Uchaguzi 2020 Same, Kilimanjaro: WanaCCM Kata ya Bwambo waandamana kumpinga Mgombea Udiwani aliyepitishwa na Halmashauri Kuu

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Wanachama wa CCM wakiwemo Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Kata ya Bwambo Wilayani Same, Kilimanjaro wameandamana kumpinga mgombea aliyeshika namba 2 kwenye kura za maoni na kupitishwa na Halmashauri Kuu kugombea Udiwani

Mshindi wa pili, Gerald Ngale alipata kura 83 na mshindi wa kwanza ni Ahiya Msoka aliyepata kura 117. Wanachama walionekana Mtaani wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali

Wanachama hao wamemuomba Rais Magufuli na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Bashiru Ali kuingilia kati suala hilo na kusema kuwa wanamtaka aliyeongoza kwenye kura za maoni na sio mshindi wa pili aliyepitishwa

Mmoja wa Wanachama hao, John Piniel amesema “Tunataka Viongozi Wakuu wa Chama chetu watusikie, kwa awamu hii hatutanyamaza, hatutavumilia kwasababu Katiba ya Chama inasema kuwa kura ndio inatupa Kiongozi. Waliotuwakilisha kwenye kura za maoni wamefanya kazi tuliyohiyaji na kumchagua Msoka.”

Ameongeza, “Baada ya Msoka kuchaguliwa, tulipokuwa tunashangilia, Viongozi wa juu wa Chama kwenye Kata hii wakatuambia tumepiga vigelegele kwa mtoto kuzaliwa wakati bado hajalia. Kumbe walikuwa na ajenda wanaifahamu. Na katika kutudhihirishia hilo wamekata jina la Msoka”

Aidha, Mkazi mwingine Nanzia Irigo amesema, “Kata ya Bwambo tumeonewa kwa muda mrefu. Kila tukienda kwenye kura za maoni tukichagua mtu, wenzetu wa Kitongoji cha Bwambo wanatufanyia hila. Mwaka 2005, tulimchagua Mann Fred walimkata na kumleta Christopher Irira. Safari hii hatukubali.”

Mwaka huu maccm hakuna rangi wataacha ona, ccm mpya ya Dr.jiwe inayoongoza kwa rushwa lazima imfie mikononi.
 
Hao wananchi wanatakiwa wajue wanafikidha salamu kwa mwenyekiti wa chama na sio Rais.. japo ni mtu mmoja lakini kuna utofauti hapo
 
CCM wanachopaswa kufanya, wpitishwe wote waliopita Kwa Kura za wananchi wajumbe kihalali, waliotoa Rushwa ndio waenguliwe, la sivyo wajue wanamlisha kuku wa jirani
 
A.k.
Wanachama wa CCM wakiwemo Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa Kata ya Bwambo Wilayani Same, Kilimanjaro wameandamana kumpinga mgombea aliyeshika namba 2 kwenye kura za maoni na kupitishwa na Halmashauri Kuu kugombea Udiwani

Mshindi wa pili, Gerald Ngale alipata kura 83 na mshindi wa kwanza ni Ahiya Msoka aliyepata kura 117. Wanachama walionekana Mtaani wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali

Wanachama hao wamemuomba Rais Magufuli na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Bashiru Ali kuingilia kati suala hilo na kusema kuwa wanamtaka aliyeongoza kwenye kura za maoni na sio mshindi wa pili aliyepitishwa

Mmoja wa Wanachama hao, John Piniel amesema “Tunataka Viongozi Wakuu wa Chama chetu watusikie, kwa awamu hii hatutanyamaza, hatutavumilia kwasababu Katiba ya Chama inasema kuwa kura ndio inatupa Kiongozi. Waliotuwakilisha kwenye kura za maoni wamefanya kazi tuliyohiyaji na kumchagua Msoka.”

Ameongeza, “Baada ya Msoka kuchaguliwa, tulipokuwa tunashangilia, Viongozi wa juu wa Chama kwenye Kata hii wakatuambia tumepiga vigelegele kwa mtoto kuzaliwa wakati bado hajalia. Kumbe walikuwa na ajenda wanaifahamu. Na katika kutudhihirishia hilo wamekata jina la Msoka”

Aidha, Mkazi mwingine Nanzia Irigo amesema, “Kata ya Bwambo tumeonewa kwa muda mrefu. Kila tukienda kwenye kura za maoni tukichagua mtu, wenzetu wa Kitongoji cha Bwambo wanatufanyia hila. Mwaka 2005, tulimchagua Mann Fred walimkata na kumleta Christopher Irira. Safari hii hatukubali.”

View attachment 1542217
Cuf ya Lipumba.
 
Bila kukatana mitama hamna kiti hao. Mwanaume ili uoneshe umekasirika kata mtu mtama kama alivyofanya mchomvi na kule dodoma
 
Back
Top Bottom