tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Hata ikija katiba mpya bado hakutakua na jipya. Uondoe ushindani, ufunge jela wapinzani wako, uteke na kuua, alafu usuburi katiba mpya ndio kuja kuwa nzuri ili kuleta haki?Ni vigumu kuwaamini mpaka tujionee kwa macho.
Nilimuuliza mwanaccm, hii mnayosema katiba mpya itakua na jipya gani ikiwa mmeshateka na kuua, mmefunga wapinzani mmebaki wenyewe, alafu ndio mtakuja na katiba bora?Kwenye tume huru ya uchaguzi ametuletea kiini macho! Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kumuamini kirahisi tu. Hiyo Katiba mpya ataibadilisha jina tu, ila maudhui yake yote yatakuwa ni yale yale ya Katiba mbovu ya mwaka 1977!
Na katika hili, wananchi hatuko tayari kuendelea kuburuzwa na pia kuchezewa akili na wanasiasa wachache wabinafsi ndani ya nchi yetu.
Katiba ni yetu sisi Wananchi na sisi ndio tunatakiwa tuwe wakali pale Katiba inapokiukwa bila kujali itikadi na uvyama wetu.Hata ikija katiba mpya bado hakutakua na jipya. Uondoe ushindani, ufunge jela wapinzani wako, uteke na kuua, alafu usuburi katiba mpya ndio kuja kuwa nzuri ili kuleta haki?
Katiba ya CCM nani anaitaka? Katiba ya Mafisadi nani anaitaka?Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa mchakato wakupata Katiba mpya utakaika katika kipindi cha awamu ya sita.
Soma pia: Samia: Tutaendeleza mchakato wa Katiba Mpya kama ilivyo katika ilani yetu ya CCM
View attachment 3486629
“Pamoja na hayo CCM inatambua kwamba zaidi mshikamano wa Watanzania kwa kukamilisha mchakato wa Katiba mpya kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani yetu ya 2025-2030, haya ni matakwa ya makundi mbalimbali ya Watanzania kwa nyakati tofauti, tulijaribu wakati wa awamu ya nne mchakato haukukamilika, awamu ya sita tunaenda kuendeleza mchakato huo,” amesema Samia.
Samia amebainisha hayo leo, Ijumaa Oktoba 10, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Mwenge, Wilaya ya Butiama mkoani Mara na kuongeza kuwa hawatakubali nchi iyumbe kwa kisingizio chochote kile.
Ile rasimu ya Warioba vipi?Katiba ya CCM nani anaitaka? Katiba ya Mafisadi nani anaitaka?
CCM hawawezi kutuba Katiba bora kamwe? Nani wa kutupa Katiba bora? Hawa wanaojinufaisha kwa Ufisadi??
Hakuna CCM wa kukupa hata Katiba ya Warioba wewe.Ile rasimu ya Warioba vipi?
Never......never labda JK akinyongwa....au Afe kibudu....ila aliwepo na remote anayo yeye hakuna kitu unafikiiiMgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa mchakato wakupata Katiba mpya utakaika katika kipindi cha awamu ya sita.
Soma pia: Samia: Tutaendeleza mchakato wa Katiba Mpya kama ilivyo katika ilani yetu ya CCM
View attachment 3486629
“Pamoja na hayo CCM inatambua kwamba zaidi mshikamano wa Watanzania kwa kukamilisha mchakato wa Katiba mpya kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani yetu ya 2025-2030, haya ni matakwa ya makundi mbalimbali ya Watanzania kwa nyakati tofauti, tulijaribu wakati wa awamu ya nne mchakato haukukamilika, awamu ya sita tunaenda kuendeleza mchakato huo,” amesema Samia.
Samia amebainisha hayo leo, Ijumaa Oktoba 10, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Mwenge, Wilaya ya Butiama mkoani Mara na kuongeza kuwa hawatakubali nchi iyumbe kwa kisingizio chochote kile.
Ngoja tuone 29/10Hakuna CCM wa kukupa hata Katiba ya Warioba wewe.
Na mali za Umma wanazoiba na kujinufaisha na familia zao wakupe Katiba mpya iliyo bora ili iwaahughulikie?
Hawa dawa pekee kwao ni kuwaondoa madarakani hiyo Oktoba 29
Nitakua front line nikiwa nimebeba bango kubwa nikisubiri risasi kutoka kwa wale wauaji watesaji watekajiNgoja tuone 29/10
Katiba haiwezi kuwa yetu, Bali ni yaoKatiba ni yetu sisi Wananchi na sisi ndio tunatakiwa tuwe wakali pale Katiba inapokiukwa bila kujali itikadi na uvyama wetu.
Wananchi wanatakiwa wapewe elimu ili waelewe Katiba ya nchi lakini hivi sasa wananchi waliowengi hawana uelewa wa Katiba yao ndio maana inakiukwa inakanyagwa na wao wanachojali ni Simba na Yanga.Katiba haiwezi kuwa yetu, Bali ni yao
Katiba imekiukwa sana huo ukali wa wananchi upo wapi?
Watu mnnashindwa kuelewa kuwa na katiba ni jambo moja na kuifuata ni Jambo lingine. Unafikiri katiba ya sasa inaruhusu watu kutekwa na kuuwawa?
Hii tu iliyopo hakuna anayeifuata
Utakuwa katika Mji au Kijiji gani?Nitakua front line nikiwa nimebeba bango kubwa nikisubiri risasi kutoka kwa wale wauaji watesaji watekaji