Sarafu ya Tanzania (TZS) yazidi kuporomoka dhidi ya Dollar (USD)

Mr. JF

Member
Joined
Dec 14, 2015
Posts
79
Reaction score
107


Power to the People Wanajamvi!!!
Kama umekuwa ukifuatilia mwenendo wa SARAFU yetu pendwa ya TZS kuanzia mwezi wa 5, utagundua kwamba imeporomoka sana kwenye soko la ubadilishaji wa fedha za kigeni.

Kiwango ambacho TZS imeporomoka sasa hivi, hakijawahi kufikiwa tangu uwepo wa TZS duniani, yaani ipo kwenye ukanda wa A.T.H (All the Time High), na wala hakuna anayelizungumzia hili, wala tamko lolote sio waziri sio gavana.

Cha ajabu ukicheck rates za exchange, zilizopo kwenye website ya BOT, utakuta rates za chini kabisa, ila sasa, nenda kafanye transaction ya Dollar Online, au kabadilishe kwenye Bureau De Change, ndio utaona shughuli yake!
 
Ila BOT Wao wanakwambia ni 2336
 
Nimeshangaa pia shilingi ya Kenya kuporomoka kutoka around 90 hadi zaidi ya 140 per USD.
 

Juzi nimetuma hela Kenya nikashangaa sana shilingi moja ya Kenya iko around 17 Tanzanian shilings na USD moja ilikuwa kama 138 Kenyan shillings.
 
Hivi sababu zipi hupelekea kiwango cha pesa ya nchi fulani kushuka
 
Nimeshangaa pia shilingi ya Kenya kuporomoka kutoka around 90 hadi zaidi ya 140 per USD.
Kuna uhaba sana wa USD. Uhaba huu unapandisha thamani ya dola.

Ujinga ni kwamba, hata tunapofanya intra-African trade kuuziana vitu wenyewe Africa, bado tunatumia US dollars, kitu kinachoizidishia US dollar thamani unnecessarily.

Ndiyo maana Rais William Ruto wa Kenya anataka nchi za Kiafrika ziache kutumia US dollar katika kufanya biashara baina yao.

 
Juzi kati nilichekelea sana nilipokuwa Zanzibari ile naingia bureau de change nampa 100 ananipa 242kl daa nilitoka nje kuangalia ubao nikihisi kanizidishia kumbe tayari issue ya bandari ni effectively hadi sasa πŸ˜‚!.
 
Hili linadhoofisha sana sarafu za Africa. Lakini pia nchi za Africa zinatumia kama njia ya kupata dola za kununulia bidhaa mfano Petroleum Products, magari na mitambo bila kusahau makoti suti kutoka ughaibuni.
 
Hebu tupeni somo mnaojua mambo ya Fedha,.....ina maana kama nina vidola vyangu uvunguni nikivitoa leo vitakuwa vina nguvu kuliko mwaka jana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…