Saruji ya magendo yaipotezea Serikali Sh15 bilioni kwa mwaka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


KWA UFUPI

  • Yadaiwa kuingia kupitia Zanzibar hadi bara ambako inauzwa kwa bei ndogo kuliko inayotengenezwa nchini

Tanga. Serikali kila mwaka inapoteza Sh15 bilioni kutokana na kuingizwa nchini kwa saruji ya magendo ambayo hailipiwi ushuru wala kodi zingine jambo ambalo linachangia upotevu wa mapato, ilifahamika.

Akizungumza wakati wa kukabidhi nyumba ya polisi kwa ajili ya Kituo cha Polisi Makorora, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji Tanzania (TCCL) Erik Westerberg alisema ipo saruji nyingi ya magendo ambazo z inaingizwa nchini kinyemela na kuuzwa kwa bei ya chini kuliko inayozalishwa na viwanda vya ndani.

Alisema saruji hiyo hailipiwi kodi wala ushuru hivyo kuathiri ile ambayo inazalishwa nchini ambayo viwanda vyake vimetoa ajira kwa maelfu ya Watanzania na upande mwingine alisema magendo hayo yanazorotesha uzalishaji wa viwanda vya ndani.

Mkurugenzi huyo alisema asilimia 70 ya saruji hiyo ya magendo inaingia kupitia Zanzibar hali ambayo inaviweka viwanda vya ndani katika wakati mgumu kibiashara na iwapo udhibiti hautafanyika kwa wakati basi ni wazi kuwa vitajiendesha kwa hasara na mwisho wa siku wafanyakazi watajikuta wanapoteza ajira.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constastine Massawe alishukuru kwa msaada huo na kutaka wadau wengine zaidi wajitokeze na kuiga mfano huo wa TCCL wa kuwasaidia polisi hilo ili liweze kutekeleza ipasavyo majukumu yao ikiwa ni pamoja na kudhibiti uhalifu.

Wakati huo huo Salum Maige anaripoti kutoka Geita kuwa Kampuni ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ya Buziba Gold Mining (BGM) inayoendesha shughuli zake katika Kijiji cha Buziba, Kata ya Lwamgasa wilayani Geita, inakusudia kutumia zaidi ya Sh360 milioni katika huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha polisi na nyumba tano za kuishi askari zaidi ya 10.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Mapinda Manjuga alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika mgodi huo unaokadiriwa kuwa na zaidi ya watu 10,000 wanaoishi katika eneo hilo kwa kutegemea shughuli za uchimbaji na biashara ndogondogo.

katika hatua ya kwanza ya mpango kazi wa utekelezaji wa miradi hiyo, tayari ujenzi wa kituo cha polisi umeanza na mara baada ya kukamilisha ujenzi huo nyumba tano za kuishi askari zitajengwa kwa gharama ya Sh 165 milioni.Saruji ya magendo yaipotezea Serikali Sh15 bilioni kwa mwaka - Biashara - mwananchi.co.tz





 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…