Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri

Njaa mbaya sana

Ridhika na mkate wako wako wa kila siku hiyo ndio riziki yako

Kama kipo kikubwa zaidi kitakuja tu we ishi kwa misingi ya haki na ukweli kikubwa unachokitumaini kitakuja tu

Propaganda hazitakuinua never kinyume chake zitakupoteza
 
We ni mwandishi gani wa habari,gazeti halikumsakama bali lilikuwa linatimiza wajibu wake wa kiuandishi wa habari
 
Pascal una lugha chonganishi sana Kaka, Magufuli hakuwahi kusakamwa sema hamkutaka kuambiwa ukweli. Yote yaliyozungumzwa yalikuwa kweli na kweli tu, ndio Maana hata Samia kaanza kuwaondoa watu wa karibu wa Magufuli, hili tu linatosha kuhitimisha kuwa Magufuli alikua na mambo mengi kama unga wa ngano
 
Hawa ni kinyongo chao ilikuwa inshu ya madini, ndio sheria zimesha andikwa, hata aje nani zitaendelea tu ...
Mbona mimi ni mkulima tu lakini nakubaliana nao kwa asilimia mia, kuwa huyu mama kamwe hawezi kuwa mbaya zaidi ya meko?je na mimi nina ishu ya madini?!!acha hizo, eti zimeshaandikwa hiyo ni biblia??mangapi mazuri aliyakuta huyo meko, akaja kuyavuluga?jana bungeni umesikia juu ya sheria ya bodi ya mkopo??tayari wamekubali kuiangalia upya, pole pole tu, mambo mengi yalitungwa kwa ajili ya mtu mmoja tu.
 
Paschal unacheza na wakati vipindi, ahahaha...

Ulipamba sana kipindi kile ila leo unapabomoa, now umeanza kujenga wakati huu, hebu ngoja tusubiri tuone😁!.
 
Vifo vya vigogo vilivyofatana mwaka huu chanzo chake ni corona.
OVER
Kwani haya ya hili gazeti si yanaandikwa na yule kibaraka wao aliyekuwa akitumiwa pesa ili awape vijana kumchafua JPM kwenye mitandao ya kijamii? Bahati mbaya baadaye aliposhtukiwa akashtakiwa kihalali kwa kutakatisha pesa? Ulitegemea aandike nini baada ya rais mwingine kiingia madarakani? Ajue tu kuwa hata akijipendekeza vipi historia yake ipo na akirudia transactions zake za money laundering yale yale yatamrudia.
 
Serikali inajua nini kifanyike katika kusimamia mambo ya nchi, kuhusu Covid-19 si lazima tufanye kama walivyofanya wenzetu, hakuna mtu aliyekatazwa kujitenga mwenyewe, hakuna mtu aliyekatazwa kuvaa barakoa, hakuna mtu aliyezuiwa kusafiri kwenda kutafuta chanjo kama inaihitaji. Tuwaheshimu viongozi wetu ndipo nao viongozi watakapokuwa na huruma kwa wanaowaongoza. Sisi ni mashahidi tuliona jinsi gani wale waliyokejeli na kudhihaki viongozi kwa kisingizio cha upinzani tumeona yaliyotokea. Huenda Pascal ni mwanahabari mahiri lakini si mwanasiasa au mwanadiplomasia makini. Na si kila habari inayoandikwa kwenye magazeti ya nje inapaswa kusomwa na watanzania au kuichambua na kuijibu kwani huwezi kumrushia mawe kila mbwa anayebweka hutoweza fika anapopakusudia kwa wakati. Naomba tujikite sana katika habari za ndani ili tuweze kuchangia mawazo katika kuleta maendeleo. Ikiwa tutaamini Covid-19 ni tatizo basi tuwaachiye wataalamu wa afya wafanye yao na tuwache kufananisha kati ya mtu na mtu au taifa na taifa. Mungu ibariki Tanzania.
 
Wewe nae unakera kujipendekeza. Huja jifunza lolote kwa Magufuli ambaye licha ya kujipendekeza kwako kucha kutwa alikupuuza na hakukuteua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…