Sanamu ya baba wa Taifa iliyo taaban ya azimio la busara la Tabora (uamuzi wa busara)1958

Sanamu ya baba wa Taifa iliyo taaban ya azimio la busara la Tabora (uamuzi wa busara)1958

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SANAMU YA BABA WA TAIFA ILIYO TAABAN YA AZIMIO LA BUSARA LA TABORA (UAMUZI WA BUSARA)1958

1568437828002.png
''Wengi wamesahau athari na alama za harakati za TANU na uhuru; wanafaidi uhuru na matunda yake wamesahau harakati zilizoleta uhuru.''
Bakari Maligwa Mohamed


Rafiki yangu kaniletea hiyo picha ya sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyoko Tabora inayoonyesha kumbukumbu ya Azimio la Tabora lakini iko hoi kwa kukosa matunzo.

Huu ni mkutano ambao Mwalimu Nyerere alihutubia na kutokwa na machozi na kuwaliza wote waliokuwapo katika mkutano ule.

Inasikitisha kuwa kumbukumbu hii iko katika hali mbaya lau kama ni sehemu muhimu katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes nilifanya mazungumzo na wazalenso wawili ambao walikuwapo katika mkutano ule na wakanipa historia yote kwa ukamilifu wake.

Nilizungumza kwanza na Bilal Rehani Waikela na Germano Pacha waasisi wa TANU Tabora kisha nikazungumza na mmoja waasisi wa TANU Tanga Sheikh Abdallah Rashid Sembe.

Mtu aliyesababisha mkutano huuu muhimu ufanyike Tabora na si kwengineko ni Peter Mhando ambae alikuwa mmoja wa waasisi wa TANU Tanga aliyehamishiwa TANU HQ New Street Dar es Salaam na kutoka hapo akahamishiwa Tabora kwenda kutatua matatizo ambayo yalikuwa yameigubika Tabora katika siku za mwanzo za chama.

Mkutano wa Tabora inasemekana ulikuwa na agenda 60 lakini agenda iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wajumbe wa mkutano ilikuwa suala la Kura Tatu.

Waingereza waliitisha uchaguzi ambao ulihitaji wapiga kura kupiga kura tatu akichagua Mzungu, Muasia na Mwafrika.

Pamoja na sharti hili kulikuwa na sharti la elimu, kipato na kazi inayokubalika.
Masharti haya yalikuwa ya kibaguzi na TANU ilitishia kuwa haitakubali kuingia katika uchaguzi ule.
Wapinzani wakuu wa Kura Tatu walikuwa Sheikh Suleiman Takadiri Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU na Zuberi Mtemvu.

Ilihofiwa kuwa ikiwa TANU hawatakubaliana katika suala hili la Kura Tatu chama cha TANU kitameguka na hii itarudisha nyuma juhudi za kupigania uhuru.

Matokeo ya mkutano wa Tabora kukubali kushiriki katika uchaguzi ule kwa haukukimega TANU lakini kwa hakika uamuzi ule ulisababisha kuundwa vyama viwili - African National Congress (ANC) chama alichokiunda Zuberi Mtemvu na All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT) chama kilichoundwa na Ramadhani Mashado Plantan na wenzake na Sheikh Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU akafukuzwa chama.

Historia ya Uchaguzi wa Kura Tatu ni kisa cha kusisimua sana hasa unapofuatana na Mwalimu Nyerere katika safari yake akielekea Tanga akiwa na Amon Kissenge hadi anafika Tanga na kufanya mkutano na viongozi wa TANU wa Tanga Hamisi Heri, Rashid Sembe na viongozi wengine wanakubaliana kuweka mkakati wa ushindi kuwaangusha wapinzani wa Kura Tatu na mwisho kufanya kisomo Mnyanjani na Nyerere akishiriki kuomba msaada wa Allah wazishinde njama za wakoloni.

Picha: Kumbukumbu ya Azimio la Busara, Tabora, Peter Mhando, Viongozi wa TANU kulia Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia wakiwa na Bantu Group, Baraza la Wazee wa TANU, Nyerere akipiga kura ya Kura Tatu na kitabu cha ''Uamuzi wa Busara.''

 

Attachments

  • 1568437736290.png
    1568437736290.png
    71.7 KB · Views: 27
Sisi tuliozaliwa enzi za tanu na kukulia enzi za CCM tunakuelewa sana, vijana hawa wa miaka hii wakina bashite, musiba, n.k. hawaelewi kitu ndiyo maana wanathubutu hata kumpiga makofi mzee warioba yaani mpaka tunatamani kulia
 
Acha porojo wewe,changia hoja,usianzishe upuuzi wako humu,eti warioba alipigwa na makonda!!!!? ,hili ni jukwaa la historia sio porojo na siasa za kipuuuzi.
 
Samahani mkuu, sasa hapa hawa wawili uliowataja, walikuwa wapinzani kivipi? Kamba walikuwa wanapinga hizo kura tatu, au walikuwa wanaziunga mkono?
[emoji116]
"Wapinzani wakuu wa Kura Tatu walikuwa Sheikh Suleiman Takadiri Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU na Zuberi Mtemvu"
 
Back
Top Bottom