Samsung Galaxy One UI feature set

Reuben Challe

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
2,940
Reaction score
5,511

Samsung Galaxy One UI, sio jina geni kulisikia, si ndio?
Hii ni software inayotumika kwenye simu na tablet za kampuni ya Kikorea Samsung.
Samsung walipoanza kutengeneza simu mwaka 2008 walikuwa wanatumia software ya Touchwiz, baadae wakahamia Samsung Experience na mwaka 2008 kwa mara ya kwanza wakatuletea software ya One UI kwenye Samsung Galaxy S9. One UI imeleta mapinduzi makubwa kwenye simu za Samsung kwa sababu imeleta improvements nyingi na kufanya iwe miongoni mwa software bora zaidi kwa simu duniani. Leo hii One UI ina features nyingi na customization kuliko software yoyote ile ya simu. Binafsi naipenda kuliko iOS.
Software ninazozipenda sana binafsi ni Xiaomi's HyperOS, Huawei's HarmonyOS, Samsung's One UI na Oppo's ColorOS.
Kwa sasa nataka niiongelee One UI. Sio kuelezea historia yake au kuichimba sana, nataka tu nitaje features zake.

Bila kupoteza muda naanza kuorodhesha features za software hii kutoka kwenye kampuni ya Korea Kusini.

1. IMAGE COPY AND PASTE

Hii feature ipo kwenye One UI 3.1 kwenda juu. Ni kwamba unaweza ku copy picha kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwenye simu yako. Kwa mfano kama umepiga picha ya mtu aliyesimama mbele ya garden, unaweza kumhold mtu huyo kwa kidole chako halafu unagusa option ya Copy. Baada ya hapo swipe kwenda kwenye image nyingine halafu ihold hiyo image then chagua "Paste" Huyo mtu atatokea kwenye hiyo image nyingine uliyo paste picha. Hapa maana yake unaweza kupiga picha upo bafuni halafu ukauhamisha mwili wako kwenda kwenye picha ya jangwani halafu una paste unaonekana upo jangwani. Pia unaweza kuongeza au kupunguza ukubwa wa picha ya mwili wako ili ufit vizuri kwenye image unayo paste.

Feature hii haijaishia hapo. Unaweza ku copy picha kutoka kwenye simu moja ya Samsung na ukaipaste kwenye simu nyingine ya Samsung au tablet. Easy sharing


2. LOCK SCREEN CUSTOMIZATION

One UI inakupa option nyingi sana za ku customize lockscreen. Kwenye lock screen ya Samsung kuna option ya kuweka widget za Battery, Calendar, Clock, Reminder, Samsung Health, weather nk. Hapa kwa mfano ukichagua clock zinakuja widget nyingi za clock katika style tofauti tofauti kwa hiyo unaangalia ipi unaipenda. So unaweza kuremba lock screen na widget nyingi nyingi na kila widget unaweza kui-resize kuifanya iwe na ukubwa unaoutaka wewe. Unaweza kubadilisha na fonts za clock pia. Kuna option kibao za fonts wamekuwekea pale na usiporidhika nazo unaweza kudownload fonts nyingi zaidi kwenye Galaxy Store

Kwa wale wapenzi wa Always On Display (AoD), kwenye Samsung sasahivi unaweza kuchagua wallpaper itumike ku display AOD badala ya ukuta mweusi kama ilivyo kwenye UI nyingine. Huku ni wewe unaamua black wall au your favorite wallpaper ndio itumike kwa AOD. Na option za wallpaper zipo nyingi
Kwenye lock screen ya One UI kuna option ya Effects ambayo inakuruhusu kuipa wallpaper yako effects tofauti tofauti kama iwe ya bluu yote, au wallpaper iwe inang'aang'aa nk.
Kuna option ya frame kama kwenye picha hapo juu, ambayo hii inakuwezesha kuwekea frame wallpaper ya kwenye lock screen yako. Frame zipo nyingi nyingi za shape tofauti tofauti, unachagua shape unayotaka. Pia unaweza kuchagua rangi ya kuweka kwenye background ya frame. Kijani, njano, bluu, zambarau, pinki, nyeusi, dhahabu au nyekundu ni wewe tu. Unaweza kuminimize ukubwa wa picha au uka enlarge picha iwe kubwa hadi itoke nje ya frame, kisha unaanza ku customize background vile inafaa.

3. GALAXY AI

Samsung imeleta Galaxy AI kwenye S series sasahivi na imeleta features nyingi za kuvutia
Baadhi ya feature hizo ni

*AI Summarization
Mfano ukikutana na habari au article yoyote mitandaoni na ni ndefu sana unaona uvivu kuisoma yote basi Galaxy AI itakupa summary ya kinachoongelewa hapo. Itakuwa rahisi kwako kusoma vitu vichache na kupata ujumbe kamili.

AI Summarization haijaishia hapo. Angalia hii picha hapo juu. Hapa kinachofanyika ni kwamba kama kuna audio inayoelezea mada fulani Galaxy AI itasikiliza hiyo audio au voice note na ita summarize kinachoongelewa. Amazing!

* AI Interpreter

AI interpreter inasaidia kuelewa lugha inayoongelewa na watu wengine halafu wewe huijui. Kwa mfano ukiwa kwenye mkutano halafu watu wanaongea Kichina kwenye mkutano, AI itasikiliza na kukupa tafsiri ya wanachokiongea kwenye simu yako, katika muda huohuo. Hii itakusaidia sana siku ukienda kutembelea jamii nyingine mfano Japan ambapo watu wengi hawajui Kiingereza. Unaweza kuwasiliana nao kwa msaada wa Galaxy AI.

*AI Live Translator

Hii inakuwezesha ku translate calls zako. Unaweza kuongea na mtu kwenye simu, yeye akawa anaongea Kihispaniola wewe unamjibu kwa Kiswahili. AI itakuwa inawasikiliza huku inawapa translation papo hapo.

* Circle to Search

Feature hii imekuwa connected na Google Lens directly. Ukiona kitu labda hukijui, iwe Facebook, Instagram, X, Youtube au kwenye Gallery yako unaweza kukizungushia tu duara halafu AI itasaidia kusearch kitu hiko across the web.

*AI Wallpapers

Kwenye Samsung unaweza kuisimulia AI wallpaper unayoitaka ilivyo. Kisha AI itakutengenezea wallpaper tofauti tofauti kulingana na maelezo yako halafu utachagua ipi inakufaa

*AI Editing

Galaxy AI inaweza ku move object kwenye picha, kufuta objects kwenye picha, kubadilisha mwonekano wa mawingu, kukuza objects au kufanya ziwe ndogo na vingine vingi vya kuvutia.

Kwa sasa Galaxy AI ipo tu kwenye Samsung Galaxy S24, S24+, S24 Ultra, S23, S23+, S23 Ultra, S23 FE, S24 FE, Z Fold 5, Z Fold 6, Z Flip 5, Z Flip 6, Tab S8, Tab S8+, Tab S8 Ultra, Tab S9, Tab S9+ na Tab S9 Ultra. Sina uhakika sana na S22 series. Galaxy AI pia ipo kwenye baadhi ya saa za Samsung kama Samsung Galaxy Watch Ultra na Watch 7 ila haipo kwenye A series.

4. SLOW MOTION VIDEOS

Achana na kurekodi video za slow motion, hiyo simu nyingi zinafanya. Kuna hii feature ya kuhold video for slow mo kwenye gallery. Kama unaangalia video ukiihold video hiyo inaanza kwenda slow. Pia unaweza kuchagua kama video ina urefu wa dakika 4 mfano, unaweza kuset ukiplay ikifika dakika ya kwanza sekunde ya 46 ianze slow motiona hadi dakika ya kwanza sekunde ya 54 halafu iendelee ila ikifika tena dakika ya 3 sekunde ya 11 iende slow hadi dakika ya 3 sekunde ya 32. Basi ukiplay video hiyo itafuata sheria hizohizo ulizoweka wewe. Na kweli ikifika dakika ya 1 sekunde ya 46 video inaenda slow

5. DRAG AND DROP

Kama kuna picha gallery unataka kushare whatsapp, Facebook, Instagram au kokote kule unaweza kuihold picha hiyo halafu ukaivuta kama unaiburuza hivi (kudrag) kutoka kwenye gallery kwenda kwenye app nyingine mfano WhatsApp halafu ukai share picha hiyo. Unaweza kuchagua hata picha 20 halafu zote ukazibind na kuzidrag kama picha moja vile then una share kwenye app nyingine, na zote 20 zinatumwa kama inavyotakiwa. Insane!

Leo nimeanza na hizi 5 ika kuna mengi sana Samsung ina offer kwenye One UI. Kwa hiyo nitazidi ku edit hii thread mara kwa mara, ili niendelee kuongeza features hadi features zitakapokuwa nyingi, kama 30 hivi then nitaacha, maana kuna vingi hapa sijagusia mfano Goodlock, Themes, Samsung DeX, Color parlette, etc

Samsung One UI 7 Beta imetoka na features zinazidi kuongezwa. Mfano wamebadilisha style ya Control center kwenye One UI 7, sasahivi unaweza kuset app drawer iwe unascroll down application badala ya app drawer nayo kuiswipe kwenda kulia na kushoto kama homescreen.

One UI ni software nzuri sana. Nitaendelea siku nyingine.
 
SamsungšŸ”„
 
Kuna ile option ya ku-split screen, ni nzuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…