Katika pita pita zangu kwenye ofisi za umma nimejifunza Haya!
Ukipeleka maoni yako au kero yako kwa unaeamini ni boss (In charge) wa ofisi ndiyo kwanza unaiongezea ugumu huduma unayotafta
Ukiandika maoni yako na kuyaposti kwenye kisanduku cha maoni (suggestion box), Unaemlalamikia ndiye mwenye funguo wa hicho kibox
Ukilalamika kwa boss kwamba mfanyakazi (A) kakuomba rushwa! Wataonesha kukusikiliza kwa makini kama wameguswa, lakini ukitega mgongo wanang'ong'a nakuambizana "yule mteja bwege kweli yaani anataka mambo kirahisi rahisi" Achana nae!