Samatta agoma kwenda Ulaya

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801




Na Zahoro Mlanzi

MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Mbwana Samatta amekataa sh. milioni 200 kutoka kwa Klabu ya Austria Vienna ya Austria kutokana na klabu hiyo kumuhitaji kwa ajili
ya majaribio, badala ya kumsajili moja kwa moja.

Klabu hiyo ilikuwa imetenga zaidi ya sh. milioni 200 kwa Samatta, endapo angefuzu majaribio ambapo inashiriki Ligi Kuu ya nchini humo ya Austria Bundesliga.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam juzi, Mshauri wa mchezaji huyo ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa African Lyon, Jamal Kisongo alisema wakati wanasaini mkataba wa Samatta kwenda TP Mazembe, walishapokea ofa mbalimbali za mchezaji huyo kutakiwa Ulaya.

"Unajua huyu kijana (Samatta), ana bahati sana, huwezi amini alitengewa mamilioni ya fedha na Klabu ya Austria Vienna ya Austria, ambazo ni zaidi ya zile zilizompeleleka Mazembe, lakini tulifikiria mbali na kuamua asiende huko.

"Uzuri Mazembe walikubali moja kwa moja kumsajili na wakataja dau lao, lakini hiyo timu nyingine walimuhitaji kwa majaribio alafu akishafaulu ndipo watoe hayo mamilioni yao, tukajiuliza asipofuzu itakuwaje ndipo tulipoona bora aende Mazembe," alisema.

Alisema endapo klabu hiyo ingeonesha nia ya kumsajili moja kwa moja kama ilivyofanya TP Mazembe, basi wangekubali Samatta aende kucheza soka la kulipwa nchini humo.

Kisongo alisema hata hivyo ana uhakika TP Mazembe, kutokana na timu hiyo kujulikana karibu ulimwenguni kote, hana shaka akiwa na bidii basi atazidi kusonga mbele kwa kucheza Ulaya.

Historia ya Austria Vienna, inaonesha kwamba ndiyo timu iliyotwaa mara nyingi ubingwa wa ligi ya kwao kwa kutwaa mara 23, Kombe la Austria Super mara sita, Kombe la ligi mara 27 na ilishawahi kushiriki michuano ya Ligi ya Ulaya mwaka 1978.
 
Hana bahati tu, pia jina lake zuri, la kibiashara, mpende au la jina nalo lina sehemu yake hasa klabu kubwa za ulaya, hawataki majina ya kiaina flani ili watoto wao wazoee hayo majina, hata Arabuni ukienda kimichezo lazima wakupe jina leo, huwezi ukaendelea kujiita Samuel, ndivyo hivvo Uzunguni huwezi kwenda na jina Mohamed, na kadhalika...
 

El Haji Diof!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Dogo aende ulaya...africa hapa hakuna jipya ati.
 
Huwa wanaogopa maisha ya ulaya na lugha pia wakati mwingine unawafanya wanakuwa wapweke....pia hakuna vijiti...manaa wachezaji wetu wa tz kwa vijitii balaaaa bila hvy kiwango kalasi kabisa.....kumbuka chan walivyokuwa mazuzu
 
wabongo bana,wanaangalia ugali wa kesho tu,huyo mshauri wake na njaa zake kaamua kucvhukua hizo pesa ndogo haraka sababu hakuna majaribio,kaacha kumshauri dogo aende majaribio kule na km anajiamini angechota hizo mil 200 na mkataba mzuri hapo baadaye.lakin...:bange:
 
Wewe nawe wacha kutudanganya...kuna wachezaji kama kina El Muhammad, Al Habsi, mohammed diame etc etc
 
kwanai anaogopa nini kujaribiwa? hajiamini nini? angeenda ulaya angepata exposures zaidi na kuonekana kwenye timu kubwa zaidi na anga lingempeleka mpaka sijui wapi. huko mazembe akiwekwa benchi nani atamuona tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…