KERO Saranga na Mpakani kwa Mpapula Dar es Salaam hakuna maji kabisa zaidi ya mwaka, maisha ni magumu sana

KERO Saranga na Mpakani kwa Mpapula Dar es Salaam hakuna maji kabisa zaidi ya mwaka, maisha ni magumu sana

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
,🥲🥲

Mimi ninaishi kata ya Saranga, kwa Mpapula jijini Dar es Salaam. Jamani huku tunahangaika maji hakuna, hatujaona maji mwaka umeisha sasa, mabomba hayatoi maji tunaishi kwa taabu sana , Kuna muda mpaka unahisi labda tupo jangwani

Kwa Mpapula na Saranga mpakani kote maji hakuna kabisa hayatoki, ambacho huwa tunafanya kuna watu wanatuuzia maji kwenye magari, yaani inabidi tuagizie kwenye magari ndio watuletee, Lita 1,000 tunanunua kwa shilingi 20,000

Tumeshapiga kelele sana kwenye uongozi lakini wapi, pia inaonekana kwamba hao wenye magari ya kuuza maji ndio wale wale viongozi wa huku, wananchi wanachota maji ya mitaroni sasa kwenye vyoo, hali ni mbaya kiukweli tunahitaji msaada sana tunakufa na kiu.

saranga.jpg
saranga 2.jpg
 
Bora ninyi hayajatoka mwa mmoja tu.Sisi Huku mbezi msakuzi hatujawahi kuya ona maji ya dawasa Toka tupate uhuru.serikali ya mama chura inachojua ni kutoa zawadi ya milioni kumi Kwa Kila goli lakini mambo ya muhimu kama ya maji inadai haiwahusu.
 
Kabisa yaani , ni mambo ya ajabu sana .
 
Back
Top Bottom