpwa uwe unazikagua thread kabla ya kutuma....mwenzio kabandika jana hii...wakati ilishawekwa hapa jamvini na Xpin muda kidogo!!
 
Where is CHRISPIN mzee ya Valuuuuuuuu na Pick-up?????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…