Samahani Kwa Wabunge wetu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Samahani Kwa Wabunge wetu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

APA CHICAGO

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
259
Reaction score
292
Salaam kwenu wanabodi wa jukwaa hili kubwa na lenye heshima ndani na nje ya nchi yetu.Sio tu linaheshima lkn pia lina taarifa za kuaminika.

Nimeanza na neno samahani kwa wabunge wetu kwa sababu kelele zimekuwa nyingi sana huko bungeni wengi wa wabunge wanaopata nafasi ya kuchangia wamekuwa wakizungumzia masrahi ya wafanyakazio ikiwemo kupanda madaraja, mishahara na pension za wastaafu.

Kinachonishangaza kutoka kwa waheshimiwa hawa ni kuwa walikuwepo tangu awamu ya tano ilipoingia madarakani rasimi tangu 2016 hadi leo lakini walikuwa wanaimba mapambio ya Uhakiki wa wafanya kazi hewa na ujenzi wa miundo mbinu leo hao hao wamegeuza gia angani utazani hawakuwepo kabisa kipindi hiki chote ambacho watumishi wa umma walinyimwa stahiki zao na hadi leo wanaishi kwa mshahara alioupandisha Mara ya mwisho mhe,Jakaya Kikwete mwaka 2015.

Wana bodi kwa maoni yangu wabunge wetu hawana uwezo wa kuisimamia serikali badala yake wanatenda kazi zao kwa kuangalia Rais wa nchi aliyepo wakati huo anataka nini?

Ushauri wangu kwa wabunge ninawaomba wadai katiba mpya kwa niaba ya watanzania wote itakayo tupa nafasi ya kujenga Taasisi imara badala ya kutegemea utashi wa kiongozi aliyeshika madaraka wakati huo. Hii itasaidia pia kuwapa uwezo wabunge wetu kuisimamia serikali pia bunge letu tukufu liamue kufuta sheria na nyaraka kandamizi kwa mfano waraka wa Katibu Mkuu kiongozi unaowataka watumishi wa umma kuomba likizo ya bila malipo miezi miwili wakati wa kugombea nyazifa za kisiasa ni waraka wa hovyo katika nchi huru kama Tanzania.

Wote tumejionea chini ya uongozi wa hayati Dr.John Pombe Joseph Magufuli watu wazima wamechapwa viboko hadharani na wateule wa rais, Watumishi wa umma wa umma wamenyanyaswa vya kutosha kwa sababu tumekosa taasisi imara zinazopewa nguvu kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Wabunge wetu ambao ni wawakilishi wetu tusaidieni kudai Katiba mpya kama mna nia ya dhati.
 
Wanasiasa kama wamerogwa vile, mambo ya maana kwa taifa wao wanaona kama mabaya yani wanaangalia matumbo yao. Tuombe Mungu siku wote wapo bungeni ndege iangukie mle au mabomo yalipukie pale, ili tupate kizazi kipya huenda kikaja na mawazo mapya.. maana wana katisha sana tamaaa
 
Katiba mpya wanaigopa pia itapunguza ulaji wao. Ni mtanziko sawa.
 
ukikaa kimya hata usipige na meza bungeni! hupunguziwi chochote kwenye mafao jumla
 
Kama nyongeza ya mishahara ipo kisheria na wabunge walipiga kimya ili kuendana na utawala uliokuwepo uliokuwa kinyume na hiyo sheria, Je katiba mpya itawafungua vipi midomo wabunge wa aina hiyo katika utawala wa aina yoyote?
Katiba iliyopo ni kweli inamapungufu ila sisi watu ndio tuna mapungufu zaidi. Kwa aina ya sisi watu wa nchi hii hata tukipewa katiba ya marekani mambo yatakuwa hivi hivi. Tunatakiwa tubadilike sisi watu kwanza.

Tunaweza kuwa na tume huru ya uchaguzi lakini kwa aina ya sisi watu wa nchi hii kiongozi wa hiyo tume hatakuwa huru.
 
Back
Top Bottom