sarufi

sajumo

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2013
Posts
1,834
Reaction score
1,055
naomba uwe wa kwanza kujua makosa tunayoyatenda kila siku
asubuhi njema
mchana mwema
usiku mwema
kwa nini neno asubuh tutumie njema mchana na usiku tuseme mwema je ni neno gani sahih kati ya njema na mwema
njema (nje)hapa imesimama kuonesha hali (mchana)
mfano nina afya njema.
mwema(mwe) ni kiambishi kinacho onesha nafsi ya tatu umoja mwema mfano mtoto mwema ni makosa ambayo yamezoeleka mno nami wacha niwaage usiku njema
 

Kwa mawazo yangu nadhani hapo imetumika kanuni ya kuendana kwa maneno yaani ukiona neno "msikiti" unategemea kufuatiwa na "wa ijumaa" hali kadhalika ukiona neno "kanisa" unategemea kuona "la wasabato" aghalabu japo si mara zote kulingana na muktadha.
Asubuhi njema,
Siku njema,
Mchana mwema,
Usiku mwema,
Mafanikio mema.

Nikutakie siku njema na mafanikio mema.

FaizaFoxy pita hapa usaidie.
 
Last edited by a moderator:

Tenda wema "wende" zako au "uende" zako?

Wacha kuhororoja, Kiswahili si lugha mama kwenu.
 
Hapa ngeli za nomino hufanya kazi yake. Kwa mfano kwa kufuata kanuni za ngeli za nomino, utasikika ukisema hivi: asubuhi imekwisha na wala sio asubuhi umekwisha; mchana umekwisha na wala sio mchana imekwisha; usiku umekwisha na wala sio usiku imekwisha.

Kwa hiyo hapa kinachotawala uhusiano wa maneno hayo ni ngeli (nomino) zilizotumika.
 

Ufafanuzi murua kabisa, asante mkuu na nikutakie jioni njema.
 

hiki kigezo cha ngeli za nomino kiliwapa shda weng kipindi kile kwa mfano
kipof anatetembe
kuna walotaka
itamkwe,
kipofu kinantembea.
kama tunavyotamka kisu kinatembea. lazima tutumie maarifa tuliyonayo kufikiri zaid iweje muda utambulishwe na neno njema kasoro mchana na usiku "aliyezoea kukosea hujiona yupo sahih kama hajajua kama anakosea na atadai haki itakayomruhusu aendele kukosea pind atakapoambiwa aache makosa"asubuh njema
jioni njema
adhuhur njema
fajir njema hata mchana pia njema
 
kitu kingne wadau
ni kwanini tunasema
gari moja
magari mawili
magari matatu
magari sita kwa nini isiwe
magari masita.
usahih wake hatuna uwing hapa inatakiwa tuseme gari moja gari mbili gari tatu na kuendelea tujitahd kuongea kiswahili sahih saa moja njema
 
hili jukwaa linahitaji kufikiria kwa makini me linanishinda haki ya nani kiswahili kigum kila siku navikuta vitu vipya huku.
 
Hapo kwenye red, kitaaluma tunaita umilisi wa lugha-hatuwezi kufikiri zaidi ya umilisi wa lugha tulionao, zaidi utakua unajenga hoja ya kitaaluma, na kama unataka kufanya hivyo ni lazima ufanye utafiti na ujenge hoja za kushawishi ili watu waache kusema mchana mwema na waseme mchana njema.
 

ntakujibu wacha nipekue zaid nahs hoja nlizozitoa juu hazijakutosheleza
 
Lakini neno 'wacha; ni la kiswahili kweli?. Mengine ni haya
asubui = asubuhi
alafu = halafu
 
Nisema mawili hapa. Kwanza, tunatakiwa kuangalia watu wanasemaje, na ndipo tutafute ruwaza na kusema watu husema hivi au vile. Ukianza na sheria, kuna hatari ya kuwa na makosa katika sheria au ukapingana sana na watu wanavyosema.
Pili, ngeli zote zinahusu nafsi ya tatu umoja na uwingi. Kwa hivyo hoja yako isiwe ni kwa sababu ni nafsi ya tatu. Hoja yako inatakiwa kuangalia ni ngeli gani. Na ngeli zimeainishwa kwa msingi wa mambo makuu mawili: (a) viambishi awali vya nomino, (b) upatanisho wa kisarufi. Ingawa usiku na mchana ni maneno yanayozungumzia nyakati za siku, ni nomino zilizo katika ngeli tofauti kabisa kwa mujibu wa viunzi hivyo viwili.
 

nimekuelewa ndugu ila hiki kigezo cha upatanisho wa kisarufi naona nacho muda mwingne kinakanganya mfano ngeli ya "li ya" nomino zake unapozitamka katika namba znakataa cjajua tunao kosea ni sisi au lugha yenyewe au ndo usahh wake
mf
gari moja
magari mawil
magar sita na si masita
 
Ngeli zote zina upatanisho wa kisarufi kwa nambari 1-5 (na 8 pengine). Si ajabu. Katika lugha nyingi za Kibantu tarakimu za asili zilikuwa 1-5. Ndiyo maana kuna upatanisho. Nambari kama 6 au 7 zimetoka kwenye lugha nyingine, na upatanisho kwake ni shida.
Upatanisho wa kisarufi ktk Kiswahili uko vizuri kabisa wala haukudanganyi lolote. Kwa hakika kila ukiona lugha ina upatanisho wa kisarufi, una kanuni zake. Ukifungua macho zaidi utaona hauko rahisi. Kuna visheria na masharti, mengine yana nguvu na mengine ni hafifu.

 

nijibu hli ndugu ipi sentesi sahihi hapa?

zimenunuliwa bati elfu moja.
au,
yamenunuliwa mabati elfu moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…