Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. SANTIEL KIRUMBA ACHANGIA BAJETI YA TAMISEMI SEKTA YA ELIMU
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Eric Kirumba ameunga mkono hoja ya kupitisha bajeti ya Wizara ya TAMISEMI ambapo amechangia hasa upande wa Elimu kwa watoto kupewa chakula mashuleni.
Mwaka 2021 Bunge lilipitisha mpango wa kitaifa kuhusu kutoa chakula mashuleni kupitia Wizara ya TAMISEMI.
Mkoa wa Shinyanga Mpango wa kutoa chakula umetekelezeka kwa Shule 205 na kati ya Shule 609 zilizopo Mkoa wa Shinyanga ni Shule 290 tu zinazotoa chakula cha mchana
Kukosa chakula mashuleni kunapelekea watoto kuwa watoro mashuleni, wadumavu kiafya na kurudi nyuma kielimu. Shule nyingi hazifanyi vizuri kutokana kwamba watoto hawapati chakula shuleni
Mtoto mdogo wa miaka saba mpaka kumi na nne anaenda shuleni anakaa saa moja asubuhi mpaka saa tisa mchana bila chakula, kwa namna yoyote Mtoto hawezi kufanya vizuri kwenye masomo
Mhe. Santiel Kirumba ameishauri Serikali kuwa vipindi vya masomo mashuleni vianze saa tatu asubuhi
Pia, Mhe. Santiel ameshauri Serikali itumie wadau wa elimu kama PCI waweze kusaidia kutoa chakula mashuleni ili kupunguza utoro, kuongeza ufaulu wa watoto na kupunguza Udumavu wa Afya.