GE2025 Samia: CCM tunataka ushindi wa heshima tuwazibe midomo wale wengine

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ushindi wa heshima kwa ushindani gani, huo wa kushindana na Salum Mwalimu? Hizi pombe za mchana hizi ni shida sana.
 
Sasa ushindi wa heshima ni wa kushindana na akina Salumu Mwalimu kweli??? Bora hata Mpina angekuwepo?? Huyo Mwalimu kura nyingi atakazopata ni za watu wa huko kisiwandui,bububu,mwanakwerekwe n.k. Nchi ngumu sana hii. 😀 😀 😀
 
Mungu atakuwa kasahawaziba midomo nyi kabla ya hayo matokeo

Watch ...it's very close...
 
Hamna haja hata ya kupiga kura, mtu unashindana peke yako utashindwaje sasa.
 
Na huyo ni Rais wa Wote ambaye hata akishinda inabidi awe kiongozi wa Wote ili kukusanya Nguvu za Wote kwenye Common Goals za Kupambana na Maadui zetu (Umasikini, Magonjwa na Ujinga) LAKINI anaongelea WALE / WAO na kuzibana Midomo as if kuna watu Sio walipa Kodi au amesahau ni pesa zao ndio zinamuweka Mjini
 
Ushindi wa heshima ni kama wa Ruto 51% vs Raila 48% huo ushindani ata Jumuia ya kimataifa itakuheshimu,,,ila Samia 98% afu Mwalimu 2% hiyo ni takataka
 

Wasifanye MAKOSA wakampa Maza percentage ndogo kuliko ya JPM 2020. Itakuwa ni aibu ya Mwaka. KURA YA "YES NAND NO"
 
Wakuu,

Hivi ushindi wa heshima ndio ukoje? CCM wanashindana wenyewe, sasa heshima hapo ipo wapi? Heshima ni kushinda wakati mpinzani wako mkuu umemtia lokapu? Au ule wa kusepa na kijiji huku tunajua kura zimeibwa?

=====

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni tarehe leo Septemba 23, 2025, Mangaka, wilaya ya Nanyumbu, mkoa wa Mtwara amesema chama hicho akina shida na ushindi kwa kuwa ni uhakika lakini watu wakapige kura ili kuwafunga midomo wale wengine.
Your browser is not able to display this video.
 

..Ushindi wa heshima bila ushindani wa kweli, na mchakato ulioendeshwa kwa haki na usawa?
 
Anashindana na nani hivi huyu mwanamke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…