Sare za Shule, Kwa nini?

Sare ni muhimu sana! Sare inawafanya wazazi wafikirie kuzaa kwa mpango ili kupunguza gharama za sare. Maisha yakirahisihwa, bila ya sare, kuna uwezekano mkubwa watoto wakazaliwa wengi sana. Hususani kama gharama za kuendesha shule (michango) haitokuwepo kabisa.
Kuzaa watoto wengi ndiko kunakopelekea, kwa kiasi kikubwa, wazazi hususani wa vijijini, kushindwa kumudu gharama za sare.
Nasema hivyo kwa kuwa sare, kama mashati na sketi/kapptula, hazinunukiwi kila mwaka. Kwa mzazi mwenye watoto wengi ni lazima kila mwaka aende sokoni kununua sare. Hamasisha uzazi wa mpango.
Kwa kutotilia mkazo sare, kunaweza kuibuka hoja ya kutoruhusu viatu, kuoga/kufua, ....
Sare ni muhimu! Sare zinasaidia kuhakikisha usafi wa wanafunzi, utambuzi, usawa (zinaficha hali za wazazi wa wanafunzi), ...
Ukiona Elimu ni ghali jaribu ujinga.
 
mtoa mada ungekua umesoma kitu inaitwa saikolojia ya elimu wala usingeleta huu upuuzi wako huku
 
Yaan nyie ni kati ya watu wanaopelekea watu kupewa ban,hvi wewe kama mtoto anakosa sare,je gharama chache za kuchangia pamoja na serikal ili kuendesha shule ataziwezea wap?duh nina mashaka na uwepo wako jf,umekuta akaunt ya mtu ukapost huu utumbo,!?
 
Tukiruhusu vazi lolote,tutaleta utabaka shuleni,pia maadili ya uanafunzi yatashuka,labda itumike mbinu mbadala ya kuwatambua wenye changamoto hizo na kuwapa msaada,Asante.
 

mzazi kuwa na mtoto usiyeweza kumhudumia ni dhambi, kama za sare huna unamlisha nini ili naye ajione ana wazazi? Tuache kasumba ya kusingizia umaskini, hata Tanzania ni maskini pia.
 
Sare za shule huwa ni utambulisho wa mwanafunzi popote pale alipo hii humtofautisha yeye na jamii(Kumfanya awe special)kama ilivyo kwa askari
 
Unajua wewe ni sawa sawa na yule anayesema watu wote wasiokuwa na kazi ni Wazembe, ni kwa nini hawatafuti kazi, mimi mbona mimi nina kazi? Ndio Tafsiri ya maneno yako... wewe haujatembea Hii nchi ndio maana unaongea hivyo!


Maana yangu sio unavyoiweka wewe, kama mzazi una majukumu yako na huwezi kutegemea kusaidiwa kwa mambo yote. Jukumu la kumpeleka mwanao shuleni kwanza sehemu kubwa ushasaidiwa na serikali, hata sare nazo unataka kubewa, si mwisho wa siku utaomba na chakula wakuletee nyumani mbona jukumu la kuwtafuta hao watoto nalo usitake msaada, naweza kuondoa neno uzembe lakini mahala pake, mzazi lazima awajibike kuhakikisha mchango wake kwa elimu ya mwanae upo na sio kuzaa na kusingizia mengine.
 

Kazi na jukumu la Serikali ktk Nchi yoyote ile Dunia hii ni kuweka Mazingira rafiki ambayo Mtu anaweza kujikomboa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba kila Mtoto anapata Elimu, na kusiwe na sababu yoyote ile inayoweza kuzuia Mtoto asipate Elimu ikiwa ni pamoja na Mtoto kukosa Sare!

Kama unaona shilingi 15 000 ni ndogo kwa Mtanzania wa kawaida na anayeishi kijijini, fikiria hili, zaidi ya nusu ya Watz wanaishi kwa chini ya Dola Moja ya Kimarekani kwa siku yaani senti 0.68 kutokana na Takwimu za Umoja wa Mataifa na Serikali yetu imezikubali ambayo ni sawa na shilingi 367 200 (laki tatu) kwa mwaka (sio kwa mwezi) na hiyo namba ni kujumisha wakazi wa Majiji kama Dar, Mwanza, Arusha n.k achilia vijijini ambako ndiko zaidi ya 70% yetu wanaishi, sasa kama unajua Hisabati utaona kwamba ktk Kipato kama hicho kwenda kumwambia Mtu lazima atoe shilingi 15 000 ya kununua sare na Viatu labda inakuja 20 000 ataweza?

Kumbuka huyu Mtu ana watoto wanahitaji kula, yaani kununua mafuta ya kupikia, saa nyingine Maji ya kunywa kununua kisimani, anahitaji kununua aspirini akiumwa aidha yeye ama Mtoto (na nimetumia Mtoto Umoja na sio Wingi), anahitaji kununua Daftari, penseli na Kalamu, kifutio, sijaongelea seti na rula, anahitaji kununua yoote hayo, anapaswa kulipa kwa kutumia hiyo shilingi laki tatu anayopata kwa MWAKA Sio Mwezi sasa huoni kwamba hakuna pesa itabaki ya kununua Sare za Shule?

Ni kwa nini Serikali isiseme Mtoto aende Shule vyovyote vile ili mradi aweze kusoma ili mwisho wa siku aweze kujikomboa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…