SoC02 Sarafu ya Kuzimu

SoC02 Sarafu ya Kuzimu

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 27, 2022
Posts
8
Reaction score
4
Ndugu msomaji wa stories for change nakuandikia uzi huu wa kusisimua unaomuhusu Majuto kama kijana aliyepitia changamoto ya kiuchumi wakati wa mahusiano yake na mpenzi wake aitwae Chawote katika kila tukio ikionekana kuna jambo la kujifunza kama kijana;

Shuka nao....

Kipenzi changu chawote,
Natumaini u mzima wa afya. Mimi pia sijambo na ninaendelea vizuri.Nimekukumbuka sana mpenzi. Macho, umbo na rangi yako ya kiafrika bado vinanifanya nisisimke na kujiona Mwanaume niliekamilika. Kila nifungapo kope zangu naliona tabasamu ya midomo yako miembamba na nyekundu. Bado naziona siku tulizotembea nikiishika mikono yako laini na yenye kutereza. Baridi la njombe linanifanya nizikumbuke siku nilizokukumbata gubigubi.

Barafu wa moyo wangu, umenifanya niwe mbali nawe.Umefanya ndugu, jamaa na rafiki waamini mimi ni mtu mbaya. Lbda ni kweli sistahili kuandika wala kutafakari kuhusu wewe. Ila bado najiuliza nimlaumu nani? Je nijilaumu mimi? wazazi? Elimu? Serikali? Au nikulaumu wewe Malikia?

Mpenzi chawote, nazikumbuka siku tulizocheza na kuruka pamoja. Siku tulizocheza kombolela na kupeana vidali poo wakati giza lilipotanda huku tukisubiri mawio ya jua ili tucheze tena na tena. Kukua pamoja na wewe ilikua ni furaha isiyo kifani. Nakumbuka bubujiko la machozi siku niliyokuaga naenda masomoni.

Nazikumbuka na zile ahadi nikimaliza chuo tungekua na maisha mazuri, nyumba, mavazi na magari ya kifahari. Sio kwamba nilikudanganya lahasha ni kweli kutoka moyoni nilipanga kukufanya uwe mwanamke mwenye kuishi kama Malikia. Zile nywele, viatu na nguo ulizotaka zote nilipanga kukutimizia.

Siku zote za kusoma kwangu chuoni IFM nilijiona kama muhasibu na mtu niliekua na kiti changu benki kikinisubiri. Vilee vihela hela ulivyokua ukiona nakuhongaa wakati nipo chuoni vilikua vya bodi ya mkopo. Na masalia yake ndio ilikua mahari yako mke wangu baada ya kumaliza chuo.

Zile siku nilizokuaga naenda kazini nilizitumia kuzunguka kuomba kazi. Ama kweli kisicho ridhiki akiliwi wengine waliniomba pesa na wapo walioniomba ngono ili waniajili. Vitu ambavyo sikuweza kuvimudu. Na ndio maana niliamua kufunguka kwako mpenzi.

Sikuwahi kudhani kama ulimi wako ungekua kisu cha moyo wangu. Nilivumilia sana maneno ya kejeli na masimango uliyonipatia wakati nikitoka kutafuta na kurudi mikono mitupu. Ni mara kadhaa nilifunga midomo yangu nisijibu lolote nakuishia kusugua meno ndani kwa ndani ili kusitiri hasira zangu.

Nyumba yetu niliyoiona kua pepo ya amani ya moyo sasa iligeuka kaa la kuukaanga moyo wangu. Moyoni nilijiuliza sana ivi ni wewe niliekuita rafiki wa dhati wa moyo wangu!. Nilijikongoja na kukopa hapa na pale na kuanzisha ule mtaji wangu wa kuuza karanga kwenye soko la kariakoo.

Nalikumbuka lile tabasamu lako ulilonionyesha siku niliokuletea kile kipisi cha kanga. Ama kwa hakika ulinifanya kidogo niufurahie unyumba tuliokua tumeupoteza ndani ya ile miezi mitatu ya nyuma.

Naikumbuka tarehe 14/6 nilipata pigo kubwa baada ya kusikia mazao yote niliokua natarajia kuuza yameungua na moto ndani ya soko la kariakoo.Kweli sikua na chochote mfukoni mke wangu kwani siku tatu kabla ya janga hili nilimtumia mama hela ya kwenda hospitali kumuuguza baba.

Ila hukujali nipone madonda ya kutolipwa fidia ya mazao yangu yaliyoungua kabla ya kunipa pigo la kutembea na rafiki angu wa karibu Sam. Labda ni kweli nilistahili hili ila sio kwa wakati huu. Labda ningekuuliza zile nyama na tambi ulizokua unapika ulitoa wapi? Au ningekuuliza yale maziwa ya mgando tuliokua tunakunywa ulinunua na nin?. Ila nilishindwa kwani sikua na chochote mfukoni kusitiri tumbo langu. Ni kweli najutia maamuzi yangu kumchoma kisu Sam.

Hukumu yangu imetoka jana na nimeukumiwa kunyongwa kesho saa 6 mchana ila kinachoniumiza zaidi hutaweza kuisoma barua hii bali kuisikia, hutoweza kuniona tena bali kunihisi. Nisamehe kwa kukutenda ivo, mpende sana mwanangu na mwambie baba ake anaipambania SARAFU KUZIMU.
Wako Majuto.

FUNZO
•Amka, Angaza na chomoza! kama kijana shupavu mwenye kuiona changamoto yoyote kama fursa inayoweza kukukwamua kiuchumi. Acha kuidharau kazi au kipato kidogo unachoingiza kwani Haba na Haba hujaza kibaba.

•"Fimbo ya mbali haiui nyoka". Ni ukweli usiopingika kua Mtahara wa Elimu unaotumika kufundishia katika Nchi yetu ya Tanzania umuandaa kijana anaehitaji kuajiriwa kuliko kujiajiri. Ivyo nipende kutoa pendekezo kwa wadau wa Elimu kujikita katika kutoa Elimu ya ujasiriamali ili kuweza kumuandaa kijana kuingia kwenye hili soko la ushindani wa kiuchumi.

•Ongezeko la magonjwa ya akili, ulevi, utumiaji wa madawa ya kulevya na wizi unaambatana sana na ukosefu wa ajira kwa vijana. Hivyo ni jukumu la serikali kuangalia pia kwa jicho la pili ni kwa namna gani wanaweza kutengeneza fursa kwa vijana ili kuwakomboa na uchumi mbovu.

•Kidole kimoja Akivunji chawa! Sote kwa pamoja kama ndugu, Rafiki, Serikali na jamii kwa ujumla ni wakati wa kuondoa minyororo inayofunga fikra zetu juu ya nani wa kulaumiwa bali tusimame na kutafuta njia nzuri ya kushinda UMASIKINI.

ANGALIZO
Wahusika katika simulizi hii ni wa kubuni.
 
Upvote 7

Hongera Sanàaa👍🔥🔥HAKIKA NIMEJIFUNZA KITU
 
Back
Top Bottom