Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,210
Wapenda michezo JF naomba msome makala hii fupi niliyoinukuu toka kwenye tovuti ya gazeti la Mwananchi.
Kwa ufupi nimesikitishwa na ufafanuzi finyu wa Sappi ambaye anaangalia udhaifu wa kocha bila kuangalia udhaifu wa muundo mzima wa FA ulioifanya Tanzania iwe kichwa cha mwendawazimu na wachezaji kuwa wa kiwango cha chini kwa muda mrefu.
Huyu mpenda michezo naona amesahau kuwa club ziewahi kuwa na makoca kutoka kwenye maeneo ya hizo nchi lakini wote walishindwa kufaya kazi kutokana na miundo mibovu ya klabu, ambayo inafanana kabisa na ya FAT. Maximo amejitahidi kufika hapo alipo leo anaonekana hana uwezo, sijui ana suggest nini?
Sijui kama anafahamu kuwa mafanikio ya timu hayatokani na kocha peke yake, tunaweza kumchukua hata Maurinho lakini bado tutakuwa hovyo.

Maximo adaiwa hana uwezo zaidi ya hatua aliyoifikisha Taifa Stars
MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Hussein Sappi amesema tukubali ukomo wa kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo na staili ya soka anayofundisha timu haiwezi kufika mbali.
Akizungumza katika kipindi cha Kumepambuzuka cha Radio One jana, Sapi alisema makocha wa Brazil wengi hawana rekodi katika ulimwengu wa soka zaidi ya nchi yao.
Alisema Brazil wazuri kwa wao wenyewe lakini hawana rekodi nzuri duniani.
"Mimi nadhani wakati umefika sasa tubadilike, tuangalie Ulaya Mashariki, kule tunaweza kupata makocha wazuri na hata soka yao inajulikana.
"Tunakubali kuwa Brazil wana makocha wazuri lakini kwa faida yao, wapi kuna mafanikio kwa kocha wa Brazil? Tunaona Afrika Kusini inavyoyumba.
"Kulikuwa na Felipe Scolari, alikuwa Ureno, hakuna kitu, kaondoka akaenda Afrika Kusini, akatoka akaja Chelsea, na sasa hayupo, kuna nini pale. Angalia makocha wa Hispania, Ufaransa, Uholanzi, Russia, Jamhuri ya Czech wapo na naamini tunawamudu...," alisema.
Akizungumza huku akionyesha kukerwa, alisema: "Isije kufika wakati tukapigana mawe Uwanja wa Taifa pale, mimi hili nalisema kama Mtanzania mwenye haki ya kuzungumza langu na sidhani kama Maximo anatufaa tena," alisema.
Chanzo: Mwananchi