“Sambaza Shangwe za Mama, Tanzania ya Leo Siyo ya Jana” social media campaign concept note (Noti Zana)
Utangulizi
Katika kipindi kifupi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Raisi Samia Suluhu Hasan, kumeshuhudiwa mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za kijamii. Mheshimiwa Raisi Samia Suluhu Hasani amekuwa kiongozi makini, mzalendo na ameweza kutatua changamoto mbalimbali tena kwa kipindi kifupi hivyo kuleta shangwe na furaha kwa Watanzania.
Akiwa ndiye Mwenyekiti wa chama tawala (Chama cha Mapinduzi), ameweza kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa umahiri na uzalendo mkubwa hivyo kufanikiwa kuyaweka yaliyomo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020 katika hali halisi. Uimarishaji miundombinu hususani barabara, reli, viwanja vya ndege, bandari, huduma za kiuchumi na kijamii, huduma za maji, utawala bora, uwekezaji na utalii, ujenzi wa madarasa, hospitali, zahanati, na vituo vya afya, demokrasia, utumishi, maswala ya jinsia na mengine mengi ni baadhi ya mambo ambayo yamekuja kuleta shangwe kubwa katika uma wa Watanzania.
Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, Chama cha Mapinduzi kwa maana ya wanachama na wakereketwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wana jukumu la kuhakikisha kazi hizi kubwa na nzuri zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hasani ambaye ndiye Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania zinatangazwa, zinaonyeshwa na kuelezwa, ili wananchi wapate kuelewa juu ya mambo yaliyofanyika, yanayofanyika na yatayofanyika na hivyo kuiunga mkono Serikali yao pendwa ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hasani ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.
Kwanini “Sambaza Shangwe za Mama, Tanzania ya Leo Siyo ya Jana” social media campaign?
Kutokana na ongezeko la watumiaji wa simu janja na huduma ya mtandao (intanenti) nchini, Tanzania imekuwa ni miongoni mwa nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zinazofanya vizuri katika matumizi ya mitandao ya jamii. Taarifa za mamlaka ya mawasiliano (TCRA) inasema watumiaji wa intanenti hadi kufikia Juni 2021 walikuwa milioni 29 sawa na asilimia 49 ya Watanzania na watumiaji wa mitandao ya kijamii walio hai walikuwa milioni 5.
Mitandao ya kijamii kama Facebook, YouTube, WhatsApp, Instagram, Twitter, TikTok, Telegram, Snapchat imekuwa chanzo chenye nguvu cha usambazaji wa habari, matukio, utoaji elimu na ufanyaji wa biashara nchini Tanzania. Kwa kutumia mitandao ya kijamii, habari na matukio yanaweza kufikia watu wengi, kwa kutumia muda mfupi na kwa gharama ndogo, tena kwa kupitia simu za mikononi na komputa. Hii imewavutia Watanzania wengi, haswa kundi la vijana, kuvutiwa na kuanza kutumia mitandao ya kijamii kama chanzo kikuu cha kupata habari, matukio mbalimbali pia fursa ya kutangaza na kufanya biashara.
Katika kuhakikisha taarifa za utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ya 2020-2025 na tatuzi za changamoto mbalimbali zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasani, zinafika kwa Watanzania walio wengi kwa kutumia muda mfupi, mitandao ya kijamii kwa kutumia kampeni ya “SAMBAZA SHANGWE ZA MAMA, TANZANIA YA LEO SIYO YA JANA” ni njia bora, shirikishi na yenye gharama nafuu, na itasaidia kwa kiasi kikubwa kuyatangaza mambo ambayo yamefanywa na serikali ya awamu ya sita, hivyo kusaidia jamii ya Tanzania kusimama pamoja na Rais wetu Mama Samia Suluhu Hasani.
Ukiangalia mgawanyiko wa idadi ya watu nchini Tanzania, rika la vijana ndiyo rika lenye watu wengi zaidi kulinganisha na watu wazima na wazee, na vijana hawa ndiyo watumiaji zaidi wa mitandao ya kijamii kulinganisha na marika mengine. Vijana ndiyo wapiga kura, kwa hiyo kampeni ya “SAMBAZA SHANGWE ZA MAMA, TANZANIA YA LEO SIYO YA JANA” ni ya muhimu katika kutafuta kuungwa mkono na kundi la vijana, kwa sababu vijana ndiyo wanatumia zaidi mitandao ya kijamii. Katika kuyaelezea, kuyatangaza, na kuyaonyesha mafanikio ya Awamu ya Sita, Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikifanya vizuri zaidi kwenye majukwaa mengine kama radio, runinga, magazeti, na kwenye majukwaa ya kisiasa, ukilinganisha na mitandao ya kijamii ambapo dunia ya sasa inategemea zaidi mitandao ya kijamii katika kujitangaza. Mfano siyo jambo la kushangaza habari ya Mh. Rais kufungua mradi mkubwa wa maji mchana kuzidiwa umaarufu kwenye mitandao ya kijamii na habari ya mtu aliyefumaniwa katika siku hiyo, jambo ambalo siyo afya kwenye kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
“Sambaza Shangwe za Mama, Tanzania ya Leo Siyo ya Jana” ni kampeni itakayotumia mitandao ya kijamii katika kuhamasishana kusambaza taarifa zinazohusiana na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020-2025, pia utatuzi wa changamoto mbalimbali zilizotatuliwa na serikali ya Awamu ya Sita. Kwenye kampeni hii, wananchama, wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi watatakiwa kupiga picha na kurekodi video fupi zinazoonyesha utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi, tatuzi mbalimbali zilizofanywa na serikali ya Awamu wa Sita pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye maeneo wanayotoka na kuzisambaza video, picha, na taarifa za miradi ya kimaendeleo kwenye makundi ya ndugu, jamaa, na marafiki, na kwenye kurasa zao za kimatandao ya kijamii, n.k. Chama cha Mapinduzi kina wanachama na wakereketwa zaidi ya milioni 10 ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Huu ni mtaji mkubwa sana katika kutekeleza kampeni hii ya “Sambaza Shangwe za Mama, Tanzania ya Leo Siyo ya Jana”.
Katika wanachama na wakereketwa wa chama cha mapinduzi zaidi ya milioni 10 kwa siku moja wakitokea wanachama na wakereketwa 200 tu wakapiga picha,au kutengeneza video fupi zinazoonyesha mafanikio ya awamu ya sita katika maeneo yao halafu wakazisambaza kwa ndugu jamaa na marafiki,ni rahisi habari hizi kuwafikia watanzania walio wengi ndani ya muda mfupi hivyo wananchi kuiunga mkono serikali yao na kusafisha njia kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Chama cha mapinduzi kina bahati na utajiri mkubwa wakupendwa na watu mashuhuri kwenye jamii zetu kama wanasiasa,wanamichezo,wafanyabiashara,viongozi wa dini,wanamuziki,waigizaji,watangazaji n.k,kupendwa huku na watu hawa pia ni mtaji mkubwa sana katika kufanikisha kampeni hii ya “SAMBAZA SHANGWE ZA MAMA,TANZANIA YA LEO SIYO YA JANA”,kutokana na watu hawa kuwa na mamilioni ya wafuasi kwenye mitandao ya kijamii watu hawa mashuhuri wanaweza pia kutumika katika kusambaza shangwe za mama na taarifa kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi na tatuzi za changamoto mbalimbali zikawafikia watu wengi tena kwa muda mfupi hivo watanzania wengi kusimama pamoja na serikali ya chama cha mapinduzi inayoongoza na muheshimiwa Samia Suluhu Hasani jambo ambalo litarahisisha katika kushika dola kwa mara nyingine katika uchaguzi mkuu wa 2025.
MALENGO:
Wanachama, wakereketwa, na wananchi wenye mapenzi mema na Tanzania kipiga picha na kuchukua video fupifupi zinazoonyesha na kuelezea utatutuzi wa changamoto, utekelezaji wa ilani, na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika maeneo yao na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Faida za Sambaza Shangwe za Mama Tanzania ya Leo siyo ya Jana Social Media Campaign:
Chama cha mapinduzi kuendelea kuungwa mkono na wananchi na kuendelea kushika dola, lengo kuu la chama cha mapinduzi ni kuendelea kuwa chama tawala, kampeni hii itaongeza imani ya wananchi kwa chama cha mapinduzi hivo kurahisisha zoezi la kushika dola.
Chama cha mapinduzi kuweza kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa awamu ya sita bila kutumia gharama yoyote, wanachama na wakereketwa wa chama cha mapinduzi ndiyo wenye jukumu la kusambaza mafanikio ya serikali. Mapenzi ya wanachama na wakereketwa wa chama cha mapinduzi kwa chama chao yataongezeka, kwa sababu kampeni hii ni ya hiari pia shirikishi.
Kampeni hii pia itakisaidia chama cha mapinduzi kuvuna mashabiki, wapenzi, na wanachama wapya, hii inatokana na wananchi kupata taarifa juu ya maendeleo yanayofanywa na chama cha mapinduzi katika maeneo mbalimbali nchini. Ushawishi wa chama cha mapinduzi kwa kundi la vijana utaongezeka maradufu, vijana ndiyo watumiaji wakuu wa mitandao wa kijamii, hivo kampeni hii kutumia mitandao ya kijamii itasababisha taarifa zinazohusu utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kuwafikia vijana walio wengi hivo chama kuongeza ushawishi kwa kundi la vijana.
Uzalendo wa wananchi kwa nchi yao utaongezeka maradufu, hii ni kutokana na kwa kupitia kampeni hii mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita yataonyeshwa na mapenzi ya wananchi kwa serikali yao yataongezeka maradufu. Umarufu wa chama cha mapinduzi utaongezeka ndani na nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania.
Washiriki ni Chama cha Mapinduzi, wananchi, na watu mashuhuri. Kidumu Chama cha Mapinduzi.

- Kuhakikisha jamii ya Tanzania inasimama pamoja na chama cha mapinduzi katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
- Kuhakikisha jamii ya Tanzania inasimama pamoja na Rais wetu Mama Samia Suluhu Hasani katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
- Kuhakikisha kuwa wananchi wanapata uelewa ya mambo ya kimaendeleo yaliyofanyika,yanayofanyika na yatakayofanyika hivo kuendelea kuiunga mkono serikali yao pendwa ya awamu ya sita.
- Kuhakikisha kuwa wanachama na wakereketwa wa chama cha mapinduzi wanashiriki moja kwa moja katika kunadi utekelezaji wa ilani wa chama cha mapinduzi wa 2020-2025 kwa kusambaza habari na matukio yanayohusu mafanikio ya serikali ya awamu ya sita.