SoC02 Sanduku la jamii [kero, matatizo, changamoto na mapendekezo]

SoC02 Sanduku la jamii [kero, matatizo, changamoto na mapendekezo]

Stories of Change - 2022 Competition

DENG XIAOPING

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2022
Posts
2,396
Reaction score
2,598
Awali ya yote yatupasa kufahamu nini maana ya maneno:- i, Sanduku
ii, Jamii
iii, Sanduku la jamii

SANDUKU
Ni kifaa au kasha lililo tengenezwa kwa mbao, chuma au karatasi gumu ambalo hutumika kupakia na kuhifadhia vitu mbalimbali ndani yake.

JAMII
Ni watu wanao ishi au kutoka sehemu moja ambao hushirikiana kwa pamoja katika mambo mbalimbali yakiwemo ya kitamaduni, kiuchumi n.k

SANDUKU LA JAMII
Ni kifaa kilicho tengenezwa kwa mbao ngumu au chuma imara kwa matumizi ya kuhifadhia kero, matatizo, changamoto na mapendekezo ya wanajamii kuhusu maeneo wanayo ishi.

17977_14232_2953.jpg

[Picha kutoka mtandaoni ikionesha mfanano wa namna sanduku la jamii linavyo paswa kuwa]

NAMNA SANDUKU LA JAMII LINAVYO PASWA KUTUMIKA
Utekelezaji wa sanduku la jamii una paswa kuzingatia mambo mbalimbali muhimu kama yafuatayo:-

i, Uwekaji wa sanduku la jamii mahali panapo fikika kirahisi na watu wote wa eneo husika.

ii, Uwekaji wa sanduku la jamii mahali palipo na uwazi na salama kwa taarifa za mwananchi [kero, changamoto, matatizo na mapendekezo] zinapo hifadhiwa. ili kuepuka upotevu wa taarifa hizo pia kumlinda zaidi mwananchi na taarifa atakazo kuwa ameweka kwenye sanduku la jamii.

iii, Uwekaji wa sanduku/masanduku ya jamii kulingana na ukubwa wa eneo la jamii husika.mfano uwekaji wa masanduku ya jamii katika kata utazingatia ukubwa wa kata na hivyo kutoa jawabu la idadi gani ya masanduku ya jamii yatakayo hitajika kwa kata nzima kutokana na ukubwa wa kata husika.

iv, Uandishi wa wananchi kuhusu changamoto, kero, matatizo na mapendekezo yao una paswa kuzingatia mambo ya msingi na ya kweli wanayo kumbana nayo ndani ya jamii zao na sio mambo ya kutunga na yasiyo faa mfano lugha za matusi, kuudhi, chuki n.k ili kuepusha migongano isiyo ya lazima kati ya wananchi na viongozi.

v, Uandishi wa changamoto zao wananchi una paswa kuwa mfupi au mrefu wa wastani katika mfumo wa vipeperushi au barua pepe ukieleza ni eneo lipi lenye changamoto mfano jina la kijiji, mtaa, makazi [ anwani ya nyumba ] n.k

vi, Sanduku la jamii linapaswa kutengenezwa kwa chuma imara lisiloweza kuharibika kirahisi na kwa muda mfupi na pia lisiloweza kupoteza yale yaliyo andikwa na wananchi yaliyo ndani yake.

vii, Sanduku la jamii linapaswa kuwa na maelekezo pembeni yake ili kumfanya mweka changamoto, kero, mapendekezo kuzingatia yaliyo elekezwa kwenye karatasi la mwongozo lililo pembezoni mwake ili kuweka kitu sahihi na kwa njia sahihi.

viii, Sanduku la jamii kwa njia ya mtandao linapaswa kuwa katika mfumo wa e-mail au website [ mfano www.sanduku la jamii.co.tz ]. Kupokea changamoto, kero, matatizo na mapendekezo ya wananchi kwa njia ya mtandao.

ix, Sanduku la jamii kwa njia ya mtandao lita husisha pia uwekaji wa picha au video kama kuta kuwa na ulazima wa kufanya hivyo kutokana na aina ya changamoto, kero au tatizo husika.

x, Taarifa za mtoa malalamiko ndani ya sanduku la jamii kwa njia ya mtandao, zinapaswa kulindwa ili kuepusha jamii kujenga hofu na kushindwa kutoa malalamiko na kero zao kwa kuhofia taarifa zao kuvuja.

xi, Waandishi ambao ni wananchi wanapaswa kutumia vizuri sanduku la jamii kwa njia ya mtandao kwa uandishi utakao jikita moja kwa moja kwenye changamoto, kero, matatizo na mapendekezo na sio uandishi usio na tija kwa kuandika mambo yasiyo faa mfano habari za kutunga, lugha chafu , chuki n.k

FAIDA ZA UWEPO WA SANDUKU LA JAMII
- Sanduku la jamii litakuwa ni chanzo mojawapo cha kuchochea na kusababisha uwepo wa maendeleo katika jamii husika iwe katika ngazi ya kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa na nchi kwa ujumla hii ni kupitia kero, matatizo, changamoto na mapendekezo mbalimbali yatakayo kuwa yana tolewa katika sanduku la jamii na kufanyiwa utatuzi.

- Utatuzi wa kero za wananchi ndani ya jamii utafanyika kwa haraka zaidi hii ni kutokana na wananchi kupata sehemu yao ya haraka zaidi ya kuelezea kero zao kupitia sanduku la jamii na kero za wananchi kuwafikia viongozi kwa haraka na kufanyiwa utatuzi.

- Sanduku la jamii litakuwa ni kisemeo kilicho huru na salama kwa wananchi kwa kuwa taarifa binafsi za mtoa kero na malalamiko hazita kuwa wazi hivyo hakuta kuwa na migongano binafsi ya wananchi na viongozi hivyo kujenga hari ya wananchi kuwa huru na kujiamini kuandika shida, matatizo na kero zao.

- Sanduku la jamii litawaweka karibu zaidi viongozi na jamii wanayo itumikia hii ni kutokana na utatuzi mbalimbali watakao kuwa wanaufanya kutokana na kero, changamoto na malalamiko ya wananchi kuwafikia kwa haraka zaidi tofauti na awali.

- Sanduku la jamii lita chochea utendaji kazi uliobora kwa viongozi ndani ya serikali kutokana na upokeaji wa kero mbalimbali za wananchi kupitia sanduku la jamii zenye kuhitaji utatuzi kitu kitakacho wafanya viongozi kuchakalika muda wote ni kwa namna gani na ni kwa mbinu gani wataweza kutatua changamoto za wananchi.

- Sanduku la jamii litaondoa utegemezi wa rais kutatua changamoto na kero zote katika taifa na hivyo kuleta mgawanyo ulio bora zaidi wa utatuzi wa shida, kero, matatizo na changamoto mbalimbali zitakazo kuwa zina tatuliwa katika taifa kwa kuanzia ngazi ya chini zaidi ya nchi na viongozi wake mpaka ngazi ya juu.

- Sanduku la jamii litasaidi zaidi serikali kupambana na kila aina ya uovu utakao kuwa unajitokeza na kuikumba jamii mfano shughuli haramu zitakazo fanyika ndani ya jamii zitaweza kupata mwarobaini wake. shughuli kama vile uuzaji wa madawa ya kulevya, uingizaji wa bidhaa kwa njia ya magendo pia serikali itaweza kupambana na rushwa kwa njia iliyo rahisishwa kutokana na malalamiko ya utoaji rushwa yatakayo kuwa yana andikwa na kuwekwa katika sanduku la jamii mfano rushwa ndani ya ofisi, rushwa ndani ya maeneo ya hospitali n.k

- Sanduku la jamii ndio njia pekee na iliyo bora iliyobaki katika karne hii ya ishirini na moja [ 21 ] itakayo wafanya wananchi kuweza kuzungumza na serikali walio ichagua Kupitia utoaji wa kero, changamoto, matatizo na mapendekezo yao yaliyo ndani ya jamii zao na kuweza kusikilizwa na kutatuliwa kwa haraka zaidi tofauti na njia ya hapo awali kutumia vikao vya serikali ya eneo husika na wananchi wa hilo eneo. jambo ambalo kwa sasa linakuwa gumu kufanikiwa kutokana na majukumu ya kutafuta kipato kuongezeka baina ya watu ndani ya jamii yanayo wanyima muda wa vikao vya mara kwa mara.
 
Upvote 0
Vipo na vitazid kuwepo but hakuna something positive kitabadilika au vitaleta social changes kwa jamii
 
Vipo na vitazid kuwepo but hakuna something positive kitabadilika au vitaleta social changes kwa jamii
1. Vipo katika maeneo gani katika jamii zetu mbona hatuvioni zaidi ni vikao vya kijamii ndio hutumika kwa Sana Kama njia za uongozi ndani ya jamii kuwasiliana na wananchi wake ili kujua kero, changamoto na matatizo yanayo zikabili jamii ?

2. Kwa nini unasema havija leta matokeo chanya ? Wakati kwenye jamii havijawekwa hili kupima matokeo yake ?
 
Sorry naomba dimension za ivo vitu katika jamii labda sijaelewa
Visanduku vya jamii hivi visanduku ambavyo vitakuwa vinawekwa katika jamii kwa kazi maalumu ya kukusanya kero, changamoto na matatizo yanayo zikabili jamii mfano katika ngazi ya kata kila mtaa utapaswa kuwa kisanduku chake cha jamii kilicho eneo la wazi la mtaa husika ambalo mwananchi wa mtaa huo ataruhusiwa kuweka mapendekezo yake kuhusu mtaa wake na hata kata yake pia ataweka matatizo anayo kumbana nayo kwenye mtaa na kata yake, kero, changamoto n.k na uongozi wa mtaa na kata utakuwa na jukumu la kuyatoa mapendekezo, kero, changamoto zilizo wekwa na wananchi katika masanduku hayo na kuzitatua.

- Sanduku la jamii kwa njia ya mtandao lenyewe litakuwa na jukumu mfanano na sanduku la jamii kwa njia ya mtaa kupokea [ changamoto, kero, matatizo na mapendekezo ] utofauti wake utakuwa hili sanduku la jamii kwa njia ya mtandao litakuwa kwa mfumo wa website { mfano www.sanduku la jamii.co.tz } na kwa mfumo wa e-mail wakati sanduku la jamii kwa njia ya mtaa likiwa katika mfumo wa kisanduku cha chuma kigumu . rejea picha ya namna sanduku la jamii linavyo paswa kuwa niliyo weka kwenye maelezo ya mwanzo kuhusu sanduku la jamii.
 
Picha sio ni msingi but function ya ivo visanduku ni msingi muhimu zaidi but unajaribu kutofautisha but purpose ni moja its better to think unthinkable things
 
Jaribu kutembea katika ofisi ya kijiji chako au mtaa utaona
Sanduku la jamii ninalo zungumzia mimi halipaswi kuwa katika Ofisi ya kijiji bali kwa kuwa halito kidhi mahitaji ya kijiji kizima bali yanapaswa kuwepo masanduku mengi ya jamii kulingana na ukubwa wa eneo husika mfano Ukubwa wa Kijiji utaamua masanduku mangapi yana paswa kuwepo na yanapaswa kuwekwa sehemu itakayo mpa Uhuru mwananchi kuweka mapendekezo,kero, changamoto kwa Uhuru zaidi na usalama wake tofauti na kuwa katika Ofisi ya kijiji kwanza haitakidhi mahitaji ya jamii nzima pia haita mpa Uhuru mwananchi kuweka maoni yake na kingine ni rahisi zaidi kuleta migogoro baina ya wananchi na viongozi wake kwa kuwa taarifa za aliweka changamoto na kero zake ndani ya kisanduku cha jamii zitakuwa wazi zaidi kitu kitakacho weka urahisi zaidi wa kutokea migongano baina ya viongozi na wananchi wao.
 
Picha sio ni msingi but function ya ivo visanduku ni msingi muhimu zaidi but unajaribu kutofautisha but purpose ni moja its better to think unthinkable things
Una maoni gani juu ya sanduku la jamii kwa njia ya mtandao ?
 
Sanduku la jamii ninalo zungumzia mimi halipaswi kuwa katika Ofisi ya kijiji bali kwa kuwa halito kidhi mahitaji ya kijiji kizima bali yanapaswa kuwepo masanduku mengi ya jamii kulingana na ukubwa wa eneo husika mfano Ukubwa wa Kijiji utaamua masanduku mangapi yana paswa kuwepo na yanapaswa kuwekwa sehemu itakayo mpa Uhuru mwananchi kuweka mapendekezo,kero, changamoto kwa Uhuru zaidi na usalama wake tofauti na kuwa katika Ofisi ya kijiji kwanza haitakidhi mahitaji ya jamii nzima pia haita mpa Uhuru mwananchi kuweka maoni yake na kingine ni rahisi zaidi kuleta migogoro baina ya wananchi na viongozi wake kwa kuwa taarifa za aliweka changamoto na kero zake ndani ya kisanduku cha jamii zitakuwa wazi zaidi kitu kitakacho weka urahisi zaidi wa kutokea migongano baina ya viongozi na wananchi wao.
Sawah na nani anayapkea ayo maoni kuyapeleka katika srhemu husika?
 
Sawah na nani anayapkea ayo maoni kuyapeleka katika srhemu husika?
Uongozi wa eneo husika utakuwa na jukumu la kufungua na kutoa yale yaliyo ndani ya sanduku la jamii na wao ndio wenye jukumu la kutatua changamoto, kero watakazo kutana nazo.
 
Maoni yangu katika hilo lipo Sawah but lilimit some condition maana watanzania ukiwapa freedom of expression pia ni harmful
Ndio maana nimependekeza kuwa sanduku la jamii litakuwa na karatasi mwongozo pembezoni mwake ili kumwongoza mwekaji kero, changamoto, matatizo na mapendekezo ajue nini kinachopaswa kuwekwa na ni njia gani sanduku la jamii linavyo fanya kazi.
 
Uongozi wa eneo husika utakuwa na jukumu la kufungua na kutoa yale yaliyo ndani ya sanduku la jamii na wao ndio wenye jukumu la kutatua changamoto, kero watakazo kutana nazo.
Perfect aya mfano kama ulivyosema kutatua migogoro kati ya viongoz na wananch mfano mwenyekit na wananchi unadhani mwenyekit akisoma hayo malalamiko atayapeleka katika srhemu uhusika?
 
Ndio maana nimependekeza kuwa sanduku la jamii litakuwa na karatasi mwongozo pembezoni mwake ili kumwongoza mwekaji kero, changamoto, matatizo na mapendekezo ajue nini kinachopaswa kuwekwa na ni njia gani sanduku la jamii linavyo fanya kazi.
Defence mechanisms but all in all congratulations
 
Back
Top Bottom