Samsung kuachana na Google kama Default Search Engine

Mzee wa kupambania

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2022
Posts
21,111
Reaction score
53,092
Imeripotiwa kuwa Samsung wana mpango wa kuanza kutumia Bing ya Microsoft kama default search engine.

Taarifa zinasema kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya AI chatbot ambapo ChatGPT iliyo chini ya Microsoft kuonekana kuwavutia wengi imefanya Samsung wafikirie kutumia Bing kama default search engine.

Kutokana na uamuzi huu Google itapoteza mapato yenye thamani ya $3 billion kwa mwaka kutoka Samsung

Jumatatu ya leo hisa za Microsoft zilipanda kwa 1.4% huku za Google zikishuka kwa 3.2%

Google bado ni search engine inayopendwa zaidi duniani ikiwa na matumizi kwa 90% na Bing ni chini ya 3%
 
Google is here to stay
 
Google sasa imekua ya kitoto mno! Hakuna features mpya wala nini...Hii ndio sababu Samsung anatoka huko kwani wamejaa watumiaji wa infinix,tecno na simu nyingine local
Waliridhika sana kutawala soko ona Microsoft wamewachallenge na hii chatGPT nao wamekuja na Bard chatbot ila kwa sasa inatumiwa Marekani na Uingereza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…