Samahanini wazee wa Legum Baccalaureus.......

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Posts
2,149
Reaction score
1,718
Itifaki imezingatiwa, ningependa kujua kukata affidavit ina gharimu shilingi ngapi? maana juzi nilienda mahakamani nikamkuta jamaa akaniambia eti nimpe elfu kumi ya kitanzania. Machale yakanicheza nikaacha. Ningependa kuskia kutoka kwenu, hiv itanigharimu shilingi ngapi? Naombeni majibu yenu tafadhali.
 
Mbona sijibiwi? au nimepotea njia? wanasheria mpo? au mnataka consultation fee?
 
wewe ulitaka umpe ngapi? Kumbuka muhuri analipia na ule muda wake wa draft
 
Mahakaman kwa kumi kubwa mno mara nyng ni tano tu na sio sheria unaweza ukafanyiwa bure unaweza ukaambiwa hata laki ni utashi wa mtu tu anayekupa huduma yake. Ukienda kwa mawakili binafsi ndo inakua hiyo kumi mara nyng.. But narudia sio sheria yeyote anaweza kukwambia bei anayotaka.
 
Nyie ndio mnaidhalilisha taaluma ya sheria kama uliona elfu kumi ni nyingi si ungejiandikia mwenyewe.
Hivi unaona ni rahisi tu kuandika na kugonga muhuri eeh..ebu jaribu kujiandikia na wewe uone..
Mi ukija kwenye law firm bila 50 muhuri hupati na kama unataka ni draft hiyo affidavit nahisi andaa 250 labda naweza kukufikiria..
So hiyo elfu kumi kakupendelea sana..ningekua wewe nisingepoteza muda
 

Kwani na wewe unaandika from scratch au unakopi kopi tu toka kwenye templates?
 
(Tusi la wastani) Ulitaka kutoa bei gani? Ukifika umri wa kuoa( kama wewe ni mwanaume) ukishapewa bei ya mahari urudi jamvini kuja kuulizia bei halali ya mahari,usisahau kutuwekea picha ya mchumba wako!
 
Mwongo wewe. Huna ubavu wa kutengeneza mwenyewe. Unakopi kopi tu kama wafanyavyo wengine.

Nahisi we ndio ulikua lecture wangu miaka yote minne wakati nasoma legal drafting...that's why unaujua uwezo wangu..
FYI mi ni Mbeky mi sio hao wengine
 
Last edited by a moderator:
Nahisi we ndio ulikua lecture wangu miaka yote minne wakati nasoma legal drafting...that's why unaujua uwezo wangu..
FYI mi ni Mbeky mi sio hao wengine

Huna ubavu wa kuandika legal document from scratch wewe. Na hauna tofauti na wengine. Mnadesa kwenye templates tu.
 
Huna ubavu wa kuandika legal document from scracth wewe. Na hauna tofauti na wengine. Mnadesa kwenye templates tu.

Sina haja ya kubishana nawe katika hili naona naendeleza malumbano yasiyokua na tija afu it is unethical to me.
Nimepitia link yako hiyo unayodai ndio unapata legal documents sa kwa kua we unaaccess basi ni vizuri ukamsaidia huyu mleta uzi kumpatia hiyo affidavit na ikiwezakana ufanyie na verification kabisa maana naona hiyo page itakua inatoa uwezo wa deponents kuswear online.
Kila la kheri brother
 

Hapana, siendelezi malumbano yasiyo na tija.

Ukweli ni kwamba legal documents nyingi watu wanadesa kwenye templates tu. Na kudesa kwenye template wala si kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…