Samatta aomba Shomari Kapombe apewe Zawadi kama wachezaji wengine

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Kapteni wa Taifa Stars, Samatta ameomba TFF impatie Mchezaji mwenzake Kapombe zawadi kama Wachezaji wengine, likishindikana hilo amewaomba Wachezaji wenzake wote wamchangie mwenzao huyo na kama hilo litashindikana pia basi atagawana nae nusu kwa nusu ktk ahadi ya RC Makonda.

#MillardAyoSPORTS

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Well said! Kama kuna aliyeyesoma msg ya Samatta baada ya mchezo ilikuwa nzuri na bila mihemuko, alimshukuru Mungu, akawashukuru wachezaji wenzie, akawashukuru mashabiki na mwisho waandaaji wa mechi. Ni kama alijua baada ya mchezo zingeibuka ngojera za "waliofanikisha ushindi" na kaamua kujionndokea usiku ule ule kuepuka kulishwa maneno.
Katika hili tuna mengi ya kujifunza na mbaya zaidi ni hizi petty politics zisizo na kichwa wala miguu!
 
Kapombe aliumia katika kambi ya starz, japo TFF walishafunika kombe, asante samata. Kuna wachezaji ambao walikuwa na timu phase zote ila hawakuitwa phase ya mwisho kama wakina abdul banda. Na tunawachukulia kama hawakuwa kwenye kikosi kilichofanikisha haya. Politics ikiingia kwenye mpira tunategemea kuona mambo kama haya.
 
Kwani Kapombe tangu aumie amepata nn toka starz zaidi ya Simba kumtibu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Inanikumbusha 1990s George Magere Masatu beki Wa Kutumainiwa wa Simba alivunjika Mguu akiokoa Mpira uliokuwa unaenda kwny nyavu kwa kuvamia Mwamba wa Goli akiwa Taifa Stars
Msaada wa TFF ya wakati huo ( FAT) ilikuwa kwenda kumlaza Muhimbili
 
Kaptein anawazidi TFF na wizara ya michezo.
Hongera POPA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…