Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Natembea sana nje ya Tanzania. Natembea sana ndani ya Tanzania. Najua dunia inaenda wapi na inahitaji vitu gani kwa sasa!
Kwa maeneo mengi ya nje ya Tanzania niliyotembelea, Tanzania inasemwa vizuri saivi, hali ya kuvutia uwekezaji wa ndani na nje inasemwa kuwa nzuri sana!
Hata Dar ambapo ndo kitovu cha uchumi wa nchi, saivi tunaona miradi mingi ikifufuka. Ujenzi wa shopping malls unaendelea vizuri, njia ya Rose Garden, Kawe Housing Project, Morocco Square, Kijitonyama Road unaona project kubwa za ujenzi zikiendelea. Project hizi zinaonesha uhai kwenye ukuaji wa uchumi kwa sababu zinahusisha sekta binafsi na sekta ya umma tofauti na Dodoma ambapo miradi mingi ya ujenzi wa miradi inafanywa na Serikali tu.
Pamoja na haya yote kuna changamoto kubwa naiona mbeleni kwa Tanzania, nayo ni wanasiasa kuwa na nguvu kuliko mifumo ya nchi. Tatizo hili linatifanya tusiwe na uhakika wa kasi ya ukuaji wa uchumi kwa muda wote. Pia inafanya mifumo kufanya kazi kwa kuangalia mtu na sio mifumo yenyewe.
Mapungufu ya Samia yanaweza kurekebishwa na mifumo imara. Na mifumo imara ya kikatiba ndicho kitu pekee kitakachotuwezesha kupata maendeleo ya uhakika kwa muda mrefu bila kuwa na hofu yeyote au uharibifu wowote.
Napenda kumaliza kwa kusema. Bado tunahitaji Katiba Mpya ambayo ni bora ili kutuhakikishia tunakuwa na mifumo imara itakayosimamia viongozi wetu vizuri na kutuhakikishia maendeleo wakati wote.