SoC03 Sanaa ni mama wa sayansi

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Jun 25, 2023
Posts
45
Reaction score
32
SANAA, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU ndiyo MAMA na CHANZO cha SAYANSI kwani pasipo SANAA, UBUNIFU NA TEKNOLOJIA; SAYANSI hukosa uhai hivyo ni lazima iwe dhaifu, isiyozaa matunda, inayozaa matunda dhaifu au iliyokufa kabisa. Ulimwengu umekuwa ukichukulia Wanasanaa kuwa ni vilaza na dhaifu mbele ya Wanasayansi kwa kigezo cha masomo na kozi anazosomea mtu, lakini UKWELI ni kwamba ukiona kitu kipya kimebuniwa na kuvumbuliwa hata kama ni dawa, kemikali, majengo, miundombinu, vyakula, vinywaji, na kadhalika ujue ni KIPAWA cha UBUNIFU, SANAA NA TEKNOLOJIA kilichopo ndani ya mtu aliyegundua.

JE! KWANINI SANAA, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU NI MAMA NA CHANZO CHA SAYANSI?
Katika ulimwengu huu, Somo la baiolojia linatambulika kama somo la sayansi linalofundisha kuhusu mwanadamu, sehemu za mwili wa mwanadamu, wanyama na mimea; lakini chanzo cha somo hili ni MUNGU Aliyetumia SANAA, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU Kuwaumba wanadamu, wanyama, mimea na sehemu zao za miili ndani na nje (Biblia Takatifu; Mwanzo 1:1-31)

Katika ulimwengu huu, Masomo ya fizikia na jiografia yanajulikana kama masomo ya sayansi yanayofundisha kuhusu masuala ya anga, mvutano, mazingira, maada, mwendo, mwanga na kadhalika; lakini chanzo cha masomo haya NI MUNGU ALIYETUMIA SANAA, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU KUUMBA ANGA NA MIANGA (Biblia Takatifu; Mwanzo 1:6-7), MAZINGIRA, DUNIA NA VYOTE VILIVYOMO (Biblia Takatifu; Mwanzo 1:1), MAADA; VIMIMINIKA ambavyo ni MAJI (Biblia Takatifu; Mwanzo 1:9) , HEWA ambayo ni PUMZI (Biblia Takatifu; Mwanzo 2:7), MVUKE ambao ni UKUNGU (Biblia Takatifu; Mwanzo 2:6)

Katika ulimwengu huu, Somo la Kemia linajulikana kama somo la sayansi linalofundisha kuhusu mabadiliko ya kikemikali (Chemical Changes), lakini SOMO hili lisingekuwepo kama MUNGU ASINGETUMIA SANAA YA UUMBAJI AMBAYO NI SANAA, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU KUUMBA miti ya matunda ambayo baada ya mti kuzaa matunda, matunda hukua na baada ya muda hubadilika na kuiva; kuiva kwa tunda ni kitendo cha mabadiliko ya kikemikali yaani tunda linapoiva haliwezi kurudia hali yake ya kwanza ya ubichi tofauti na mabadiliko ya kiumbo (fizikia) ambapo Maji yanaweza kubadilika na kuwa barafu lakini baadaye likayeyuka na kuwa tena Maji ambayo pia yanaweza kubadilika na kuwa mvuke ambao ukipoozwa unarudi tena kuwa Maji ambayo yakigandishwa yanaweza tena kuwa barafu.

Miti na mimea ni mfano mzuri wa mabadiliko ya kikemikali kwani mbali na matunda pia majani huchipua, huwa mabichi, hukauka, huanguka na kuwa mbolea ardhini na kamwe jani hili haliwezi kurudi tena mtini na kuwa chipukizi. Chanzo cha somo hili NI MUNGU Aliyetumia SANAA, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU KUUMBA miti na mimea, hewa na ukungu (gases), na kadhalika (Biblia Takatifu; Mwanzo 1:12) (Biblia Takatifu; Mwanzo 2:9)

Tafsiri yake ni kuwa, mwanadamu anaweza kuwa amesoma Fizikia, Kemia, Baiolojia, au Jiografia na hatimaye Akasoma Udaktari au Urubani au Ukemia au Uhandisi lakini bado ni Mwanasanaa mwenye KIPAWA CHA SANAA NA UBUNIFU wa Kubuni na Kuvumbua mambo mema, mazuri na mapya kupitia masomo haya ambayo chanzo chake ni SANAA NA UBUNIFU; iwapo atapata NEEMA YA KUWA NA HEKIMA YA MUNGU ndani yake na kuitumia katika Kufanya kazi yake ya Udaktari, Uhandisi, na kadhalika.

Hii ndiyo sababu hatutakiwi kuwatafsiri Wanasanaa na Wanasayansi kwa masomo wanayosoma, kozi wanazosoma, vitivo wanavyosoma na kazi wanazozifanya bali kwa aidha HEKIMA YA MUNGU au hekima ya wanadamu iliyo ndani ya mtu binafsi.

MWANZILISHI WA SANAA NA SAYANSI IKIWA NDANI YAKE NI MUNGU MWENYEWE. Mwanadamu alichofanya ni kuichepusha Sayansi na kuitumia kuipiga na kuiangusha SANAA pasipo kujua kuwa hakuna mtoto (Sayansi) atakayefanikiwa kumpiga mzazi wake (SANAA) pasipo MUNGU Kumuumbua. Hii ndiyo sababu sayansi imekuwa ikivutia kwake na kuviita vitu ambavyo si vya kwake kuwa ni vya kwake kwa sababu palipo na mawazo ya Mwanadamu nyuma yake yupo ibilisi ambaye anatamani kila kilicho cha MUNGU kiwe cha kwake lakini uzuri ni kwamba MUNGU Haibiwi.

Sayansi imefanya ulimwengu mzima udhani kuwa Udaktari ni Uanasayansi pasipo kujua kuwa Udaktari asili yake na chanzo chake ni SANAA ndiyo maana Daktari anapomfanyia oparesheni mgonjwa kwanza anampasua mahali husika na kisha baada ya kumaliza kazi yake anamshona kwa kutumia nyuzi pasipo kujua kuwa anachokifanya ni SANAA YA UFUNDI YA USHONAJI.

Pia Daktari anapomshauri mama mjamzito au mama mwenye mtoto kuhusu tiba lishe, usafi wa vyakula, maandalizi mazuri ya vyakula, hapa inayotumika ni SANAA YA UFUNDI YA UPISHI WA VYAKULA.

Miandiko ya Madaktari ni SANAA YA UFUNDI YA UANDISHI ili kuzipa faragha taarifa za mgonjwa.

Daktari anapowasiliana na mgonjwa haanzi kuzungumza yeye, ndiyo maana mgonjwa anapofika kwa daktari, daktari anaanza kumuuliza enhe! Niambie nini tatizo? Mgonjwa anapojibu labda anahisi tumbo linamuuma bado Daktari atataka tena kujua hii hali ilimuanza lini? Mgonjwa atakapojibu ilimuanza siku moja au mbili au tatu zilizopita bado daktari atataka tena kujua, tumbo linaumaje? Linachomachoma au kama limejaa gesi au kama tumbo la kichefuchefu? Jibu la mgonjwa ndilo litamfanya Daktari aamue aidha mgonjwa akapime minyoo, amoeba, typhoid au vidonda vya tumbo. Kumbuka wakati mazungumzo yanaendelea, daktari anaandika maelezo kwenye daftari la mgonjwa. Haya yote yanafanyika pasipo kujua kuwa Daktari anatumia SANAA YA UFUNDI WA LUGHA; Mazungumzo (Speaking), Usikilizaji (Listening) na Uandishi (Writing) na hatimaye ndani ya akili yake daktari anatumia FASIHI ambayo ni TASWIRA au PICHA kuhisi kile ambacho mgonjwa anaumwa baada ya kuzungumza na mgonjwa, kumsikiliza na kuandika maelezo. Mambo hayaishii hapo, daftari linapokwenda maabara kwa yale maelezo aliyoyaandika Daktari kwenye daftari la mgonjwa kwa namna miandiko ya Madaktari ilivyo; inamlazimu Fundi Maabara kutumia SANAA YA UFUNDI WA LUGHA; Usomaji (Reading) ili aweze Kufanya kile ambacho kimeandikwa na daktari.

Maabara pia zinatumika SANAA MBALIMBALI ambapo;
Vifaa vyote vya Maabara vimetengenezwa kwa kutumia SANAA, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU. Fundi na Msanifu Maabara anapotumia vifaa hivi mfano Microscope anatumia jicho lake kutazama na kugundua majibu ya alichompima mgonjwa. Kile alichokiona kwa jicho lake la Ufundi ambalo mtu mwingine anapotazama ndani ya microscope anaweza asielewe chochote; anakitafsiri (Interpretation/Translation) kwanza kwenye ubongo wake kisha kwa mkono wake anaandika majibu kwenye daftari la mgonjwa kwa mwandiko ambao pia unatunza faragha ya taarifa za mgonjwa.

Vitendo vyote hivi anavyovifanya Fundi au Msanifu Maabara ni SANAA ZA UFUNDI pamoja na SANAA ZA LUGHA ndiyo maana anaitwa 'Laboratory Technician' tafsiri yake ni FUNDI MAABARA au MSANIFU MAABARA.

Zile tiba, sindano, huduma kama vile bandeji, plasta, ambazo mfamasia anamhudumia mgonjwa kuna watu ambao walitumia SANAA YA UBUNIFU NA UVUMBUZI ILI KUZIGUNDUA NA KUZITENGENEZA.

Vivyo hivyo Sayansi pia imefanya ulimwengu mzima udhani kuwa Uhandisi na Ukandarasi ni Uanasayansi pasipo kujua kuwa Uhandisi na Ukandarasi asili yake ni Uanasanaa ndiyo maana Mhandisi au Mkandarasi husanifu majengo, hujenga barabara, huchora ramani, wengine huchonga ramani kwa kutumia vitu mbalimbali, huandaa vipimo vya ujenzi, hukadiria uwiano wa vitendea kazi kwa ajili ya ujenzi, hutoboa miamba kupisha ujenzi wa miundombinu kama barabara, pasipo kujua kuwa anachokifanya Mhandisi au Mkandarasi huyu ni SANAA YA UFUNDI YA UCHORAJI, UCHONGAJI NA UJENZI.

Lakini pia Sayansi imefanya ulimwengu mzima udhani kuwa Urubani au Unahodha ni Uanasayansi pasipo kujua kuwa Urubani na Unahodha asili yake ni Uanasanaa ndiyo maana Rubani au Nahodha huendesha chombo cha usafiri. Kuendesha chombo cha usafiri asili yake ni SANAA YA UDEREVA (Driving) ambayo hufundishwa kwenye vyuo vya SANAA YA UFUNDI; tofauti ni kuwa kuna dereva wa vyombo vya usafiri vya nchi kavu, kuna dereva wa vyombo vya usafiri vya kwenye maji na kuna dereva wa vyombo vya usafiri vya angani hivyo kila mmoja anafundishwa SANAA YA UFUNDI STADI wa kukiendesha chombo chake cha usafiri kulingana na chombo husika na njia husika ya chombo hicho.

Hii ndiyo sababu inayofanya wasomi kuongezeka kila siku duniani kote, lakini maswali yanayokosa majibu na changamoto zinazoikumba dunia kuongezeka zaidi kila siku ulimwenguni kwa sababu dunia imeamua kuwaficha watu UKWELI unaowaelezea wao ni kina nani na wafanye nini ili walete matokeo Mapya, Mema na Mazuri ya kutatua changamoto zinazoikumba dunia kisha kuleta majibu sahihi ya maswali yaliyokosa majibu duniani.

Haya yote yanatokea kwa sababu tayari ki-saikolojia Dunia imeshamwambia Daktari kuwa yeye ni Mwanasayansi wakati MUNGU Anamngoja Daktari huyohuyo afahamu kuwa yeye ni Mwanasayansi sawa lakini chanzo na asili ya Sayansi ni SANAA na SANAA imo ndani yake Daktari huyu ili aweze kufanya Ubunifu na Uvumbuzi wa vitu vipya, mambo mapya, mambo mema na mambo mazuri kwa ajili ya jamii yake, taifa lake na ulimwengu mzima kwa kutumia Ustadi wake wa Udaktari.

Nia na Madhumuni ya kuelezea haya yote sio kuwashusha na kuwadharau Wanasayansi hapana, bali ni kuchochea na kuamsha ulimwengu uweze kutambua umuhimu wa ufanyaji kazi kwa UPENDO NA USHIRIKIANO kati ya Wanasanaa na Wanasayansi kuliko ulimwengu mzima kuwatazamia na kuwategemea Wanasayansi pekee kuwa ndio watatuzi na wafumbuzi wa changamoto zilizomo duniani huku Wanasanaa tukihesabika kuwa si kitu katika ulimwengu huu wakati MUNGU MWENYEWE NDIYE MWANASANAA NAMBA MOJA (Mwanzo 1:1-3) BWANA YESU KRISTO NDIYE MWANASANAA NAMBA MOJA; FUNDI STADI SEREMALA (Marko 6:2-3) NA ROHO YA MUNGU NDIYO HUMIMINWA NDANI YA WANADAMU ILI KULETA VIPAWA VYA SANAA NA UBUNIFU (Kutoka 31:1-6) (Kutoka 35:30-35)

By E.N
 
Upvote 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…