Wewe kama ni mmiliki wa Channel ya YouTube au mmiliki wa Website na unapata pesa kwa njia ya Google Adsense basi jua sasa hivi TRA wanakata Kodi mpaka huko YouTube na kwenye Websites kwa pesa unayokusanya kupitia Google AdSense. Hivyo uwezi kutoa pesa mpaka uwe na TIN namba pia, tofauti na zamani Google walikuwa wanataka kitambulisho cha NIDA, Leseni ya udereva na Passport tu na anuani ya makazi.
Ila mpaka mwaka huu 2025 naona TRA wamekuwa makini na kuongeza ukusanyaji kodi mpaka mitandao, na hii haina muda mrefu sana itakuwa imeeanza miezi ya June, July, August au September hapa katikati, maana mimi mwezi May 2025, nilichukua pesa Google AdSense bila kuombwa TIN Number. Leo nimepita kuangalia naona wanaomba niweke TIN Number au namba ya mlipa Kodi au cheti cha mlipa Kodi.
Ngoja waje wajuzi wa mambo... TRA inakusanya sasa hivi kodi kila eneo... mpaka inataka mawinga walipe kodi cha kushangaza mbona hatusikii pato la nchi kuongezeka...
Kodi ni muhimu sana ili kufadhili shughuli za serikali, huduma kwa umma kama vile barabara na mashule, Usalama wa Jamii, Afya na Mengineyo.
Sasa kama hata hayo kuanzia Elimu (Mikopo na Shule Binafsi); Afya tuna BIMA ya Afya na kulipia Private; Kuhakikisha wafanyakazi wanalipwa ujira stahiki hilo pia limekwenda kwenye free market...; Usafiri tuna watu binafsi n.k.; Ujenzi wa Barabara tunafanya PPPs which means hata gharama ya kulipia hio Miradi tutalipa kwa levies na tolls.
Mbaya zaidi huduma nyingi za watu binafsi gharama imekuwa kubwa sababu ya Tozo za Serikali (mfano bila Tozo; bundle...
Kuna Notion kwamba Watu hawalipi Kodi, na bila kuongeza vyanzo kwa kuwakamua zaidi Nchi haiwezi kuendelea...
Kwanza kabisa sio kweli kwamba watu hawalipi Kodi; kila mtu analipa Kodi indirectly na kutokana na vyanzo vyetu na Tozo tunaweza kuendesha nchi hata bila Kodi ya Mapato; Nikitoa Scenario moja tu ya Makusanyo ambayo mtu analimwa; Kila ukitoa Pesa kwenye Simu, Serikali Inakula, Wakala akipata faida yake Serikali inakula; Kampuni kwenye faida yake Serikali inakula..., na kwa kula kwote huku hakuna value for money inayopatikana..., Kila halmashauri kuna makusanyo yanafanyika ya...
NB: kutoka Google - Yes, you need to pay taxes on your Google AdSense income, as it is considered taxable income. It's important to report all earnings to the tax authorities in your country.