Sarpong aondolewe kwenye mipango ya kikosi cha kwanza cha Mwl Kaze

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Sina jambo lolote dhidi ya Sarpong.

Ushauri wangu kwa klabu ya Yanga SC ni kwamba huu ni wakati sahihi wa kuhakikisha Sarpong anaondolewa kwenye mipango ya kikosi cha kwanza cha Yanga SC.

Sarpong mpaka muda muu amecheza mechi zaidi ya 11 akiwa na mabao ya ufungaji 4 tu kwenye ligi Kuu Tanzania Bara. Hizi sio takwimu nzuri kwa mshambuliaji wa Kigeni kwenye klabu kubwa kama Yanga. Hizi ni aina ya takwimu ambazo walizokuwa nazo wachezaji kama wakina Matheo Anthony na Balimi Busungu.

Sioni sababu ya kuendelea kumpa nafasi ikiwa takwimu za utendaji kazi wake ziko wazi. Katika nafasi anayo cheza tunatarajia makubwa zaidi ya uwezo wake wa kulinda mpira, uwezo wake wa nguvu zisizo na faida, mikimbio yake isiyoleta tija kwa viungo wachezeshaji.

Hebu Kaze ajaribu kumpa nafasi Fiston. Pia najua kuwa Fiston ni jamii moja ya wachezaji kama ya wakina Sarpong lakini huenda tukapata kuona kitu kutoka kwake endapo akipewa nafasi ya kutosha kama nafasi alizopewa Yacuba Sogne.

Ciao.
 
Tatizo lake kakosa wapishi, jana kuna nafasi yoyote ambayo alipata akaipoteza?
 
Kwa kweli Sarpong ni mtihani mzito! Bora Lamine achezeshwe nafasi ya ushambuliaji badala ya Sarpong! Lamine ana goli za kutosha tu mpaka sasa!
 
Mnaweza kwenda Airport kwa mbwembwe kumbe mnakwenda kupokea magarasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…