Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 620
- 1,240
Kim Kyung-Ah
Kampuni ya Samsung inayojihusisha kutengeneza vifaa mbalimbali vya kieletroniki, kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa miaka 86 iliyopita Wamemuweka mkurugenzi mtendaji mwanamke kutoka nje ya familia yao.
Hii inakua kwa mara ya kwanza katika historia ya Samsung ambapo mwanamke ataweza kuongoza kampuni kubwa ya Teknolojia, hii ni kuashiria mabadiliko makubwa katika muundo wake wa Uongozi na utamaduni wa shirika lao.
Uamuzi huu unakuja baada ya Samsung kupata changamoto kwenye soko la Kimataifa linalozidi kuwa na ushindani haswa katika sekta muhimu kama vile Semiconductors, AI na Teknolojia ya simu.
Toka kuanzishwa kwake mwaka 1938 na ikiongozwa na familia ya Lee hatimaye Leo hii ametokea CEO mwanamke toka nje ya familia yao.
#samsung #samsungtanzania #bongotech255