Samata alikuwa tatizo Aston Villa

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Aston villa walitakiwa kucheza na Manchester united mechi ya kwanza kwenye ligi,
Hawakucheza kutokana na Manchester united kuongezewa muda wa mapumziko pamoja na Manchester city

Am sure kama sio kushinda basi sare wangepata ,hadi sasa hawa mabwana wameshinda mechi 4 kati ya mechi nne walizo cheza EPL msimu huu pamoja na ile walio mbomoa Liverpool goli 7.

Kikosi chao kiko very balanced ukiwaangalia flow ya mashambulizi na namna wanavyo jilinda ni dhahiri wanajambo lao msimu huu ..

Kutoka kwenye chupu chupu kushuka daraja mpaka tittle contender ni Zaidi ya mabadiriko.
Ni mapema kusema hawa Jamaa ni tittle contender ila wameanza vema sana tofauti na matarajio ya watanzania wengi tulio wa unfollow Instagram na Twitter.

Wajuba wako serious kutu onesha kua kakaetu alikua tatizo na sio Jack Grielish kumnyima pasi .

#FAHAMUSPOTI.
 
Samata alikuwa tatizo Aston Villa na Aston Villa ilikuwa tatizo kwa samata
 
Huwezi kuwa serious mkuu, samatta aliikuta aston villa ishaelekea kibla..

Villa wamejipanga upya, hata mimibwamenishangaza, naona usajili mpya kina Barkley wameongeza kitu.. Hata sammata angekuwepo naamini angefanya vizuri kwa takwimu alizoonesha mwaka jana.
 
ngoja ligi ichanganye ndio tutaona nani ni nani na nafasi ya kila timu itajulikana
 
Ile nafasi kashika ya watu, baada ya mechi kumi kila timu itarudi kwenye nafasi iliyoizoea. Ni sawa na hapa Azam wanajua kabisa ile nafasi waliyopo sio ya kwao, na mwenye nafasi wanamjua kwa 100%
Nyota nyema huonekana asubuhi mkuu
 
Yes! Aliikuta ikiwa imesha elekea kibla na ndio sababu ya yeye kuletwa pale ,akaokoe jahazi ila kashindwa,

Wakina Rose Bakcley na Witkins wameenda wameikuta tuku hoi kama Samata ila wameonesha utofauti .
 
Samatta Amepashindwa pale Aston villa, wenzake wamepaweza.

Hilo liko wazi
 
Yes! Aliikuta ikiwa imesha elekea kibla na ndio sababu ya yeye kuletwa pale ,akaokoe jahazi ila kashindwa,

Wakina Rose Bakcley na Witkins wameenda wameikuta tuku hoi kama Samata ila wameonesha utofauti .
Nipe takwimu walimchezesha game ngapi, alianza ngapi, ngapi alitokea benchi, alitengenezewa nagasi ngapu alifunga ngapi, alikosa ngapi. Tupate kumuhukumu vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…