Pre GE2025 Samia atangaza kuchangia Milioni 20 ujenzi wa kanisa la Masanja Mkandamizaji la "Feel Free Church"

Pre GE2025 Samia atangaza kuchangia Milioni 20 ujenzi wa kanisa la Masanja Mkandamizaji la "Feel Free Church"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Rais Samia ametangaza kuchangia Milioni 20 Ujenzi wa kanisani la Feel Free Church la Mchekeshaji Masanja Mkandamizaji.

Soma pia: Rais Samia Achangia Milioni 100 katika Ujenzi wa Kanisa la AICT

Samia ametangaza mchango wake huo kupitia akaunti yake ya X

IMG_0041.jpeg
 
Rais Samia aahidi kutoa Milioni 20 kusaidia ujenzi wa kanisa la Masanja Mkandamizaji

"Emmanuel, ahsante kwa dua njema kwangu na nchi yetu. Wasaidizi wangu watawasiliana nawe kuhusu ombi la kuchangia ujenzi wa Kanisa, na kukupa mchango wa shilingi milioni ishirini. Nawatakia kila la kheri katika kukamilisha ujenzi na kutoa huduma mkizingatia sheria, mila na desturi za nchi yetu."
IMG_2026.jpeg
 
Rais wa TZ kumbe ana hela nyingi eee, mshahara wake unafikia bei gani? au hizi anatoa ni za umma?? kwa mwaka anatakiwa atumie ngapi shughuli za kijamii?
 
Her Excellency President Samia Suluhu Hassan the COMFORTER OF THE NATION !
 
Hayo anayofanya kama ni pesa zake wala hakuna shida ila kuna huku pengine panapwaya ambapo ni wajibu wake wala sio Hisani..., Watu hawana Ujira wa kuweza kuendesha maisha yao wakati bado wanakamuliwa..




NB: Tunaweza kujikuta tunafanya yale ambayo ni kwa mapenzi yetu / Hisani (well and good) Lakini tukaacha yale ambayo ni wajibu wetu na ni lazima kuyafanya
 
Back
Top Bottom