Sasa Bangi kuwa zao rasmi la biashara Tanzania

Sasa Bangi kuwa zao rasmi la biashara Tanzania

wazunguwawili

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2019
Posts
3,984
Reaction score
4,132
Spika aongoza wabunge kuunga mkono.

Mabeberu wanahitaji zaidi hili zao,hasa CANADA.

Uganda wapewa USD500M kutoka EU kuendeleza zao la bangi.

Angalizo.

Tusiwaamini sana mabeberu kwa uhitaji wa hili zao la bangi. Kama vp walime wao maana wanayo ardhi.

Siku wakigoma kuinunua bangi na kauli za wanasiasa wetu ambazo husema "tule/tuvute" wenyewe sijui itakuwaje hiyo siku.
20200206_171633.jpeg

=====
Dodoma. Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene kuwaruhusu wakulima wa bangi kuiuza katika kipindi cha miezi sita.

Amesema kwa sasa wapo wakulima wa bangi wanaoshindwa kuiuza kwa kuwa kilimo hicho hakiruhusiwi nchini, na kutaka ambao wamelima zao hilo kupewa msamaha wa miezi sita ili waweze kuuza kabla soko la zao hilo kuporomoka.
Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 3, 2020 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa kamati za Bunge.

Mara kadhaa mbunge huyo amekuwa akiitaka Serikali kuruhusu kilimo hicho kwa kuwa bangi ina soko kubwa ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumzia kauli ya mbunge huyo, Spika Job Ndugai ameitaka Serikali kuangalia jambo hilo kwa mapana kwani nchi ya Canada inapata fedha nyingi kupitia zao hilo.

Hoja ya mbunge huyo ikiwaibua mawaziri Angellah Kairuki (Uwekezaji) aliyesema kuna mwekezaji anayetaka kuwekeza katika madawa ya kutumia mbegu za pamba huku Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akisema Tanzania haina sheria ya kuruhusu kilimo cha bangi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja na mimi nijifunze kidogo kidogo kuvuta ili niingie lasimi kwenye hiki kilimo maana haiwezekani mtu uje ulime mahindi halafu ushindwe kula hata muhindi wa kuchemsha kujua zao lako ni bora au la.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku chache zilizopita nimesikia Bungeni wakijadili kuwa kuna wawekezaji wanakuja kulima bangi kwa ajili ya mafuta. Good idea!

Lakini vipi tumeandaa jengo la kuwahifadhi warukwa akili?

Kwa sasa bangi si halali na ukikamatwa unakula mvua nyingi tu jera. Lakini pamoja na kutokuwa halali mtaani kuna warukwa akili wengi ambao inasemekena ni kwa sababu ya matumizi ya Bangi.

Binafsi ninaona kuruhusu bangi kwa sasa ni kwenda kuruhusu taifa la vichaa wengi watakao vuta bangi wakidhani wanapunguza stress. Vijana wengi mijini mwili imeregea mithili ya matete kwenye maji shauri ya bangi, sasa naona tunaanza kuandaa taifa la mazobe wengi, vibaka wengi, matahira wengi na kupoteza nguvu kazi.

NINATANGULIA MARA
 
Shame on you.
Mpuliza Bange/Bangi hata siku moja hawezi kuwa legelege, kibaka wala mwehu.

Anayekuwa hivyo ni anayechanganya Bange, mirungi na pombe kali mfano Gongo ya kiwandani (Konyagi)
Huu ni mwaka wa 17 navuta Bange ila sina hayo matatizo mpaka crewe members wenzangu wote wako fresh tuna ufanisi mahala tuliko, show za sita kwa sita ni balaa, nina nguvu nyingi kupita maelezo kwa sababu nikila vyakula vyepesi sishibi kabisa.

Ubwabwa kilo moja si jambo kabisa kwangu
 
Eliud Ndabila Mwenyezi Mungu akupe kila lililo jema. Hakika kukubali kilimo cha bangi ni mkakati wa kuangamiza taifa:

- China walipiga marufuku kilimo cha bangi miaka ya zamani kwani waliona madhara yake makubwa kwa jamii yao.

- Maeneo mengi nchi hii yanayolima na kutumia bangi huwa kuna uhalifu wa kutisha; rejea Tarime, Njombe, maeneo ya Mpwapwa Dodoma n.k.

- Naona tumeichoka amani. Vijana wenye misongo ya kutokuwa na kazi na bangi iizwayo holela ni mazalia ya VURUGU. Rejea hali ya usalama nchini kabla ya mwaka 2016. Tutegeme maandamano yasiyo kwisha kudai haki za makundi mbalimbali
Serikali iwe tayari.

- Usalama wa raia na mali zao utakuwa mashakani

- Magonjwa ya akili kwenye jamii yataongezeka.
Je, tuko tayari kuangamiza sehemu ya jamii kwa akili ya tamaa ya fedha kwa watu wachache.

Elius W Ndabila,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna shama kama ekari tatu aliniachia babu nadhani litakuwa muruwa kwa hichi kilimo adhimu.
 
Shame on you.
Mpuliza Bange/Bangi hata siku moja hawezi kuwa legelege, kibaka wala mwehu.

Anayekuwa hivyo ni anayechanganya Bange, mirungi na pombe kali mfano Gongo ya kiwandani (Konyagi)
Huu ni mwaka wa 17 navuta Bange ila sina hayo matatizo mpaka crewe members wenzangu wote wako fresh tuna ufanisi mahala tuliko, show za sita kwa sita ni balaa, nina nguvu nyingi kupita maelezo kwa sababu nikila vyakula vyepesi sishibi kabisa.

Ubwabwa kilo moja si jambo kabisa kwangu
Naunga mkono hoja nashangaa hii mijitu inayosema bhangi ina madhara.
 
Bangi haina madhara mengi kama sigara,ihalalishwe tu ili serikali ipate mapato.Maana ni zao lenye soko kubwa sana huko marekani na Ulaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom