SAMATA: Atapotea kwenye Soka

Nilitaka nishangae msianze ushirikina wenu.
Giroud hajafunga game ngapi?
Vipi Sanchez
Hata huyu Rashford.
Hahahaha mkuu ulikuwa unawasubiri waje. Umetoa mfano mzuri

Kukosa magoli sio sababu ya kusema mtu hachezi vizuri au atapotea, inategemeana na majukumu anayopewa uwanjani na kocha wake.
Samatta Alivyojiunga Genk alikua akiingia Dk ya 77 ila sasa hv anaanza hii inaonesha ni jinsi gani kocha alivyomwamini
 
Gaza and Israeli,
Hebu tushauri zaidi kuliko namna ulivyoandika.
Vyema ukaanza na wachezaji wa hapa wafike zaidi yake inaonekana unajua mambo ya Mpira.
Hii kutafuta P kwa Samata atakapofeli ukasema ulishasema...ni unafiki wa kiswazi.
Sisi tunapaswa kua wa kwanza kumpa support adumu wengine waige iwe ajira kwao.
Ni mfano Samata ktk Soka....
Ukitafsiri KUKOSOA ni ushauri kua tayari kuja kuitwa MNAFIKI.
Anayejua HUSHAURI tu,si kwa namna ulivyoleta Mada.
Tumpe support !!
 
Samatta inabidi akaze sana vinginevyo atarudi africs maana wazungu wanataka matokeo na kama yule staika mwenzake akisndelea na kiwango chake Samatta atakosa namba. Hiyo ndio itakuwa mwisho wake. Shida nyingine ni kuwa hawa wachambuzi wa bongo wakina shafii, kumwembe et al.... Wanampamba sana mpaka analewa sifa. Kijana anatalent ila inabidi apambane mafanikio hayaji kirahisi
 
mkuu mbna unatuongopea. kwenye ushindi wa goli tano juzi kafunga moja, kasababisha penalt kick kwa kufanyiwa faulo kwenye box iliyomfanya goalkeeper kupewa red card. na katika ushindi huo katoa assist mbili za magoli. ivi jamani mnataka aweje. kwa takwimu nilizotoa inaonekana effect yake ya kutia pressure timu pinzani ni kubwa sana. tusifiwe panaposifiwa jamati eti
 
Sijui ninavyomfuatilia. Katika michezo muhimu sana kwa siku za hivi karibu hajaonyesha bidii ya namna hiyo. Amekuwa anavizia ndo maana hujamsikia kafanya mambo yake.

Inawezekana anazipata hizi na anafanyia kazi.

Cha msingi binafsi nikimuona anacheza vizuri ni furaha sana na tunataka aendelee hivyo angalia katika michezo 2-3 awe na goli.
 
.
Naamini kabisa sijaandika kwa kuponda ila kwa uhalisia ninaoona kila wakati. Cha msingi hata yeye kama anafuatilia, asifanye kuvizia. Bado yeye ni kijana kuliko mzee wa Kigiriki ambaye walimchukuwa kabla yake katika nafasi yake.
 
Mechi ya mwisho niliyomuona alikuwa anacheza nyuma ya washambuliaji...! Yaweza kuwa sababu.
 
Binafsi pia nimetazama mechi zao sikupenda anavyocheza anakuwa amepowa sana..... Ingawa mechi ile waliyoshinda kwenda uropa alifunga lakini hayupo kwenye kile kiwango tunachomfahamu..... Amekuwa anavizia vizia sana... Kama Tambwe na kiiza.....
 
sasa hapo ubaya upo wapi, nimeuliza analipwa bei gani kwa wiki
Umerogwa wwe mada inazungumzia namna ya uchezaji wewe unauliza mshahara anaolipwa we jamaa kilaza sana ayse
 
kimsingi huwezi kusema hilo kumbuka samata anadisplyn sana ya mpira wewe unaweza ona hivyo kumbe ni maelekezo ya kocha.
 
Yeah mkuu, anafuata maelekezo ya kocha na si jukwaa kama hapa nyumbani.
 
Alifunga goli moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…