Six Man
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 253
- 892
Jana ilikuwa ni siku ya kipekee sana kwa watanzania. Jana, mamilioni ya watanzania kwa namna mbalimbali macho yao yalikuwa katika jiji la Birmingham. Macho yao yalikuwa huko kwasababu moja tu, kumwangalia kijana wao akiwa akiichezea timu yake mpya ya Aston villa kwa mara ya kwanza.
Samatta alikuwa mtanzania wa kwanza kucheza Europa ligi. Samatta alikuwa mtanzania wa kwanza kucheza Uefa champion ligi. Samatta amekuwa mtanzania wa kwanza kucheza katika timu inayoshiriki katika ligi kuu ya Uingereza. Na sasa anaenda kuwa mtanzania wa kwanza kucheza katika uwanja mkubwa wa Wembley.
Samatta, timu yake ya Aston villa jana usiku imefanikiwa kwenda kucheza katika fainali ya Carabao itakayoenda kupigwa katika uwanja wa Wembley. Aston villa wanamsubiri mshindi wa mechi ya leo kati ya Manchester city na Manchester Utd.
Katika mechi ya kwanza Manchester city iliifunga Manchester Utd mabao matatu kwa moja. Leo ama Utd wanaenda kulipa kisasi ama wanaenda kupigwa zaidi.
Hivyo, Samatta akiwa katika jezi ya Aston villa ataivaa ama Manchester city ama Utd katika dimba la Wembley.
Kucheza katika dimba la Wembley ni bahati kubwa sana kwa Samatta. Wachezaji wengi hawajapata bahati kucheza katika dimba hilo.
Kwa kifupi tu Samatta kaenda na mguu wa bahati Aston villa.
Alisajiliwa timu ikiwa nafasi ya kumi na nane katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza na sasa wanashika nafasi ya kumi na sita huku ikiwa ya kwanza kukata tiketi ya kuelekea Wembley.
Watanzania tupo nyuma yako. Tunakusubiri kwa hamu ukikipiga ndani ya Wembley..
Naitwa Six Man.
Sent using Jamii Forums mobile app