Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa jana alikuwepo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijiji Dar es Salam wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa Madereva bodaboda na Bajaji wa Jiji la Dar es salaam.
Sare hizi zina picha ya Rais Samia kama zinavyooneka hapo, lakini pia Mchengerwa alitoa maagizo kwa madereva wa bodaboda kuacha kusumbuliwa kwakuwa wanashiriki vizuri kwenye shughuli za ujenzi wa taifa.
“Kuanzia sasa sitaki kusikia kamata kamata ya hovyo, inayotokana na wakati fulani kuwepo na sintofahamu baina yenu na Maafisa wa Serikali, mchango wenu ni mkubwa sana hivyo Serikali ya Chama cha Mapinduzi inawathamini sana ninyi Maafisa usafirishaji wa bodaboda na bajaji, na ndio maana ninataka kuona ushirikiano mzuri unakuwepo baina yenu na Serikali"
Wakuu tunajua bodaboda ndio wanaongoza kwa uvunjifu wa sheria barabarani, na wengi hawana leseni, mtu anajifunzia zake mtaani siku mbili tatu huyo mtaani, kwa agizo hili hatuoni kama ni uvunjifu wa sheria utazidi kuongezeka?
Kwanini sare hizo zimewekwa picha ya Rais? Ukijumlisha na agizo la Mchengerwa si ni kampeni hiyo kabisa ya waziwazi, kila kitu mama atenda, tuanze kuuliza kama yule Mchungaji alivyosema, kama vyote amefanya Rais, nyie Wabunge na Mawaziri mnafanya kazi gani?
====
Pia soma: Mchengerwa: Wakuu wa Mikoa wote simamieni mfumo wa Kidijitali wa kuwatambua Madereva Bodaboda na Bajaji
#KataaMachawa
#KataaUozo2025