Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 224
- 236
Anaandika Mo Mlimwengu
Ukisikia la mgambo ujue tayari kuna jambo, ni simanzi na majonzi kubwa kwa Namibia na bara la Afrika kuondokewa na mwanamapinduzi halisi. Sam Nojuma alizaliwa mnamo 12 Mei 1929 kijiji cha Etunda, Ongandjera, Ovamboland Kaskazini mwa Namibia. Ametoka kwenye kabila la Ovambo ambalo ni jamii yenye watu wengi zaidi kwa Namibia. Alizaliwa kwenye familia ya wakulima hivyo alianza kujihusisha na kilimo tangu akiwa mdogo.
Safari ya elimu ya Sam Nojuma alianzia shule ya Omangundu Mission School kwa masomo ya Msingi baadae akaendelea na shule za Misheni ambazo zilitoa elimu kwa waafrika enzi za ukoloni. Hakuweza kuendelea zaidi na shule kutokana na sababu za ufukara wa familia yao.
Mwaka 1946 aliacha shule na kuhamia mji wa Walvis Bay na kuanza kufanya kazi ya kuwa kondakta wa treni kwenye kampuni ya reli ya South Africa.Kufanya kazi kwenye reli ndio kulikochochea kuanza harakati za ukombozi baada ya kuguswa na ukandamizaji wa kikoloni uliyofanywa na wazungu hasa hasa ubaguzi wa rangi.
Sam Nujoma alianza harakati za ukombozi akiwa kwenye vyama vya wafanyakazi vilivyokuwepo wakidai haki zao. Kulikuwa na ubaguzi wa rangi uliyopindukia baadae wakaanzisha chama cha OPO( Ovamboland People's Organization) . Mwaka 1959 aliongoza maandamano dhidi ya mpango wa serikali ya wakoloni ya kuwahamisha kwa nguvu wakazi wa eneo la Windhoek Old location kwenda Katutura. Kwenye hayo maandamano watu walipoteza maisha na hili tukio lilijulikana kama Windhoek Massacre.
Mwaka 1960 alianzisha chama cha SWAPO ambacho kilitambulika kama chama kikuu cha ukombozi wa uhuru kwa Namibia. Kumbuka chama hicho kilionekana tishio kwa wakoloni akaanza kutafutiwa vipingamizi na kukamatwa ili kuzuia harakati za ukombozi. Ndani ya mwaka huo wa 1960 alikimbilia uhamishoni kwa kwenda nchi za Botswana, Tanzania, Angola na Zambia.
Vita ya ukombozi siyo shughuli ndogo aliweza kukaa uhamishoni kwa kipindi cha miaka 29 hadi kupata uhuru.Mwanaume huyo alisimama kidete kuhakikisha taifa lake analikomboa. Akiwa uhamishoni aliendeleza harakati za ukombozi ambapo SWAPO walianzisha jeshi la ukombozi lililoitwa PLAN( People's Liberation Army of Namibia). Sam Nujoma akiwa uhamishoni alipambana kutafuta msaada wa silaha za kijeshi na jeshi lake kupata mafunzo ambapo hata kwa Tanzania walitoa msaada wa kutosha kwenye jeshi lao La PLAN.
Nchi nyingine ambazo zilisaidia kutoa msaada wa silaha za kijeshi ni nchi za kisovieti kama Russia, China na Cuba. Mwaka 1966 vilianza vita rasmi vya ukombozi kwa kupeleka mashambulizi kwenye jeshi la Afrika Kusini katika eneo la Omugulugwombashe. Hili tukio ndio liliashiria mwanzo wa vita ya ukombozi wa Namibia.
Sam Nujoma alishiriki vita ipasavyo akiwa nje ya nchi.Alisimamia mikakati ya PLAN akishirikiana kwa ukaribu na makamanda wa kijeshi wakina Peter Nanyemba na Dimo Hamaambo.Alijitahidi kuongoza mapambano akiwa uhamishoni kipindi yuko Zambia na Angola. Alikuwa akiratibu uingizaji wa silaha, mafunzo ya kijeshi na kuhamasisha misaada kutoka mataifa mbalimbali na kuliimarisha jeshi la PLAN. Aliendelea kuwahamasisha wapambanaji kwa kuwajenga kiitikadi na kuwapa motisha alipowatembelea kambini. Hata hotuba zake zilisadia kuwajenga kizalendo na kutokata tamaa dhidi ya wakoloni.
Alipambana kidiplomasia kwa kwenda kwenye umoja wa afrika wakati huo unaitwa OAU na kwenda UNO. Harakati za kidiplomasia zilisaidia hadi kuanzisha mpango wa UN Resolution 435, mpango huo ulipendekezwa mwaka 1978 kwa kuweka misingi ya uhuru wa Namibia kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Afrika kusini.
Mpango huo uliamuru jeshi la Afrika Kusini liondolewe nchini hapo na waliamuru kurudishwa wakimbizi waliokuwa uhamishoni ambao ni wanachama wa SWAPO warudi nchini pasipo kubugudhiwa wala kukamatwa na walitoa msukumo zaidi watu wafanye uchaguzi wa haki na uwazi pasipo kuingiliwa. Na hii ikapelekea SWAPO kushinda kiti cha Urais na kupata uhuru mwaka 1990 na Sam Nujoma kuwa Rais wa kwanza
Sam Nujoma anatambulika baba wa maridhiano, baada ya kuwa Rais alianzisha sera ya National Reconciliation Policy ( Maridhiano ya kitaifa) . Maridhiano hayo yalilenga zaidi kuunganisha taifa baada ya vita. Nchi ilikuwa imetawaliwa na ubaguzi wa rangi. Hivyo vita vikaacha vimeligawa taifa kwa misingi ya ukabila, rangi na itikadi za kisiasa.
Hivyo yalihitajika maridhiano kuweza kuponya majeraha na kujenga umoja.Maridhiano yalizingatia kuepuka visasi na machafuko. Kuna baadhi ya watu walikuwa wanashirikiana na wakoloni kuwakandamiza wanamibia wenzao. Kueupukana na hayo na ili kuweza kujenga taifa imara na thabiti kiuchumi. Sam Nujoma alikuwa akisema We must forgive but not forget(Tuwe tayari kusamehe lakini tusisahau).
Maridhiano yalibeba dhana ya utaifa na alitumia maridhiano hayo kujifunza kutoka kwenye mataifa mengine. Aliweza kuwapa mifano ya nchi kama Zimbabwe na hata Afrika Kusini chini ya Nelson Mandela. Hii ilipelekea kufungua milango ya wawekezaji wa ndani na nje na kuendeleza biashara.Maridhiano ni mojawapo ya alama kubwa ya uongozi wake kwenye taifa la Namibia.
Sam Nujoma aliamini kwenye kushirikiana na viongozi wengine wa mataifa mengine .Kuna viongozi ambao waliunga juhudi kwenye mapambano dhidi ya ukoloni na ubaguzi wa rangi.
Mwl Nyerere ni miongoni mwa watu ambao waliunga juhudi za ukombozi kwa nchi za kiafrika ikiwemo taifa la Namibia. Keneth Kaunda alitoa msaada mkubwa ukizingatia Zambia ndio kilikuwa kituo muhimu cha mikakati ya wanamapinduzi wa Zambia.
Agostino Neto naye ni mojawapo ambaye alitoa ardhi yake kuwa kituo cha operesheni za kijeshi dhidi ya wakoloni.
Oliver Tambo na na Nelson Mandela kupitia ANC walishirikiana na SWAPO kwa ukaribu zaidi kupambana na ukoloni maana adui yao alikuwa mmoja.
Robert Mugabe alikuwa mshirika mzuri kwenye kuunga juhudi ya vita dhidi ya wakoloni .
Fidel Castro jina lake litazidi kuenziwa na waafrika wengi kwa kujitoa kusaidia baadhi ya nchi za kiafrika kwenye kupambana na ukoloni,alisaidia sana mafunzo ya kijeshi, kutoa msaada wa silaha, na msaada wa moja kwa moja kwenye vita kama ya Cuito Cuanavale ambavyo vilisaidia sana kuharakisha Namibia kupata uhuru wake ukizingatia vita hivyo ilipiganiwa kusini mwa Angola ilipelekea jeshi la Afrika kusini kupigwa na kuondosha majeshi yake.
Sam Nujoma baada ya vipindi vitatu vya urais tangu 1990-2005 .Aliachia kijiti watu wengine waongoze nchi na hii ilimpatia heshima kubwa kwa kuheshimu katiba ya nchi na misingi ya demokrasia. Aliendelea kuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika nchi yake na barani Afrika. Kwenye chama chake cha SWAPO alikuwa kiongozi wa heshima na alishiriki shughuli muhimu zinazohusu chama chao.Aliendelea kuwa mshauri kwa Marais waliofuata hadi mauti yanamkuta.Kama mdau wa maendeleo alianzisha Sam Nujoma Foundation ambayo inajikita zaidi kwenye kusaidia masuala ya afya, elimu na vijana.
Hakuishia hapo aliendelea kutoa mihadhara baadhi ya vyuo vikuu kwa kutoa mihadhara juu ya ukombozi wa Afrika na uongozi kwa ujumla.
Aliandika kitabu cha wasifu wake kiitwacho " Where Others Wavered" ambacho kinaelezea maisha yake kwa ujumla na mapambano ya kupata uhuru wa Namibia.Nujoma alijipatia umaarufu kwa kutunukiwa na digrii za heshima( Honorary doctorates) kwa vyuo vya ndani ya Afrika na nje ya Afrika.
Mwisho Sam Nujoma aliendelea kuheshimiwa kama Baba wa Taifa la Namibia. Ni miongoni mwa marais ambao wanatambulika kama true sons of Afrika. Ni mfano kuigwa kwa maisha yake yote aliyawekeza kwenye ukombozi wa taifa lake na Afrika kwa ujumla.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Taifa limepoteza hazina lakini yote aliyoyafanya yatabaki kama urithi kwa kizazi na kizazi kwa Namibia na Afrika kwa ujumla.
#mlimwengumimi
#RIPSamNujoma.
#GwijiwaNamibia
#TruePanafricanist