Samahani wenye nchi, je siku hizi VETTING hazifanyiki kabla ya teuzi?

mngony

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
5,555
Reaction score
6,972
Habarini wanajamvi, kwanza kabisa niwapongeze wale ambao hawalali usiku na mchana kwa kazi kubwa na nzito ya kizalendo kuhakikisha Taifa letu lipo Salama kabisa.

Siku za karibuni kumetokea utenguzi wa teuzi mda mchache sana baada ya mhusika kuteuliwa, mpaka sasa yameshatokea kama matukio 3 au 4 hivi. Sababu ni kinachoonekana ni makosa katika uteuzi, lakini kwa uelewa wangu mdogo teuzi serikalini huwa kuna utaratibu unaojulikana kama Vetting ambao kwa ufupi ni kuangalia kama mhusika anafaa kwa hiyo nafasi, na utaratibu huo hufanywa na Usalama. Sasa ninachoshangaa inakuaje ndani ya mda mfupi teuzi hizo 3 zinaonekana kama hazikufanyiwa huo utaraibu au haikuanyika vizuri au sijui ilikuwaje. Nakubali kuna nafasi ya makosa ya kibinadamu lakini mara 3 ni nyingi ndani ya kipindi cha miezi 6, na hili tukio la mwisho mtu kaingia mpaka Ikulu kimakosa, jambo ambalo kwa uelewa wangu mdogo ni Hatari Kiusalama
 



Security breach kivipi mkuu hayo maneno ni magumu kuyajua umetumia lugha ya magharibi badala ya kiswahili
 
Kuteuliwa Kimakosa na "Mwananchi Kuingia Ikulu kwa shughuli yoyote ile" kuna uhusiano???? Mwenye Mamlaka ya Kuteua anaweza Kutengua Mda wowote. Je, mtu akiwa msafi asubuhi, hawezi kuchafuka jioni??? Naomba jibu
 
Kuteuliwa Kimakosa na "Mwananchi Kuingia Ikulu kwa shughuli yoyote ile" kuna uhusiano???? Mwenye Mamlaka ya Kuteua anaweza Kutengua Mda wowote. Je, mtu akiwa msafi asubuhi, hawezi kuchafuka jioni??? Naomba jibu

Sawa ana mamlaka wala sina shaka nalo, ndio mara tatu ndani ya miezi 6, hao wote wanachafuka jioni Mkuu, au unatoa assumption.
 
Sawa ana mamlaka wala sina shaka nalo, ndio mara tatu ndani ya miezi 6, hao wote wanachafuka jioni Mkuu, au unatoa assumption.
Kwani hizo vetting si zinafanywa na binadamu kama wewe?
Shida kuna watu wamezoea kuchomeka majina ya watu wao sasa mchezo umeshtukiwa.
 
Ukiona mabadiliko yametokea ujue hapo ndio vetting imekamilika kwa uhakika
 
πŸ™‚ πŸ™‚ πŸ™‚ πŸ™‚
 
Sijui utaratibu wa kipindi cha vetting,ila kumwambia yule jamaa awapishe ikulu kwa kua aliandikwa kimakosa ni jambo lakusikitisha mnoo,wangemuita kando sio mbele ya kadamnasi, tena akiwa na familia yake
 

buman behaviour is not static , ndo maana hata kwenye ndo baada ya kuoa/kuolewa mtu hubadilika , sio kwamba aliolewa akiwa hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…