Sanduku la Agano liko wapi?

Sanduku la Agano liko wapi?

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
Huu ni mfano wa sanduku la agano ambalo wana wa Israel waliambiwa watengeneze na Mussa wakiwa nyikani wakitoka Egypt (Misri) wakielekea promised land (Nchi ya ahadi). Sanduku hilo lilikuwa ni kama box la mbao lililotengenezwa na aina moja ya mbao inayoitwa (acacia wood) iliyofunikwa na dhahabu. Lilikuwa la urefu wa 1.15 metres, upana wa 0.7 metres na kimo cha 0.7 metres.

Ilikuwa inabebwa na mishikio miwili mirefu ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa mbao hiyo ya acasia ambazo pia zilikuwa zimefunikwa na dhahabu. Juu ya sanduku kuliwekwa makerubi wawili waliokuwa wamegeukiana mabawa yao yakiwa yamegusana. Uwepo wa Mungu haukuwepo ndani ya sanduku bali ulikuwa juu yake katikati ya hao makerubi.

Uwepo wa Mungu juu ya sanduku hilo ulikuwa kama nuru. Kuhani mkuu alipaswa kufunika macho asiione nuru hiyo ("hakuna mwanadamu anionaye na akaishi" Kutoka 33 : 20) kila alipokuwa akiingia lilipokuwa sanduku ambapo ni patakatifu pa patakatifu.

1619056122378.png

Hapa ndipo ambapo Mungu alipokuwa akiionana na Musa. Sanduku hili lilikuwa likibebwa na wana wa Walawi pekeyake hakuna mwingine aliyeruhusiwa kulishika, yeyote aliyedhubutu kulishika pasiporuhusiwa alikufa papohapo. Hao makerubi wawili wanawakilisha utukufu wa Mungu. Ndani ya sanduku hili kulikuwa na:
  • Mawe mawili yaliyokuwa yameandikwa amri kumi za Mungu
  • Fimbo ya Aron iliyoota mauwa
  • Chombo cha dhahabu kilichokuwa na manna waliyokula wana wa Israel nyikani
Sanduku hilo lilikuwa linakaa patakatifu pa patakatifu, chumba cha ndani kabisa katika hema la kukutania. Aliyekuwa anaruhusiwa kuingia mahala hapo lilipokuwa sanduku hilo ni kuhani mkuu na alikuwa anaruhusiwa kuingia mara moja kwa mwaka. Kabla ya Kuhani mkuu kuingia patakatifu pa patakatifu alikuwa ni lazima aingie na damu ya mwana kondoo kwa niaba ya dhambi zake yeye mwenyewe na dhambi za wana wa Israel.

1619056417114.png


Sanduku la agano lilikuwa ndani ya hekalu lililojengwa na Solomon mpaka hekalu hilo lilipokujwa kuvunjwa mikononi mwa utawala wa Babylon ukioongozwa na Nebuchadnezzar. Kilichotokea kwa sanduku hilo hakijulikani ingawa haiwezekani kuwa lilichukuliwa na majeshi ya Babylon kama vilivyochukuliwa vyombo vingine vya hekalu kwasababu katika list ya vitu walivyovichukua sanduku la agano halikutajwa.

Halitajwi kati ya vyombo vilivyopelekwa Babiloni hekalu lilipohabiriwa mwaka wa 607 K.K. wala halitajwi kati ya vyombo vilivyorudishwa Yerusalemu baadaye.—2 Wafalme 25:13-17; Ezra 1:7-11

Kulingana na baadhi ya vyanzo vya habari inasemekana kuwa mfalme Josiah, mmojawapo wa wafalme wa mwisho kutawala enzi za hekalu la kwanza, kutokana na unabii uliokuwa umetolewa alijua kuwa Jerusalem itavamiwa na Babylon, akalificha sanduku la agano.

Alipolificha sanduku imekuwa kitendawili. Chanzo kingine cha habari kinasema kuwa mfalme Solomon alionyeshwa kuwa Hekalu litakujwa kuvunjwa na majeshi ya Babylon, kwahiyo akaandaa pango karibu na bahari ya shamu (dead sea) ambapo Josiah akaja kulificha sanduku.

Na pia inasemekana nabii Yeremia (Jeremiah) alilificha sanduku chini ya Hekalu lililojengwa na Solomon.

HEKALU LA MBINGUNI
Kutoka 25:8,9 Hekalu la duniani lilikuwa ni mfano wa lile la mbinguni ambalo ni halisi Musa alilo onyeshwa mlimani,pia hekalu la duniani liliwekwa vyombo(thamani) sawa na lile la mbinguni.
Ebrania 8:5 Hekalu la mbinguni ni halisi ya lile lililojengwa duniani.
Ebrania 8:2 Hekalu la mbinguni limewekwa na Mungu mwenyewe.
Ufunuo 4:5; 8:2-4 Yohana aliona katika njozi, vyombo(thamani) za Hekalu la mbinguni sawa sawa na zile za Hekalu la duniani katika Patakatifu pa mbinguni.
Ufunuo 11:19 Yohana pia aliliona Sanduku la agano ( Sanduku hili la agano ndani yake mna "Amri kumi" za Mungu alizo zitoa pale kwenye mlima Sinai), Sanduku hili lilikuwa katika Patakatifu pa Patakatifu kwenye Hekalu la Mbinguni.
Ebrania 8:1,2 Kristo baada ya kujitoa kuwa kafara ya upatanisho wa dhambi, amekuwa Kuhani wetu Mkuu wa Hekalu la Mbinguni, kwa ajili ya kutuombea na kutupatanisha na Mungu.

9781611046823.jpg
 
Where the ark of covenant is, still a mistery, every scholar comes with a theory..lets stick to the fact that it wasn't taken by romans because with their relation to roman catholic it could have been given to church but church doesn't have it so romans didn't get their hands on it during the battle this implies that jews hiden it where no one really knows up todate..🙃
 
Babylon kuacha kitu vigumu itakuwa walilibeba nao wakalipeleka wanapokujua sababu zile amri10 tunazodanganywaga na zilibadilishwa kutoka mafungu10 ya elimu kutoka kwa waumbaji mpka amri ivi kuna mtu kushikilia amri aache elimu na nguvu iliyotunukiwa na waumbaji ivyo vitu walibeba kina nebkadneza na wanajua walipoweka na kama si kuweka kuna mataifa yanumia elimu hizo za waumbaji na nguvu zile sio amri ni kinyume cha elimu(mafunzo) na yameua sana vizaz na vizaz nitatolea uzi siku1
 
Kuna Documentary niliangalia ya BBC/aljazera sina uhakika,wanasema lipo Ethiopia,kuna hekalu Fulani limewekwa huko ndani na huko anayeruhusiwa kuliona na kulilinda ni mtu mmoja tu na Mara nyingi hatoki nje.

Nje ya Hekalu hilo lina ulinzi mkali sana na hata mwandishi mwenyewe kwanza ilibidi apate ruhusa ya kufika huko na hata alipofika aliongea na mtu mmoja tu aliyekuwa nje ndio akamweleza hayo yite na wala hakuruhusiwa kusogea karibu na uzio wa Hekalu.
 
Kuna Documentary niliangalia ya BBC/aljazera sina uhakika,wanasema lipo Ethiopia,kuna hekalu Fulani limewekwa huko ndani na huko anayeruhusiwa kuliona na kulilinda ni mtu mmoja tu na Mara nyingi hatoki nje.

Nje ya Hekalu hilo lina ulinzi mkali sana na hata mwandishi mwenyewe kwanza ilibidi apate ruhusa ya kufika huko na hata alipofika aliongea na mtu mmoja tu aliyekuwa nje ndio akamweleza hayo yite na wala hakuruhusiwa kusogea karibu na uzio wa Hekalu.
BBC ma Channel 4 wana documentaries nzuri sana.
 
Back
Top Bottom