Sanaa ya ndizi iliyobandikwa ukutani kwa Duct-tape imenunuliwa kwa zaidi ya Tsh. Bilioni 16 (USD 6.2 million) katika mnada huko New York

Don Gorgon

Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
35
Reaction score
68

Banana.png

Sanaa yenyewe hii hapa
Mnada mmoja huko New York, Marekani, umeuza Sanaa iliyopewa jina la Comedian. Kazi hiyo ya sanaa imetengenezwa na msanii Maurizio Cattelan, na imeuzwa kwa dola za Kimarekani milioni 6.2, yaani zaidi ya bilioni 16 za Kitanzania.

Sanaa hii inahusisha ndizi ya kawaida iliyofungwa kwenye ukuta kwa mkanda wa gundi (duct tape) yenye rangi ya silva.

Mnunuzi alikuwa Justin Sun, mfanyabiashara wa sarafu za kidigitali, ambaye alinunua hati rasmi inayompa haki ya kurudia kazi hiyo kwa ndizi nyingine.

mnunuzi bwege tu kwani hiyo ndizi aliyonunua billioni 16 haiozi.!sio ajabu sahizi amejifungia chumbani anajuta na kulia kwa huo ulofa aliofanya kwa kutaka sifa za mda mfupi yaani mwenzio kanunua ndizi sokoni kwa shilingi 500 alafu ww unakuja kuinunua kwake kwa bilioni.! si bora ingekuwa hio ndizi ukila hutosikia njaa wala kuhitaji kula chakula mwaka mzima hapo kidogo ingeleta maana...kweli wajinga ndio waliwao baada ya siku kadhaa ndizi inaoza umefaidika nini hapo zaidi ya kujilaumu tu na kulilia mabillioni yako...
 
Daaah ila almajid bana..
Kwahyo wewe peke ako ndo umeona jamaa fala ila wengine hapo juu wameona poa tu sio...
😂😂😂😂😂😂😂

Haya majidi nikuulize swali... Unakulaga mchele mbichi
 
mnunuzi bwege tu kwani hiyo ndizi aliyonunua billioni 16 haiozi.!sio ajabu sahizi amejifungia chumbani anajuta na kulia kwa huo ulofa aliofanya kwa kutaka sifa za mda mfupi yaani mwenzio kanunua ndizi sokoni kwa shilingi 500 alafu ww unakuja kuinunua kwake kwa bilioni.! si bora ingekuwa hio ndizi ukila hutosikia njaa wala kuhitaji kula chakula mwaka mzima hapo kidogo ingeleta maana...kweli wajinga ndio waliwao baada ya siku kadhaa ndizi inaoza umefaidika nini hapo zaidi ya kujilaumu tu na kulilia mabillioni yako...
Mtu mwenye net worth 1.5 billion usd kibongo bongo nikama tirion 3 atokwe chozi Kwa kutoa billion 16 acha masihara basi
Na kitu kingine usichokijua hiyo ni mbinu ya kujitangaza(marketing) kama Kuna watu ambao walikuwa hawamjua Sasa wameshamjua na kashatangaza biashara zake
 
View attachment 3158954
Sanaa yenyewe hii hapa
Mnada mmoja huko New York, Marekani, umeuza Sanaa iliyopewa jina la Comedian. Kazi hiyo ya sanaa imetengenezwa na msanii Maurizio Cattelan, kwa dola za Kimarekani milioni 6.2, yaani zaidi ya bilioni 16 za Kitanzania.

Sanaa hii inahusisha ndizi ya kawaida iliyofungwa kwenye ukuta kwa mkanda wa gundi (duct tape) yenye rangi ya silva.

Mnunuzi alikuwa Justin Sun, mfanyabiashara wa sarafu za kidigitali, ambaye alinunua hati rasmi inayompa haki ya kurudia kazi hiyo kwa ndizi nyingine.

Kichaa cha pesa za kuzimu
 
NOTE:-
The purchase of high-priced art often raises questions about the motivations behind such transactions.
While there is no direct evidence to suggest that this particular purchase is linked to money laundering or tax evasion, art transactions at high prices can sometimes be exploited for these purposes.
 
"..i bought an artwork for 1 million, two years later that shit went for 2 million, three years later that shit went for 5 million, i can't wait to get that shit to my children.."

Jay z - story of O.J
 
Back
Top Bottom