Samaki mmoja na wenzake wakioza, ziwa haliozi. Wazazi wapeni nafasi watoto!

Samaki mmoja na wenzake wakioza, ziwa haliozi. Wazazi wapeni nafasi watoto!

Chachasteven

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2014
Posts
1,941
Reaction score
2,044
"Napenda umaarufu, nachukia mbwembwe zake" - Fid Q

Habari za wakati huu? Najua ni usiku sana na pengine unatamani kulala kutokana na uchovu wa pirika pirika lakini kabla ya kutekeleza shauri lako nikuombe uniazime dakika chache tuwemo katika hili... Ni MUHIMU!

Kwanza tukubaliane kuwa sanaa ni uwanja mpana kama wote tunavyofahamu. Umebeba mambo kibao sana na takwimu zinaonesha ndio uwanja uliotoa ajira na fursa nyingi kwa vijana duniani. Kwa lugha nyingine sanaa imefanya watu waendeshe maisha yao na hilo halina ubishi kwa sababu tunaona mifano mingi hata hapa kwetu, Tanzania - Kama kuna mtu anapinga, sio kwa sababu hajui ila ni kwa sababu ni mjinga!

Ndiyo! Wala haujakosea kusoma. Anayepinga ni mjinga.

Basi kama nilivyosema awali, sanaa imethibitisha kuwa uwanja ambao unalipa na wenye fursa zisizo na kikomo. Zamani sanaa ilifanywa kwa sababu ya mapenzi tu lakini kadri miaka ilivyokatika watu wakahamia kwenye kuifanya sanaa kuwa biashara na wamefanikiwa. Kwa sababu hiyo kila mtu anatamani kuingia kwenye sanaa kutokana na mafanikio anayoyaona kwa wale walioko kwenye sanaa. Hata hivyo, juhudi hizo kuna wakati inafika zinaishiwa mori na hamu na kizazi kipya cha wasanii kinakata au kukatishwa tamaa.

Hali hii inasababisha kutokugundua vipaji vipya. Sababu zilizo nyuma ya hili ni nyingi lakini kubwa zaidi iliyonisukuma mimi kuandika uzi huu ni hii ya matendo wanayoyafanya wasanii wetu - Ambao wanatazamwa na jamii au labda wasanii chipukizi. Wenyewe wanaita KIKI (staying on trend.)

Nitachukua mfano hai mmoja, ambao ni uvujaji wa picha za faragha za wasanii Nandy, Amber rutty, Giggy Money, Gwajima, na Meninah miongoni mwa wengi. Kibinadamu jambo linaloonekana kwenye picha hizo lipo sahihi kwani licha ya kuwa wasanii wao ni binadamu na wana hisia. Nani hafanyi mapenzi humu?? Nani??

Hivyo nieleweke, wao kufanya mapenzi sio kosa ila wao kuruhusu picha hizo zisambae ni kosa - Wanaiharibu taswira nzima ya sanaa na wasanii (Mtazamo wa kila mtu) na mwisho wa siku sanaa itaanza kuchukuliwa kama uhuni.

Kwa hali ilivyo, ni vigumu mzazi kumruhusu mwanawe, kwa hiari, kufanya sanaa kutokana na anachokiona kwa wasanii. Embu wasanii muwe makini - Kama hamjui jukumu kubwa mlilonalo kwenye jamii ni bora muuache huo usanii.

Niwaambie tu, hata sio ujanja. Embu wekezeni nguvu kubwa kwenye kuhubiri vitu vyenye mashiko kuliko uchi wenu. Imagine sasa hivi yule mtoto aliyekuwa anamtazama Meninah kama role model wake ana hali gani?? Jamani wewe ni msanii lakini kuwa na mipaka! Kuna wakati najiulizaga Myra akiwa mkubwa mara akaiona ile picha ya Giggy kabinuka?? Inasikitisha sana aisee.

Lakini bado naamini katika nafasi ya pili na ya tatu kwa sababu kukosea ni hulka ya binadamu. Kosa sio kosa ila kurudia kosa ndiyo kosa. Tusamehe ila tusisahau ili isijitokeze tena.

Na kwa wazazi na walezi, wahenga walisema, "Samaki mmoja akioza, wote wanakuwa wameoza". Wakaishia hapo. Hawakuongeza chochote, wala hakuna pahali imerekodiwa kuwa walisema na ziwa au bahari inakuwa imeoza - Na huo ndiyo ukweli kwenye ulimwengu wa sanaa pia.

Embu nisikuchoshe sana ili uufurahie usiku wako neno langu ni kuwa, wazazi wapeni watoto fursa ila mkumbuke kuwaonya. Matendo ya watu wachache yasitumiwe kama tafsiri ya maana halisi ya jambo f'lani. Tuwape watoto fursa wawe kile wanachotaka ila katika nidhamu.

Sanaa ni ajira na inalipa kama ikiheshimiwa.
Alam siki mpaka nitakapopata kalamu na karatasi tena.
 
"Napenda umaarufu, nachukukia mbwembwe zake"

Umeandika mstari ambao rafiki yangu anaupenda sana na hata tukipotezana ndani ya miezi 5 tukikutana lazima aseme huu mstari.

Ilinibidi nirudi juu kusoma I'd labda anaweza kuwa yeye.
 
"Napenda umaarufu, nachukukia mbwembwe zake"

Umeandika mstari ambao rafiki yangu anaupenda sana na hata tukipotezana ndani ya miezi 5 tukikutana lazima aseme huu mstari.

Ilinibidi nirudi juu kusoma I'd labda anaweza kuwa yeye.
Haha! Nimefurahi kusikia hivyo.
 
Back
Top Bottom