Samatta aongoza 'mauaji' ya TP Mazembe

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta ameiongoza TP Mazembe kuishinda Maghreb Tetouan ya Morocco kwa mabao 5-0 jijini Lubumbashi,DRC na kutinga nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

Samatta alifunga mabao matatu na kuwazima kabisa Wamoroko hao waliokuwa wakilingana nao kwa alama kabla ya mchezo huo wa jana. Samatta alikuwa mwiba mchungu kwenye mchezo huo uliokuwa wa kasi na ufundi.

Sasa TP Mazembe itakutana na El Merreikh ya Sudan kwenye nusu fainali.
 
Safi sana jembe endelea kutuwakilisha vyema watanzania.
 
Kwenye facebook page ya TP Mazembe jamaa wanamfananisha na Ronaldo
 
Guud samata ..umetupaisha Tz
 
Safi sana jembe endelea kutuwakilisha vyema watanzania.

Afanye hivyo hivyo hata akiwa Taifa Stars, kwa mfano angetupia hata bao moja tu dhidi ya Nigeria si tungekuwa mbali! Ufundi uanzie nyumbani (Taifa Stars) kisha ndiyo uende huko nje (TP Mazembe).
 
Hawezi kufanya hivyo kwenye timu ya Taifa kwasababu anacheza na wachezajo wengi wasiojitambua uwanjani watu ambao mpaka wavute bangi ndiyo mpira uchezwe.
 
Mechi dhidi ya nigeria sammata hakucheza vizuri..inshort alitukosesha magoli ...ni mbinafsi...na hachezi vizuri huku kwa kuwa tunamnyenyekea na kumuona ni mungu mtu tofauti na mazembe......
 
nazani we n kada wa chama fulan HV cha watukanaji
 
Afanye hivyo hivyo hata akiwa Taifa Stars, kwa mfano angetupia hata bao moja tu dhidi ya Nigeria si tungekuwa mbali! Ufundi uanzie nyumbani (Taifa Stars) kisha ndiyo uende huko nje (TP Mazembe).

Tatizo ni ushirikiano hafifu anaopata kutoka kwa wenzake. Taifa Stars hata Ronaldo akiichezea hataweza kufunga goli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…