Wile kadogosa
New Member
- Jul 30, 2022
- 1
- 1
Saratani ya mlango wa kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au seli zilizoko katika shingo ya kizazi.
Mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile.
Asilimia 99 ya saratani ya shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya Human Papilloma Virus au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma.Baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja huambukizwa kwa njia ya kujaamiana.
Saratani ya mlango wa kizazi yasemekana kuwa saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake katika nchi zinazoendelea.
Inakadiriwa asilimia 85 ya Vifo kutokana na saratani ya mlango wa kizazi hutokea katika nchi zinazoendelea.
Kwa Tanzania wastani wa wanawake 6241 huugua saratani hiyo kila mwaka na 4355 kati yao hufa hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la afya duniani (WHO)
Kwa takwimu hizi inadhihirisha kuwa tatizo hili ni kubwa nchini hivyo tunapaswa kulivulia njuga kwani wanawake wote wapo hatarini kuugua ugonjwa huu.
Mambo yanayoongezea hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi ni pamoja na kushiriki tendo la ndoa katika umri mdogo.Kuwa na wapenzi tofauti tofauti au mwenzi alie na wapenzi tofauti.Utumiaji wa sigara pia husababisha hatari ya kupata saratani hii hivyo wanawake hushauriwa kula mlo kamili.Kuwa na uzazi wa mara kwa mara na pia watu wenye kinga hafifu wapo kwenye uwezekano mkubwa wa kuugua saratani hii ya mlango wa kizazi.
Dalili kubwa mbili zinazoashiria saratani ya mlango wa kizazi ni kutokwa na majimaji au uchafu wenye harufu kali ukeni.Pia kutokwa na damu ukeni mbali na siku za mwezi au baada ya tendo la ndoa.
Dalili zingine ni pamoja na maumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo.Kuhusi maumivu wakati wa kujamiiiana,kupungua uzito wa mwili bila kukusudia,mkojo wenye matone ya damu pamoja na kuumwa mgongo na kiuno.
Saratani ya shingo ya kizazi hugunduliwa kwa vipimo vya uchunguzi vinavyofanyika ni pamoja na,
Papsmear;hiki ni kipimo rahisi na hakina madhara yoyote.Inashsuriwa kufanya kipimo hiki mara moja kwa mwaka.
kipimo kingine ni colposcopy hiki ni kipimo kinachotumia darubini kuangalia seli zilizo ndani ya ngozi inayozunguka shingo ya kizazi.
Matibabu ya saratani hutolewa kulingana na hatua ya ugonjwa.Ugonjwa ukiwa katika hatua za mwanzo huweza kutibika kabisa ingawa kuna uwezekano wa kujirudia tena.
Hatua za mwisho za ugonjwa huu haziwezi kutibika kabisa.Kinachofanyika mara nyingi ni kutoa matibabu yanatotuliza dalili na maumivu na kumwezesha mgonjwa kuishi vizuri.
Huduma za matibabu hutolewa kwa njia ya upasuaji,mionzi,dawa za saratani na mionzi pamoja na dawa za saratani.
Madhara ya saratani hii ni pamoja na Figo kushindwa kufanya kazi,fistula pamoja na kutokwa na damu kwenye uke.
Saratani hii ya mlango wa kizazi hukaa mda mrefu hadi kuja kuonyesha dalili zake.Na dalili za awali zimekuwa zikipuuzwa na wanawake wengi kwani hufanana na dalili za magonjwa ya kawaida ya maambukizi kwenye uke
Saratani hii inaweza kuzuiliwa kwa njia ya chanjo ya HPV ambayo huchomwa kwa mabinti wenye umri chini ya miaka 14 hii itawafanya kujikinga dhidi ya kirusi cha HPV ambayo ni moja ya chanzo cha saratani ya mlango wa kizazi.
Kipindi cha nyuma saratani ya kizazi ilikuwa inaonekana kwa wanawaje wenye umri wa miaka 60 na kuendelea lakini miaka ya karibuni imekuwa ikionekana hata kwa mabinti wenye umri wa miaka 28.
Hivyo kuna haja ya kutoa elimu kwa watoto wa kike kujitunza na kutoanza ngono mapema wakiwa na umri mdogo.Hii hutokea sana vijijini kwani kuna watoto wanaolewa wakiwa na umri mdogo na kuanza ngono mapema hivyo kuwaweka kwenye hatari ya kupata saratani.
Pia kinachopaswa kufanyika ni kuongeza uelewa kwa jamii ambayo itaona mtaji wao wa maisha upo katika afya hivyo kujenga tabia ya kupima mara kwa mara.
Mimi kama mwandishi wa makala hii kutokana na elimu niliyonayo katika sekta ya afya ninajitolea kutoa elimu kwa wanafunzi wa kike walio katika shule za msingi na sekondari kwani hao ni waathirika wakubwa wa saratani ya mlango wa kizazi ambayo huja kujitokeza baada ya kipindi kirefu baadae.
Ninaomba mashirika ambayo yanajali na kuthamini afya ya binti ambaye ni mwanamke wa kesho kuweza kuungana na mimi mkono kwa ajili ya kusaidia kufikisha uelewa kwa mabinti juu ya hii saratani ambayo wanaweza wasione madhara yake sasa hivi ila kuja kuyaona madhara yake baadae.Pia kuweza kuwahimiza mabinti juu ya kufanya vipimo chunguzi dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kwani inapogundulika mapema ni rahisi kutibika na kuweza kupona.
Video hiyo juu inaelezea kwa ufupi kuhusu saratani ya mlango wa kizazi na imetolewa kutoka shirika la habari la DW.

Upvote
1