"Samia must go" kampeni iliyofeli baada ya kutamkwa

"Samia must go" kampeni iliyofeli baada ya kutamkwa

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
441
Reaction score
1,065
Wengi hatufurahishwi na kinachoendelea nchini kwasasa. Utekaji na mauaji kwa watu wasio na madhara kwa serikali ni uonevu na kujiabisha kama nchi. Hili lazima lidhibitiwe

Huenda yanayosemwa ni kweli kwamba nchi nyingi duniani zinautaratibu wa namna ya kushughurika na watu ambao ni threat kwa serikali.

Tuseme ni kweli halafu tujiulize hivi hawa wanaotajwa kina Soka, hao kina Sativa, yule mshikaji aliyechoma picha ya Rais na wengine wanaosemwa semwa kweli ni tishio kwa usalama wa nchi??

Nikaanza kujiuliza, hivi hawa watu wana hata uwezo wa kutishia maisha ya mwenyekiti wa mtaa? Wanaweza kumfanya afisa mtendaji ashindwe kutimiza majukumu yake kweli? Sasa wanakuwaje threat kwa nchi?

Wanamiliki vikosi msituni? Wanawafuasi mtaani waliokunywa maji ya bendera zao? Wanaendesha mafunzo ya kupigana na serikali? au ni hii hii ya kupost post mtandaoni tu?

Any way, tuachane na hayo turudi kwenye mada. CHADEMA wamekuwa na kampeni nyingi mtaani ambazo ki uhalisia matunda yake ni kidogo sana

Hii haimaanishi kuwa wananchi wengi wanakubaliana na serikali, la hasha! Kilichopo ni kwamba wananchi wanapelekwa kwenye maandamano halafu hali inabaki vile vile na maisha yanasonga. Hii inachosha

CHADEMA imeshindwa kufanya ubunifu wa kuteka hisia za wananchi na kuwaingiza kwenye mfumo wanaoutaka.

Maandamano yalishadhihirika kuwa sio utamaduni wa watanzania na serikali haiogopi hayo maandamano kwasababu wanaoandamana hawaathiri shughuli za serikali.

Serikali haiwezi kutetemeshwa na waandamanaji wasio na ajira!

Waandamanaji wanapokuwa barabarani, wagonjwa hospitalini wanaendelea na matibabu, shuleni walimu wanafundisha, ofisini zote shughuli zinaendelea kama kawaida. Sasa hapa serikali itatetemeka kwa lipi?

Soma Pia:
Sana sana watapewa na polisi wawasindikize kulinda maandamano yao na baadae CCM wataanza kujigamba kwamba nchi ni ya kidemokrasia kwasababu watu wako huru kuandamana.

Itakuwa ajabu polisi wakileta mbwembwe zao za taarifa za kiitelijensia kuzuia maandamano ambayo agenda yake imekwisha feli hata kabla ya maandamano yenyewe kufanyika.

Kwanini nasema yamekwisha feli?

Hivi "Samia "asipo go" nini kitafanyika? Hata hao wenyewe wanaosema "Samia must go" hawaamini kwamba "Samia ata go". Sasa kwanini uje na kitu unachoamini hakitekelezeki?

Ili kuleta impact, inabidi wabuni namna nyingine ya kuendesha kampeni zao vinginevyo hii ya "Samia must go" ni mwendelezo wa kufeli kabla ya kutekelezwa
 
Assume kwanza Tanzania bila chadema itakuwaje?
Sikatai wanafanya kazi kubwa sana, lakini haiwafanyi waache kuwa wabunifu kuendelea kulisaidia Taifa.

Kwa mfano, tunaelekea uchaguzi wa serikali za mitaa. Wamejiandaa na mkakati gani madhubuti baada ya kushindwa kuzuia mkurugenzi kuwa msimamizi? Tusubiri kuwaona wakisusia uchaguzi tena? Kususia uchaguzi inasaidiaje nchi

Hivi karibuni tunashuhudia mawakala wa CCM wakipita mitaani nyumba kwa nyumba na kwenye kila penye kundi la watu kusajili wanachama kidigitali. Bila aibu wanapenya hadi kwenye shule za sekondari kwenda kuwasajili wanafunzi wawe wanachama kwa lazima

Wanajua kwanini CCM wameamua kufanya huo usajili kipindi hiki? Wanajua kwanini wameamua kusajili hadi wanafunzi wa sekondari tena kwa kuwalazimisha?

Haya yote kama chama mbadala ilitakiwa wajiwekee strategiea madhubuti za kupamba na CCM hadi washindwe kupata usingizi
 
Umesahau bakabaka kufanya usafi barabani kisa UKUTA, na siku ya kupanda miti Umesahau ililetwa kwa sababu gani?

Sisi watanzania tunajua haki zetu ila tunapenda kumwachia Mungu 🙄 wanyonge.
 
Sikatai wanafanya kazi kubwa sana, lakini haiwafanyi waache kuwa wabunifu kuendelea kulisaidia Taifa.

Kwa mfano, tunaelekea uchaguzi wa serikali za mitaa. Wamejiandaa na mkakati gani madhubuti baada ya kushindwa kuzuia mkurugenzi kuwa msimamizi? Tusubiri kuwaona wakisusia uchaguzi tena? Kususia uchaguzi inasaidiaje nch...
Mzee unajua kuchimba ...nimeiona point yako
 
Chadema hawajawahi fanya maandamano kuzuia shughuli za serikali.... aina ya maandamano uyatakayo huja watu wakijitambua bila kujali vyama vyao
 
Chadema hawajawahi fanya maandamano kuzuia shughuli za serikali.... aina ya maandamano uyatakayo huja watu wakijitambua bila kujali vyama vyao
Nadhani sasa shughuli yao kubwa ingekuwa kuwafanya watu wajitambue kwanza na kubeba agenda ya nchi badala ya chama
 
Rais asiyetambuwa kuwa ni custodian wa usalama wa raia, afaa kitu gani?
 
Back
Top Bottom